Kha! Halafu nimekawia bila kwenda hayo maeneo ya Upperhill na kuna uwezekano mwaka utapita kabla sijaenda, hebu waza nitakavyokenua meno kuona dubwasha lote hili limeibuka na linatumika ilhali sikuliacha, naona nikigeuza geuza gari kwenda na kurudi ili kufurahia utamu wake.
Kwa wenzetu wa kusini naomba niwape mfano wa nini kinajengwa hapa, watu wa Dar hebu hapo mlipo muwaze barabara ya juu imejengwa kutokea Usalama kule Magomeni, ikakatiza Jangwani pale kwa Yanga na kushukia kituo cha Fire.