Sifahamu, ni tatizo la kiufundi, mifumo mbovu au mazingira ya rushwa? Ukitaka kufanya malipo kwenye taasisi hizi za umma kama Tanesco, Duwasa kwa Dodoma na nyingine kama hizo, ili upatiwe huduma husika imekuwa ni shida sana kupata 'CONTROL number' kwa ajili ya kufanya malipo. Mara nyingi watoa huduma hawa wamekuwa wakisingizia kutokuwepo kwa mtandao (Network inasumbua!).
Kumbe Tanzania kuna tatizo kubwa hivi la kimtandao kwenye taasisi za umma za kukusanyia mapato ya serikali!? Control number inachukua hadi wiki kuipata, na hapo uwe umefuatilia kweli kweli hadi kwa kwenda physically ofisini!
Serikali inapataje pesa kama mifumo ya kukusanyia pesa inakuwa na shida kiasi hiki!? Hebu Watanzania (hasa watendaji wa taasisi za serikali) tubadilike na tuweke mifumo yetu vizuri ili wananchi tukitaka kulipia huduma za umma kusiwepo na visingizio vya mtandao, control number zitoke kwa haraka watu walipie huduma, Serikali ipate pesa kwa wakati na ninyi watendaji mlipwe mishahara kwa wakati! Kha, ni hatari sana, badilikeni.
Nashauri kwa taasisi za serikali zinazo husika na utoaji wa huduma zinazoendana na ukusanyaji wa mapato ya serikali, mishahara ya wafanyakazi wao itokane na makusanyo kutoka kwa wateja labda wafanyakazi watawajibika na kuwa wepesi kuwahudumia wateja.