Congo crisis. Imeandikwa na Malisa GJ

#PART4

Baada ya Ntaganda kupelekwa The Heague, M23 iliongozwa na Sultan Makenga, Mtutsi wa Rutshuru huko Kivu Kaskazini. Mwaka 1990 Makenga akiwa na miaka 17 tu alienda Rwanda kujiunga na kikundi cha waasi RPF kilichokuwa kinaongozwa na Jenerali Fredy Rwigyema. Sultan Makenga akiwa askari wa RPF alipigana msituni dhidi ya serikali ya kihutu ya Juvenile Habyarimana.

Baada RPF ilishika dola, Askari wote wa RPF waliingizwa katika jeshi la Rwanda akiwemo Sultan Makenga. Alihudumu katika jeshi hilo kwa muda mrefu hadi kufikia cheo cha Kanali kabla ya kurudi "nyumbani" Congo, kujiunga na kikundi cha waasi cha CNDP. Baada ya mkataba wa amani wa March 23, 2009 Sultan Makenga alikuwa miongoni mwa askari 600 wa CNDP waliokataa kujiunga na jeshi la Congo (FARDC).

Mwaka 2012 Bosco Ntaganda alipojitoa kwenye jeshi la Congo na kuunga kikundi cha waasi cha M23, Sultan Makenga alikua wa kwanza kujiunga. Baada ya Ntaganda kujisalimisha, Makenga akapewa uongozi wa M23. Akaongoza kuanzia 2013 hadi 2016 kisha akaachia uongozi na kuhamia uhamishoni nchini Rwanda. July 2024 Makenga alizungunza na media kwa mara ya kwanza akiwa Kigali na kueleza bado ana azma ya kuikomboa DRC.

Baada ya Makenga, M23 ikapata viongozi ambao hawakuwa mashuhuri hadi 2022 ilipompata Corneille Nangaa, aliyekua Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi (CENI) na ndiye aliyemtangaza Tshikeshedi kuwa mshindi wa kiti cha Urais kwenye uchaguzi wa December 30 mwaka 2018.

Katika mambo yanayoshangaza na kufanya vita ya Congo kuonekana ngumu, ni jinsi Nangaa alivyotoka kuwa Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, hadi kuanzisha coalition ya vikundi vya waasi, Congo River Alliance (CRA) na kuingiza M23. Nangaa ndiye ameongoza M23 kuutwaa mji wa Goma January 2025, na kuyafurusha majeshi ya serikali. Nangaa ametangaza nia ya kumuondoa madarakani Rais Tshisekedi, ambaye mwaka 2018 alimtangaza kuwa Rais.

August 2024 Mahakama ya kijeshi mjini Kinshasa ilimhukumu Nangaa adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa kosa la uhaini. Hukumu hiyo ilitolewa bila yeye kuwepo mahakamani (death sentence in absentia). Nangaa amesema ikiwa M23 itashika dola, wale waliomhukumu ndio watanyongwa kwa niaba yake.!

Itaendelea.... (popcorn zisiishe).!
 
Mapatano alikuwa anasema mpiganaji mmoja juzi ni kwamba kwa kumuondoa Mobutu Rwanda itapewa North and South Kivu na Uganda itapewa Ituri..
Lakini kama watu wandaiana malipo kama hayo,it is something that can be estimated and calculated.
Nakumbuka wakati ule Tony Blair alipokuwa Waziri Mkuu siku moja ilitangazwa," Leo Uingereza imelipa installment ya mwisho ya deni lake kwa USA kwa msaada iliopata WW2"
 
Good luck
 
haaaaaaa pandora box hiii ....huu mgogoro ni mkubwa sana damu za watu zilizwamwagwa hapa hii nchii haiwezi tulia labda ikatwe iwe ndogo ndogo ila kwa ukubwa huo haiwezi tawalika
Damu inamwagika ili familiya za kagame na mseven ziishi Kama peponi...hao wanajeshi nao NI wajinga wanashindwa kumtwanga kagame warudi kwao Rwanda Kama anawapenda kwa Nini haearudiahi nyumbani Kigali..wanataka Kongo isiyo yao...
 
Damu inamwagika ili familiya za kagame na mseven ziishi Kama peponi...hao wanajeshi nao NI wajinga wanashindwa kumtwanga kagame warudi kwao Rwanda Kama anawapenda kwa Nini haearudiahi nyumbani Kigali..wanataka Kongo isiyo yao...
kagame ni moja ya matatizo hata yeye akifa sasa hivi hii vita haiwezi isha miaka 1000.....kuna vikundi vidogo zaidi ya 100 na nchi ni kubwa sana na maliasili ni nyingi na dunia nzima inafaidika ila wakongo ndo wanapata hasara maamuzi yafanyike kwa maslahi ya wakongo
 
Survival for the fitness

Ova
 
Hivi haikuwa kipindi Cha Donald Cameroon
 
#PART5

Baada ya M23 kuitwaa Goma walidai hawana mpango wa kuchukua miji mingine. Jeshi la Congo (FARDC) likarelax. Kumbe ilikua mbinu ya kivita. Ghafla M23 wakavamia na kuuteka mji wa Rutshuru wenye utajiri wa dhahabu, tin na Tungsten na mji wa Masisi wenye utajiri wa dhahabu na cassiterite.

Mpango wa M23 ni kufika Kinshasa na kuuangusha utawala wa Rais Felix Tshisekedi. Madai ya M23 ni yaleyale ya siku zote, ambayo ni kulinda maslahi ya Watutsi waishio mashariki mwa nchi hiyo, kupambana na wanamgambo wa Kihutu wa FDLR (Interahamwe), na kutaka Banyamulenge watambuliwe kama raia halali wa Congo.

