Hakuna scientific prove ambaye amewahi thibitisha kuvuta bang kunasabisha kichaa, kama unazo zilete tuzione
BAADA ya kuwepo kwa baadhi ya tafiti
zilizokuwa zikiruhusu uvutaji wa bangi
kwa madai kwamba ilisaidia wagonjwa
waliosumbuliwa na msongo wa
mawazo, hali hiyo imesababisha baadhi
ya nchi kuruhusu matumizi yake.
Pamoja na mawazo ya wengi kufikiria
kuwa kutokana na nchi ya Jamaica
ndiyo ilikuwa mstari wa mbele kwa
watumiaji wengi ingekuwa ya kwanza
kuruhusu bangi, lakini ukweli ni kwamba
nchi ya Canada
ndiyo ilikuwa ya kwanza kukubali bangi
kutumiwa kama dawa ya maradhi.
Baada ya utafiti huo wa awali hivi
karibuni watafiti wengine wamegundua
kuwa matumizi ya bangi kwa muda
mrefu yanasababisha kujiongezea
madhara badala ya kutibu kama
ilivyokuwa ikisemekana hapo awali.
Watafiti hao wamekwenda kinyume na
wale wa kwanza kwa kusema kuwa
matumizi yake yana uwezekano
mkubwa wa kumletea mtumiaji
magonjwa ya kupungua uzito mara kwa
mara, magonjwa ya figo, ini na ugonjwa
wa akili.
Watafiti waliogundua athari hizo ni wale
wanaotokea nchini Australia ambao
katika utafiti wao wamegundua kuwa
zaidi ya vijana 3,100 walio katika umri
wa miaka 20 ndio wamekuwa watumiaji
wakubwa wa bangi.
Utafiti wao umekwenda mbali na
kubaini kwamba asilimia 18 ya vijana
hao ni wale waliojiingiza katika
matumizi ya dawa hizo za kulevya kwa
muda wa miaka miwili au mitatu.
Asilimia nyingine 16 ya vijana wa umri
huo wamebainika kutumia kwa muda
wa kati ya miaka minne hadi mitano.
65 kati ya watumiaji wamegundulika
wameshaathirika na maradhi ya
ugonjwa wa akili.
Wakati hao wakisumbuliwa na tatizo
hilo wengine 233 wamebainika
kuathirika kwa figo na ini.
Watafiti wamebaini vijana wengine kati
yao wanasumbuliwa na tatizo la kupata
uchizi (wehu).
Baada ya kubaini hayo watafiti
wametoa ushauri kwa vijana kutotumia
dawa hizo za kulevya kwa vijana kwa
zaidi ya miaka sita au zaidi tangu pale
siku ya kwanza alipoanza kutumia.
Wanasema kuwa kwa wale ambao sasa
wamevuta kwa muda mrefu kati ya
miaka 15 na zaidi wengi wao
wamekumbwa na tatizo la kiakili.
Kwa mujibu wa Dk. John McGrath, wa
kituo cha uchunguzi wa afya ya
wagonjwa wenye mtindio wa ubongo
cha Queensland, nchini Marekani,
anasema: "Wengi wa wagonjwa ambao
wamekumbwa na matatizo hayo
tumegundua ni wale waliowahi kutumia
bangi kwa muda mrefu na hatimaye
kujikuta wakipata tatizo la akili."
Daktari huyo anasema kuwa ni nadra
sana kukutana na wagonjwa wa akili
vijana halafu wakawa hawajawahi
kutumia bangi, iwe mwaka mmoja au
zaidi.
Anasema kuwa iwapo matumizi ya
bangi yatakomeshwa tatizo la vijana
kupata matatizo ya utaahira
yatapungua kwa kiasi kikubwa duniani...
Nimekopi kwa post ya
MziziMkavu
https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/288102-madhara-ya-bangi.html