Copa America 2021 Final: Argentina Vs Brazil

Copa America 2021 Final: Argentina Vs Brazil

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Usiku wa leo, Katika dimba la Maracana pale Brazil, kutapigwa mchezo wa kukata na shoka kati ya Argentina Vs Brazil kuanzia saa 9:00 Usiku kwa masaa ya Afrika Mashariki.

Mara ya mwisho Argentina kutwaa ubingwa huo ni mwaka 1993 wakati Brazil ni bingwa mtetezi.

Brazil imeandaa michuano hiyo mara 5 na imefanikiwa kushinda mara zote 5 iliyoandaa.

Lionel Adreas Messi, nahodha wa Argentina, Mchezaji bora kabisa katika michuano hii, je ataweza kuiongoza Argentina kutwaa michuano hii? Ikumbukwe katika mechi zote walizocheza katika michuano hii, Messi amefunga au kutoa assist katika kila mechi.

Hii ni nafasi ya mwisho kwa Lionel Messi kuweza kutwaa ndoo akiwa na Argentina, je ataweza? Tusubirie tuone.

NB:
Fuatilia mechi hii kupitia Hesgoal.com
Muda ni saa 9:00 Usiku
Tukutane hap muda huo...

A47A5D95-0D96-43B3-B8AF-EC538375C935.jpeg
 
Jamani hivi kwa wenye Dstv kuna chaneli gani ya kawaida naweza ona hii mechi ukiondoa zile za package ya juu??

Hii copa dstv hamna popote mkuu
Nina premium, huwa naishia kukesha na sion chochote 😀

Azam yaleyale😀😀😀😀

Star times nimekesha siku moja nikambulia kuona replay Badala ya live mech in progress 😂😂😂😂

Sijuwi kwanini wanalibalia hili soccer la America ya kusin.....
 
Mie niko huku jirani na Malawi nina kidubwasha changu nililetewa na mshikaji wangu wa kinyasa ndicho kinanipa hii burudani kubwa. Baada ya kukipenda nilimuomba aniletee kama 10 kwa ajili ya washkaji zangu akaniambia havipatikani tena.

Mkuu tunatazama kupitia wapi

Muhimu sana tupeane maujanja
 
Mie niko huku jirani na Malawi nina kidubwasha changu nililetewa na mshikaji wangu wa kinyasa ndicho kinanipa hii burudani kubwa. Baada ya kukipenda nilimuomba aniletee kama 10 kwa ajili ya washkaji zangu akaniambia havipatikani tena.
😀😀😀🙌🙌🙌
🚶‍♂️🚶‍♂️🚶‍♂️🚶‍♂️🚶‍♂️
 
Back
Top Bottom