Corona: Afrika CDC yaipa onyo Serikali ya Tanzania

Ninamaanisha, sisi pamoja wewe tumtolee nani hiyo takwimu na nini sababu za kuwapa hizo takwimu zetu.

Sabubu za kutoa takwimu umeziandika kuwa ni janga la dunia. Nakubaliana nawe. Sasa je, mbona yapo magonjwa mengine ni janga la dunia na hatujambiwa tutoe takwimu zetu? Kwa nini corona tu!? Kuna kitu cha kufikiri hapa.

Serikali inazo takwimu zake kama ilivyo kwa magonjwa mengine. Wameng'ang'ania ng'ang'ani na takwimu za corona, kuna biashara gani hapo?

Je unadhani tukiwapa takwimu zetu, zitasaidia kuondoa corona? La hasha, hawa watu wanatuwinda watu weusi. Tusipokuwa makini watatuumiza.
 
Acha kifikiri kwa kutumia makalio,kuwa mzalendo wa Taifa lako,acha kuwa kibaraka wa wazungu,nachukia mmmno wasiojitambua
 
Potelea mbali na mashetani wako
 
Kule Tanga ushirikina mwingi sio corona msitudanganye
 
Ulaya wamefanya hivyo wamepunguza ???
 
Si kweli kwamba sisi sote hatutaki chanjo ya Wazungu.Chanjo ulizochanjwa za surua,ndui,tetekuwanga,polio na nyingine zilitengenezwa Manzese?
Jihadhari na ushabiki wa kisiasa
 
Kwa hiyo kila siku unatangaziwa ni wangapi wameugua malaria, wangapi wamekufa na wangapi wamepona?

Takwimu zote za malaria zipo. Usiwe mvivu soma na tafuta. Zote zipo na zipo kwenye public domain.

Uweze hata kuona impact ya vyandarua ambayo ni kwa hisani ya watu wa marekani.

Takwimu za magonjwa mengine yote zipo:


Wapi za corona?

Mtatafuta sana wa kumlaumu lakini ilitamkwa: "kaniki ni rangi yake!"
 
Huyu wale wapambe wake ndiyo wanampoteza
 
Jiridhishe kuwa unakosa facts na sasa unabwabwaja tu kwa vile una mdomo ambao aghalabu hata kuku anao:
Kutofautiana kwa hoja, haina maana nabwabwaja. Mtu makini hutafakari kwanza hoja ya upande wa pili kabla naye hajabwabwaja.

Taifa linatoa takwimu zote za magonjwa mengine isipokuwa corona, je huwezi kujiuliza swali hapo. Chunguza kuna nini nyuma ya pazia.
Maamuzi ya kutotoa takwimu si ya mtu mmoja bali ni jopo la watu wenye ueledi mkubwa kwa ajili ya taifa letu. Hata wanaotulazimisha kutoa takwimu nao wana jopo lao lenye malengo yao yaliyo hasi nasi.
Je wajua ya kwamba kuna njama ya kuwangamiza watu weusi barani Afrika? Hatujui watatumia silaha gani, ni lazima tujihami.
 
Kama ugonjwa upo nyinyi mnataka selikari iwafanyie nini
 

Kwanza nikupongeze kwa kutambua kuwa takwimu za magonjwa yote hapa nchini zipo wazi kwa jamii isipokuwa kwa corona.

Pili ningependa utambue kuwa ugonjwa huu upo dunia nzima Amerika Kaskazini na kusini, Asia, Australia na hata Afrika.

Njama za kumwangamiza mwafrika kwa ugonjwa huu unaziokota wapi wakati mabara yote ni waathirika vilivyo na kote hawana mtazamo kama huo?!

Afrika penyewe hakuna nchi hata moja yenye kuona kuwa inalengwa na ugonjwa huu isipokuwa kwa serikali ya Magufuli?

Ni serikali ya Magufuli peke yake inayoona hivyo. Kumbuka mimi binafsi sioni hivyo. Tusiioona hivyo tuko wengi sana ndani ya nchi hii. Usishangae kuwa hayupo mwenye uelewa aliyeko upande wenu.

Siyo siri mlioko huko ni njaa zenu na umbumbu zaidi ndiyo unaowafanya kuendekeza kucheza ngoma uchwara hizo mnazocheza.

Hivi, Magufuli na genge lake wanapojaribu kutudanganya na hadithi zao hizi wanajaribu kufanya hivyo kwa ridhaa ya nani?

Demokrasia ni wengi wape. Kwanini tusitafute ridhaa hata kwenye kura ya maoni tu? Kwanini mnataka kutulazimisha na maoni yenu tusiyokubaliana nayo? Kwanini mnataka kutufanya kama watoto wadogo? Kwanini, ..., Kwanini, .., kwanini lakini ???


Mmejipachika eti kuwa mna weledi, hakuna lolote. Fahamuni kuwa kwa kila kifo kinachopita na ugonjwa huu upo siku mtajibu.

Kwa hakika mnatukera sana hasa hasa tunapoendelea kupoteza wapendwa wetu kila siku huu nyie ikiwa haiwahusu:

 
Onyo liko wapi hapo?!

Vipi mkuu bado onyo hulioni?

Watu kama nyie mna mchango mkubwa kwenye vifo vyote vya ugonjwa huu hapa nchini kikiwamo kifo cha huyu mheshimiwa.

Mlimwingiza kingi naye akachekelea.

Yako wapi sasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…