Unaonaje ukiziweka hapa hizo “basic precautions” ambazo Serikali inapaswa kuchukua? Labda hawazijuiNi kweli sisi sote hatutaki chanjo ya wazungu, lakini kwa nini sirikali haichukui zile basic precautions ili angalau kupunguza maambukizi?
Aibu sana !Mabibi na mabwana, hatimaye tuko hapa sasa:
Afrika CDC imeionya Serikali ya Tanzania kuhusu namna inavyoshughulika na corona.
Kwa mujibu wa matangazo ya DW mchana huu, Afrika CDC imeionya Serikali ya Tanzania kuwa kwa namna hii na hili la kutotoa takwimu za ugonjwa huu, Tanzania inaliweka bara zima la Afrika hatarini.
Tumesema ya kutosha sasa yetu macho.
Tusipoangalia tutamlaumu sana beberu.
Ama kwa hakika aliona mbali sana aliyesema "asilaumiwe dobi kwani kaniki ni rangi yake."
Ninawasilisha.
Unasemaje sisi sote hatutaki chanjo!?Mitaani vilio kila mahali. Ukiingia status za whatsapp huwezi kosa marafiki 2/3 wenye msiba.
Leo humu jf jerrybanks kafiwa na baba, baba mkubwa na mjomba kwa wakati mmoja.
Juzi nipo hospitali nikakutana na jamaa mmoja hapa Dar kamsafirisha dada yake toka Tanga aje atibiwe, kule Tanga walishazika ndugu zao 3 wa baba mmoja mama mmoja ndani ya wiki 1.
This is public irresponsibility and masaccre kwa sirikali iliyopewa jukumu la kuhakikisha usalama wa raia wake lakini wao wanachukulia for granted huu mlipuko.
Ni kweli sisi sote hatutaki chanjo ya wazungu, lakini kwa nini sirikali haichukui japo zile basic precautions ili angalau kupunguza maambukizi?
Ama kweri ukipenda chongo utaita kengeza.Onyo liko wapi hapo!
Mbona huko wanakotoa takwimu ugonjwa ndio unaongezeka?Ama kweri ukipenda chongo utaita kengeza.
Wewe umeona pongezi hapo?
Uzi mzima ni paraphrase ya taarifa kama ilivyotua kutoka Afrika CDC kupitia DW.
Kutokea Lumumba unadai CDC anayesema katoa onyo wewe unasema huoni onyo?
Ustake ncheke kama mazuri vile?
Uzuri mnatambua, kwenye hili hatuko nanyi.
Joni wewe huwezi na hautaweza kuliona kamwe.Onyo liko wapi hapo?!
Mbona huko wanakotoa takwimu ugonjwa ndio unaongezeka?
Nimekutukana tusi kubwa kuliko yote na linalouma sana,kimyakimya.Tanzania inaliweka bara la Africa hatarini? Huu ndio ukoloni tunaojaribu kuukataa. Yaani Africa CDC ni zao la ubeberu wa Marekani kupitia American CDC maana wamarekani katika network yake ya kukoloni dunia na kulinda/kutega maslahi ya Marekani na washirika wake imeinstall kibaraka chake inachokiita Centre for Disiase Control in Afrika.
Kwa namna waAfrika wasivyotembeleana huwezi kusingizia eti Tanzania inaiweka Afrika yote hatarini. Waafrika wengi wanazuru Ulaya na Marekani kuliko wanavyozuru miongoni mwao. So Africa CDC waseme tu ukweli kwamba wametumwa na maboss wao American CDC kwa malengo wanayoyajua wao.
Kama viongozi wetu walitumia kikombe cha babu ambacho hakikuwa na kipimo chochote cha kisayansi, wanatoa wapi nguvu ya kupinga dawa ya kimaabara?hebu waachane na sisi, watuthibitishie ni chanjo ipi ipo salama kuliko zote.