Shipping container zipo za sizes tofauti kuanzia
60ft
View attachment 3121333
53ft
View attachment 3121336
48ft
View attachment 3121370
45ft
View attachment 3121373
43ft
View attachment 3121374
40ft
View attachment 3121377
35ft
View attachment 3121385
20ft
View attachment 3121381
15ft
View attachment 3121378
10ft
View attachment 3121382
7ft
View attachment 3121383
Swali langu jee, Container za angalau 45ft bongo zinafika? Kama ndio, napata wapi? kama hazifiki inaweza kuwepo option ya kuagiza, jee kuna semi trailer truck zenye chassis ndefu size hio ili kulibeba? Wapi napata?
Mara chache naonaga Sem trailer imebeba container Bila shaka 40ft lakini kuna nafasi kidogo nyuma imebaki, jee ndio hayo?
Habari Mkuu,
Mimi binafsi nikijihusisha na biashara ya new and used containers kwa almost miaka 6 sasa
Nina haya machache ninayoweza kusaidia
1. Container zaidi ya 40Ft kwa sheria zetu za Barabarani zinawekwa as Abnormal Load, hivyo bila kujali ya uzito uliobeba utapaswa kulisafirisha kwa escort ya magari mawili.
Moja liwe mbele ya gari lililobeba Container na jingine liwe nyuma
Yote yakiwa na bango litakalosomeka "Abnormal Load"
2. Magari ya kubebea container zaidi ya 40Ft yapo japo si mengi.
Kuna kampuni chache zenye huduma mfanano na hiyo na gharama zao hazina afueni kwa mteja wa matumizi ya kawaida
Eg. Raphael Logistics hutoza Tsh 1.5M kubeba 40Ft kwa Boxloader toka Kurasini: Temeke hadi Kibaha
Wakati huo huo kwa Flatbed ya kampuni ya kawaida hawatokutoza zaidi ya Tsh 500 000 ukijumuisha na gharama za crane offloading ni Tsh 100k kwa container.
Jumla unakuwa umetumia Tsh 600k badala ya ile ya Tsh 1.5M kutoka kwa kampuni zinazofanya heavy lifting as Raphael Logistics, Mariam Hauliers, Mainline Carrie etc
3. Bei ya Sasa ya containers kwa 40Ft na 20Ft
40Ft Container (HQ/HC)
New (Jipya): Tsh 17M (inclusive)
Used: (Exclusive VAT)
Grade A: Tsh 7.5M
Grade B: Tsh 7.3M
Grade C: Tsh 7M
Lower Grade C: Tsh 6.85M
Used 20Ft (Standard)(Exclusive VAT)
Grade A: Tsh 4.5M
Grade B: Tsh 4.3M
Grade C: Tsh 4M
Lower Grade C: Tsh 3.85M
Grade D: Tsh 3.6M (huwa zinakuwa chache)