Mzozo wa mashariki mwa Congo umegharimu maisha ya mamilioni ya watu toka ulipoanza. Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umepeleka askari wa kulinda amani. Ikumbukwe askari hao hawapigani upande wa serikali wala wa waasi. Kuna watu wanadhani askari wetu wa JWTZ walioko Congo wanapigana upande wa jeshi la serikali (FARDC). Hapana. Hawapigani upande wowote. Wanalinda amani. Lakini ikitokea kuna upande unahatarisha amani utapewa haki yake ya kikatiba.

Kwa mfano, mwaka 2012 Umoja wa mataifa uliunda jeshi la kulinda amani Congo (MONUSCO). Ndani yake kulikua na brigedi maalumu ya kunyang'anya silaha makundi ya wapiganaji - Force Intervention Bregade (FIB). Brigedi hiyo iliundwa na askari kutoka Tanzania, Malawi, Afrika Kusini na Uruguay.

April 2012, M23 wakashambulia kambi ya FIB iliyokua Rutshuru na kuua askari watatu. Aliyekua Mkuu FIB, Jenerali James Mwakibolwa alipanga vikosi vyake kujibu mapigo. M23 walichakazwa vibaya na zaidi ya askari 600 wa M23 waliuawa na wengi kujeruhiwa. Walipigwa bila huruma na kuachia miji yote waliyokua wameishikilia ikiwemo Rubaya, Kitchanga na Rutshuru. Askari 16 wa FIB nao walipoteza maisha.

Bosco Ntaganda akakimbilia Rwanda kujisalimisha ubalozi wa Marekani. Alipelekwa ICC akahukumiwa miaka 30 na sasa anatumikia adhabu gereza Leuze-en-Hainaut huko Ubelgiji. Sultan Makenga alirithi mikoba ya Ntaganda lakini nae alitandikwa na ilipofika March 2013, M23 walisalimu amri. Moja ya makosa ambayo Makenga anayajutia hadi leo ni kuingia kwenye 18 za FIB iliyokua inaongozwa na Jenerali James Aloizi Mwakibolwa.

Kumekua na jitihada mbalimbali za kumaliza mgogoro wa DRC kwa njia za kidiplomasia ikiwemo mkutano wa viongozi wakuu wa SADC na EAC uliofanyika leo jijini Dar.

#MyaTake:
1. Congo imeponzwa na ukarimu wake. Wakati wa vita vya Rwanda, Congo ilipokea Watutsi wengi na kuwapa hifadhi, akiwemo Kagame. Baada ya utawala wa Habyarimana kuangushwa Wahutu nao wakakimbilia Congo na kupewa hifadhi. Sasa hicho kimekua kigezo cha Rwanda kuingiza majeshi Congo kila mara kwa madai ya kuwatafuta Wahutu wa FDLR. Kwa lugha rahisi vita ya ndugu wawili (Wahutu na Watutsi) iliyopaswa kupiganwa Rwanda sasa inapiganwa Congo.

2. Congo inateswa na mipaka ya kikoloni. Laiti wakati wa kuchora mipaka jamii yote ya Watutsi ingewekwa Rwanda, leo kusingekuwa na Banyamulenge Congo, kwahiyo Watutsi wasingepata sababu ya kuishi Congo na kujifanya raia. Ni sawa na kukuta Wamasai 1,000 pale Longido, halafu uambiwe kati yao wapo wa Kenya. Utawajuaje? Utawatofautishaje?

3. Congo inateswa na rasilimali zake. Kama eneo la Kivu lisingekuwa na utajiri, mgogoro usingekuwa mkubwa kama ulivyo. Rejea #Part1 kujua utajiri uliopo Kivu. Kumbuka bila Kivu dunia haina laptop wala smartphones kwa sababu 80% ya coltan yote duniani inatoka Kivu.

4. Rwanda na Uganda ni Keyplayers kwenye mgogoro wa Congo. Kwa miaka mingi majeshi yao yameigeuza Congo shamba la bibi. Waondoe majeshi yao Congo.

5. Viongozi wengi wa M23 ni Wanyarwanda. Huu ni udhibitisho kuwa Rwanda ni kinara kwenye mgogoro huu.

6. Congo ni kubwa sana na hivyo inakosa jeshi imara la kutosha kulinda mipaka yake yote. Congo ni kubwa mara 90 ya Rwanda. Wapo wanaoshauri igawanywe kama njia ya kutatua mgogoro. Kama ambavyo Yugoslavia iligawanywa na kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe.

7. Kiongozi wa sasa wa M23 Corneille Nangaa alikua Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi 2019 na ndiye aliyemtangaza Tshisekedi kuwa Rais kwa ushindi wa 38%. Lakini alilaumiwa kupunguza kura za Martin Fayulu aliyepata 34%. Huenda kuna ahadi alipewa haikutimizwa ndio maana akaungana na Waasi.

Sababu hizo hapo juu zikifanyiwa kazi, mgogoro wa Congo unaweza kupungua kwa kiasi kikubwa. Mnaopenda kujifunza zaidi, naandika Kitabu. Get ready to have your copy. MWISHO.!
 
Malisa ni mwandishi mzuri sio kama chawa wa Mbowe ndugu Yericko. Yeye kitu kikitokea anadai tayari alishaelezea kwenye kitabu chake cha ujasusi.
 
Halafu anakuja mtu ameshiba makande anakwambia Kagame hahusiki. Nimempuuza sana PLO Lumumba
Kwa hisia rahisi tu, Kagame anahusika kwa sababu asipofanya hivyo, walw Banyaamulenge wakifurushwa huko Mashariki ya DRC watarudi Rwanda wakati ardhi ni ndogo. Kagame anaendelea kuwapambania wabaki huko huko DRC ili angalau hata awe anawatumia kupata chochote kitu madini
 
Noma sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…