#COVID19 Corona bado inafikirisha sana

#COVID19 Corona bado inafikirisha sana

Kuna watu wanapata virusi na kupona bila dawa yeyote halafu wewe unasema hakuna mwenye kinga ya Corona.
Acha kujibu kisiasa

1. Ni jambo la kusikitisha kufanya siasa na ugonjwa huu.
2. Suala la ugonjwa likiwamo la ugonjwa huu kama nilivyosisitiza awali ni la kitalaamu zaidi.
3. Nikurejee hapa:

IMG_20210818_100421_254.jpg


4. Mtu kuugua na akapona bila dawa hakuna maana ya kuwa huyo alikuwa na kinga.
5. Kuwapo kwa kinga mwilini ni matokeo ya mwili kuwa na ufahamu wa uwepo wa ugonjwa fulani na hivyo kuzalishwa kwa kinga (antibodies) husika ili kupambana nao.
6. Antibodies haziwepo mwilini kwa ajali bila ya kuugua ugonjwa au bila kuzalishwa kupitia chanjo.

#COVID19 - Chanjo ni Lazima: Hoja ya Mbowe ina Mashiko

Comment #154 inahusika zaidi nikushauri kuipitia.

Angalizo: Nimewahi kuwasikia washupavu wakidai Corona si ugonjwa mpya kuwa wao waliwahi ugua ugonjwa huu miaka ya 2014.

😂😂!

Nakazia: ugonjwa huu ni sayansi, kukomaa kiugumu ugumu vijiweni hiyo ndiyo kuufanyia siasa huko, hakusaidii.

Hiiiiii bagosha!
 
Mazoezi yanasaidia sana vitu vingi!!

1. Kama machungudoa hujasikia kwa nini hudhani kuchakatwa papuchi ni muarobaini?
2. Kama wanywa gongo hujawasikia kwanini hudhani tujipange kupiga gongo tu?
3. Kama vibaka hujawasikia vipi tukiingizana kwenye kukwapua kuku tu?
4. Nk.
 
Mtu mwenye covid ila haonyeshi, bado huambukiza. Wakiambukizwa walio hatarini zaidi ndiyo yanapotukuta ya kupoteza watu.

Usisahau kuwa kirusi kikiachwa kupuyanga kitakavyo kinabadilika. Delta kinaathiri hata waliokuwa hawaathiriki na vile vya mwanzo.

Suala la Corona, Chanjo na tahadhari zake ni la kitalaamu zaidi. Kwa nini hatuzungumzii ujenzi wa maghorofa, kurusha madege angani au kusaka madini ardhini?

Kila mtu amekuwa fundi au researcher wa Corona?

Nisiache kukumbusha:

"Mbona umeyakwepa yale ya machangudoa, vibaka, majambazi, wanywa gongo, wavuta bangi, mafundi saa, mafundi makoroboi, wapika gongo nk, kutosikika kuathirika na Corona?"

Au lengo ni lile lile la kudanganya watu kama watoto wadogo tu, kuwa karibu chanjo ya Corona kutoka Tanzania inakuwa tayari?

Kwani tunaweza kutengeneza hata sindano ya kushonea nguo tu?

#COVID19 - Chanjo isiwe Siasa, Vigezo na Masharti vizingatiwe

Ya nini kufanyia siasa ugonjwa huu?
Corona itakuja kuisha kwenye mataifa makubwa yaliyoendelea itabaki kusumbua vitaifa ambayo vina siasa chafu na sera ambazo haziko thabiti.
Kumbuka ugonjwa wa AIDS ulivyoanza,nchi iliyoongoza kwa wagonjwa wengi ilikuwa ni U.S.A lakini baada ya miaka kupita,nchi inayoongoza utaikuta kwenye bara la Afrika.
 
Moja kwa moja kwenye mada. Kwanini wanamichezo hasa wachezaji mpira, riadha n.k hawasumbuliwi na Covid -19?

Wengi wamekutwa na virusi lakini hawalazwi wanaendelea na mazoezi au kucheza mechi pia kama vile hawana chochote kwenye miili yao.

Wengi pia hupona bila kutumia dawa yoyote maana hawaoneshi dalili yoyote.

Hoja yangu:

1. COVID-19 inaweza kuondoka kwa mazoezi tu? Mazoezi yanaweza kuondoa virusi kwenye mapafu?
Mbona HIV hawaondoki kwa mazoezi?

2. Nahisi kuna vitu vingi vinapindishwa kuhusu huu ugonjwa na wataalamu wetu hawataki kujisumbua kutafuta majibu ya kina.

Tunahitaji ukweli na taarifa zaidi kuhusu COVID-19 kuliko propaganda.
UMETAFAKARI VYEMA
 
nyie ndio wale mademu,mtu akifanya kitu unaropoka "jiheshimu"uliyemwambia anaza kujitafakari nimefanyaje!!!!

kumbe nawewe umeropoka tu,ili uonekane mtu makini.
Wanaboa mnoo huwa nawashusha thamani watu wa hivyo. Ni wale wanaokosa hoja ni bora kunyamaza kuliko kujiona unajua wakati ukweli ni kuwa hauna hoja.
 
Ni ngumu,hasa pale wanaporuhusu mkusanyiko wa mechi ya Simba vs Yanga halafu wanadai eti hatua za tahadhari zinafuatwa.

Na mbio za mwenge, makanisani, matamasha, misikitini, magulioni, masokoni, misibani, maharusini nk.

Ni kupagawa fulani.

Waziri Ndugulile aliukataa upumbavu hadi akaishia kutumbuliwa kama Waziri wa afya.
 
Back
Top Bottom