Corona: Afrika CDC yaipa onyo Serikali ya Tanzania

Eti hii ndio ile tanzania ilikuwa inahimiza UMOJA na MSHIKAMANO ingali yenyewe haitendi inachofundisha. Aibu kwa kweli.
 
SISI KAMA TANZANIA ....HATUITAMBUI CDC .......
 
Acheni kupotosha wasiokuwa na ufahamu. Hata hivyo siku moja mtawajibika tu.
Hii ndiyo itakayokuwa aibu kubwa kwao!

Najua mwongo kawaida hana aibu, lakini siku ya kuwajibika itakapowadia itapendeza kuona nyuso za hawa watu. Mimi ningependa kumwangalia usoni "mtu aliyeokotwa Jalalani".
 
Kwamaana hiyo CDC imeanzishwa kipindi hiki cha corona?? Na kimewalenga Watz pekee??
 
hebu waachane na sisi, watuthibitishie ni chanjo ipi ipo salama kuliko zote.

Chanjo watengeneze wao. Kote duniani wanaigombea hiyo chanjo.

Sasa liko toto tundu hapa lina koroma eti sasa lithibitishiwe ipi ni salama zaidi?

Hivi mmethibitisha hata ile juice ya bupeji kama hata inatibu tu achilia mbali ile ya kuwa salama?

Eti Mungu katuvusha. Eti hatuna wagonjwa wa corona.

Ujinga mtupu!
 
Nilopoona DW ndio chanzo cha habari nikaipuuza!
Pamoja na wewe kuwa ni mjinga wa CCM kama mlivyo wote, ungepuuza TBC ya CCM ambayo Watanzania wenye akili wameikacha na kuhamia DW, VOA na BBC ambazo ndo Taasisi za Serikali za mabeberu zinazotambulika, kukubalika na kuaminika kote duniani.
 
Mkuu unamkumbuka yule Meya wa Moshi aliyewaamuru Madiwani waliovaa barakoa wazivue?? Na wao wakatii amri bila shuruti.

Huu ni mkanganyiko uliosababishwa na serikali kwa kutotoa tamko.
 
Mkuu unamkumbuka yule Meya wa Moshi aliyewaamuru Madiwani waliovaa barakoa wazivue?? Na wao wakatii amri bila shuruti.

Huu ni mkanganyiko uliosababishwa na serikali kwa kutotoa tamko.
Hapana. Ule in uzwazwa wa wale madiwani. Hawakuwa na sababu yoyote ya kuvua barakoa kwa mkwara kidogo vile
 
Haina shida mkuu
 
Wewe nawe yafaa uipate Corona ndipo utaiheshimu! Kila siku na kushadidia haya masuala ya corona, ukiipata ndipo utatulia
 
Mwenyewe unajitakia uwe chini ya ukoloni, halafu unakuja hapa kupayuka juu ya mambo usiyokuwa na ufahamu nayo?
 
Kwa kutotoa uzito unaostahili, sipendi kutumia lugha hii, lakini hatuna namna, lazima tuseme:

RAIS MAGUFULI, KAMA ULICHAGULIWA AU ULIIBA KURA, HILO KWA SASA SIYO HOJA. CHA MUHIMU NI KUWA UNA WAJIBU WA KUWALINDA WATANZANIA BADALA YA KUWAANGAMIZA.

KWA KAULI ZAKO ZA UWONGO KWAMBA TANZANIA HAKUNA CORONA, NA HIVYO KUWAFANYA WATU KUAMINI KAULI ZAKO, NA KUACHA KUCHUKUA TAHADHARI, HAKIKA WEWE NI KIONGOZI MUUAJI.

Wale ambao maisha yao yangeweza kuokolewa kwa tahadhari, lakini wamekufa kutokana na uongozi wako mbaya, laana ikawr juu yako na uzao wako maana huna huruma wala chembe ya utu.

Nayaandika haya tukiwa tunasubiri mwili wa marehemu, mama wa rafiki yangu. Mimi nikiwa nimepoteza ndugu yangu hivi karibuni akiwa na dalili za kushambuliwa na covid 19, rafiki yangu, huu ni msiba wa 5 ndani ya wiki 3, wote wakiwa na dalili za kuathiriwa na Covid 19.

Ninyi mnaomshabikia Rais wakati akitenda uovu, zioneeni huruma familia zinazoomboleza kila siku kutokana na vifo vinavyosababishwa na corona.

Wakati wa majanga kama haya, we need mentally and spiritually strong leaders not muscular leadership.
 
Ninawatuhumu sana wenye ma STL, ma STL na wote wa namna hiyo.

Kwa kodi zetu dhahama la mikusanyiko linalotuhusu sisi kwenye madalala, mabasi, ma ferry, magulioni, masokoni nk wao haliwahusu. Wako salama zaidi na hii ni at our expense.

Nani kakwambia kupambana na corona inataka lockdown peke yake? Mbona kutwa kucha upotoshaji binadamu nyie?

Kwanini mnaling'ang'ania hivi hili hujui la kupambana na ugonjwa huu wakati weledi katika mambo ya afya hamna?

Ni kweli kuwa mkuu wa nchi hapendwi. Hili wakujilaumu ni yeye mwenyewe. Sababu za kutokupendwa kwake kuu kabisa ni namna anavyotusababisahia sisi kupotelewa na wapendwa kwa sababu ambao zingeweza kuepukika.

Hebu na abadilishe mwelekeo aone jinsi gani ile upepo wa mapendo utakavyobadilika!

Hii kitu mbona iko wazi mno?
 
Kweli Tanzania imefikia hatua ya kuzodolewa kimataifa? Ni Tanzania ile ya Mwl au Tanzania nyingine? Tanzania niliyoifahamu mimi ni ya kutoa ONYO mbele ya UN GEN. ASSEMBLY na sio hii ya kuzodolewa na CDC Afrika wajameni!
Siku zote mtu anapofokia nafasi ya kuwa kiongozi wa nchi huwa ameandaliwa, sio yale mambo ya sandakalawee!!ndio yametufikisha hapa!!huoni yaliowakuta zamu hii USA?!!kwa trump!!afadhari hata trump hakuharibu sana kwani kuna baadhi ya vitu alikuwa ana kwamishwa na mfumo!!lakini ile nchi ya porto rico, mbabe ni mmoja tu, nani aseme, yaani anafanya taifa kama mali yake, nasahau kuwa kuna mambo yanaongozwa kidunia, kutokana na makubaliano yaliyowekwa!!hivi kama angekuwa ndio kiongozi wa taifa kubwa duniani, ingekuwaje?!!lakini hayo yalijulikana toka miaka hiyo!!
 
Mimi ninaona labda serikali ingeanza na vitu viwili: 1) kutest na kupublish daily covid19 data. Atleast inaweza kuleta awareness na waliotest positive wanaweza kuwa isolated
Hii inaonyesha huna taarifa kamili kuhusu msimamo wa serikali.

"Unataka watu wafe kwa hofu"? Hilo ndilo jibu kama ulikuwa hulijui kweli!
Otherwise kila mtu anapaswa kuchukua hatua stahiki. Usingoje serikali kukwambia unawe mikono au kuvaa barakoa ukienda maeneo hatarishi
Wewe unaonaje serikali inapokwambia "Corona Hakuna"?
Unahimiza watu wafuate ya kwao na siyo yale inayotangaza serikali?
Ni nini maana ya kuwa na serikali?

Ukweli ni kwamba andiko lako lote hapo juu lilikuwa la kinafiki tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…