Corolla yenye 5A engine ni gari ya namna gani?

Sexer

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2014
Posts
8,440
Reaction score
8,149
Wakuu, Kuna jamaa anataka kuniuzia Corolla yenye muundo Kama wa harrier kiaina, engine 5a afu manual namba B, ushauri wenu hizi gari ni nzuri? Changamoto zake ni zipi?
 
Attachments

  • IMG20210222153151.jpg
    218.3 KB · Views: 48
Sasa gari no.B ndugu sa hiz tunaelekea no.E huoni kua huyo Jamaa yako anataka kukupambanisha akuuzie mkweche?
 
Engine za 5A utazikuta Kwenye Carina Ti pia ni engine ngumu Sana..... tafuta fundi wa uhakika acheki engine na gear box kama ziko vizuri
 
Tafuta fundi ukague kabla hamjauziana, hiyo ni moja ya injini Bora kutengenezwa na Toyota.

Chukua 5A haina shida imefanya vizuri Sana spea na mafundi wapo kila Kona.Usiogope maneno saizi watu wanaona 1NZ/2NZ za kwenye Vits/Runx/IST ndio kimbilio.
 
Nina gari namba B niking'oa namba plate halafu uweke namba D hakuna mtu wakubisha. gari ni matunzo tu
 
Tafuta fundi ukague kabla hamjauziana, hiyo ni moja ya injini Bora kutengenezwa na Toyota.

Chukua 5A haina shida imefanya vizuri Sana spea na mafundi wapo kila Kona.Usiogope maneno saizi watu wanaona 1NZ/2NZ za kwenye Vits/Runx/IST ndio kimbilio.
Kweli mkuu ninayo Corolla ya hiyo engine namba "C" sasa hivi ina miaka 7 toka nichukue sijawahi kujuta. Engine sijawahi kuigusa, mimi ni kubadili engine oil, matairi na other minor services.... Wese lita 1 inaenda up to 12km.... Halafu uzuri mwingine watu hawanisumbui kuniazima maana hawataki manual...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…