Mkandara,Invisible,
Mkuu hata sielewi mahusiano ya kichwa cha habari na maelezo uloyatoa hapa..Sioni uhusiano wa Zitto na habari hii ikiwa wananchi wenyewe wa Kigoma hawatahusika zaidi ktk mjadala huu. Ni wao wanaofahamu uwakilishi wa Zitto kama mbunge wao na kaweza yepi.
Binafsi Zitto namtazama kama mbunge wangu wa Upinzani hivyo sifa zake zinatokana na uwakilishi wake wa hoja za upinzani ndivyo navitazama zaidi mathlan swala la Buzwagi, na mikataba feki lakini anapokuja kupendekeza tena mkataba feki mwingine inaondoa nguvu kubwa ya sifa alovuta wakati wa Buzwagi. Kwa sababu hata mkataba wa Buzwagi ungetuwezesha kuvuta japo kidogo hizo asilimia 3 na zikapunguza matatizo yetu, pia wakazi wa Buzwagi ambao wanahitaji sana huduma za Shule, Zahanati, Maji safi na Umeme wangeweza kupata japo kiduchu..Barrick wangeweza kuondoa tatizo hilo la wakazi wa Buzwagi nikitumia mtazamo wake ktk swala la Dowans..
labda zitto ni mbunge wa "tanzania yote"
btw ... nani kaendesha hii poll?
Purely UDAKU.Kwanza nimpongeze Zito, pamoja na weote walioonekana katika hiyo watatu wanaomfuatia.
Lakini hapa ndipo panapokuwa na matitizo katika design ya utafiti kama huu. Swali, unapolielekeza kutafuta mbunge aliyefanya vyema, halafun ndani yake unchanganya na mawaziri, ni lazima utapata matokeo yanayoegemea upande mmoja (biased). Waziri anawakilisha serikali, na mara nyingi wananchi inawawia vigumu kupima watu hawa 2 katika mizani moja. Ingekuwa ni waziri yupi aliyekonga nyoyo za wananchi, na ni mbunge yupi aliyekonga nyoyo za watu. Vingenevyo ni kutowaweka mawaziri katika mizani wanayostahili.
Jambo jingine, katika hizo kurasa 2 haijaelezwa kuwa watu waliohojiwa walipatikana kwa utaratibu upi, ambayo nayo kitakwimu inaweza kuwa na matatizo kufanya tathmini wakilishi.
Purely UDAKU.
labda zitto ni mbunge wa "tanzania yote"
btw ... nani kaendesha hii poll?
Kwenye utafiti kama huu, ni watu wachache tu, sio rahisi uwahusishe watanzania wote, ama sivyo itakuwa uchaguz wa rais.
Pili hii haina ubishi wala hailazimishi kila mtu akubaliane nao.
So, wote mnaopinga, aidha mfanye zenu, kuna mtu anasema bunge la Tanzania halina wabunge kabisa!!!! yet anasema , mbunge Zito ni wa Kigoma!!!!
Kuna ubishi ambao hauna msingi , ili mradi kuonekana unabisha,
kuna tatizo gani akiwa mbunge wa TZ yote
Waberoya,
Mkuu punguza jazba hii kitu haikukaa sawa kabisa. Hata Redet wana afadhari mara 10 ya kitu hii maanake hatuwezi kumpongeza Zitto kwa sababu tu yeye ni wa kwanza na amepata kura asilimia 25 yaani kati ya watu 100 ni 24 tu waliompitisha. haya ni matusi makubwa kwa kiongozi huyo.
Na ukitazama mwisho wa hizo kura utaona kisanduku kinachosema DKNone chenye asilimia 24..nikichukulia pengine ndio kusema Hakuna mbora which includes Zitto mwenyewe..hii ni dalilimbaya sana kwa wabunge wetu, labda iwe haina maana hiyo.
Kisha tazama maswali yaliyoulizwa basi, ni vitu ambavyo vinatokana na magazeti yaani sifa ambazo tunaweza kumpa mbunge ni zile tulizozisikia toka magazetini zikilenga umaarufu wa mtu..Wangesema hivyo basi kuwa hapa tunatazama umaarufu wa mtu na sii swala la kuchaguliwa ama kufanya mazuri bungeni wakati hatufahamu kabisa nani kafanya nini bungeni zaidi ya scandals za utawala huu..
Hata hao REDET hutoa takwimu za Umaarufu wa Kikwete na kwa sababu yeye ni rais wa Tanzania nzima binafsi napokea takwimu zao kama somo hata kama kuna makosa ya utekelezaji wake. Labda nikufahamishe kidogo nilichoelewa mimi upate kuona wapi nazungumzia..
Kwanza, sifa za mbunge kulingana na point walizo score.. Ya kwanza ambayo imepata kura nyingi inasema nini?..I am not keen on the issue or the name of the minister! hii wamevote kwa asilimia 19...ipo juu kabisa ya kura zote na sijui kuna ubora gani wa kiongozi yeyote zaidi ya kutupoteza kabisa..ya pili inayofuata inasema He fights for the poor!- kivipi mkuu wangu and who are the poor! Je, ni Wananchi, Walalahoi au wanatafuta mbunge mwenye mtazamo wa siasa za Kijamaa kugawana umaskini.
Hilo tuachane nalo twende mbele zaidi..
Shuka chini ktk hesabu ya Wabunge wanaotegemewa kurudi bungeni utakuta ni asilimia 42 swali la kwanza linasema - Careless in his work, hapo wame vote kwa asilimia 22 juu ya kila kipengele cha uchaguzi wa wabunge hao watakao rudi bungeni. Mimi mkuu wangu sielewi hapa wanaposema Careless on his work, wana maana gani kiasi kwamba iwe sifa ya kwanza kumrudisha mbunge..laa sivyo ni ashirio tosha kwamba hatuna wabunge wa maana (the are all negligent) kwa asilimia hiyo 19, hii sio sifa hata kidogo..
Hata hivyo naomba darasa mkuu wangu ikiwa mimi ndio sikuelewa... karibu