Mitaani misiba imekuwa mingi sana. Kwingine habari za mochwari kufurika zinasikika.
Maprofesa na hata vigogo ni baina ya wahanga.
Moja ya vipimo vya uhalisia wetu kuhusiana na huu ugonjwa ni hiki hapa:
View attachment 1878044
Babu Loliondo aliachwa kukusanya wagonjwa wa Corona nyumbani kwake pasipo na kuwepo tahadhari zozote.
Haya yakiendelea serikali na wizara ya afya wakiwa ni wapenzi watazamaji.
Bila ya kuwachukulia hatua kali wote waliozembea hata katika hili, kwa hakika hatutoboi.
Source:
Babu wa Loliondo kuzikwa Samunge Jumatano
Umesema vyema sana Kiongozi. Sasa tunarudi kwenye hoja, kwamba, kwa kuwa chanjo haitibu maambukizi, na wala hahizuii maambukizi, na kama viongozi wetu wanakuwa wapenddwa watazamaji, tuchukue hatua sisi za kujilinda. Tuzingatie kanuni zote za Afya kama tulivyovanya kwa awamu zlizopita. Kuna dawa zetu zilitumika kutibu wagonjwa waliokuwa wanalazwa na pamoja na kwamba kweli tulipoteza ndugu na wapenzi wetu, lakini tulifanya vizuri kulinganisha na jirani zetu katika ukanda wetu.
Najua ni vigumu kumlazimisha abiria mwenzako avae barakoa ama afunike uso anapokohoa ama kupiga chafya. Ni vigumu abiria kudhibiti ujazaji abiria uliokithiri ikiwa hata vyombo vya serikali vinajaza lumbesa mfano mwendo kasi na pantoni, mbio za mwenge n.k. Trafic wako kila kona lakin hakuna hata anayesimamisha gari na kudhibiti lumbesa za abiria.
Hii , ki kwetu inaitwa "YATIMA HADEKI", na kwa kule unguja inaitwa "UTAJIJU",
Tuiombe serikali, japokuwa nasikia saauti inasema "kila mtu abebe mzigo wake", tuome isaidie kupeleka dawa zetu zilzotuvusha katika vipindi vilivyopita.
Ninakumbuka Rasi alitangaza tuombe Mungu kwa siku tatu. Kweli tuliomba na ilipatikana dawa ambayo inasemekana kutibu vizuri zaidi Delta Variant ambayo inasambaa kwa kasi kuliko zilzopita. Hiyo dawa itengenezwe kwa wingi na ipelekwe kila sehemu angalua kila raia apate. Hii inaonekana ni budget kubwa lakini si kitu ukilinganisha na hasara tunayoipta kwa kupoteza hazina zilizo ndani ya watu, gharama za machanjo n.k. Ni kiasi cha kuahirisha mbio za mwenge na kujikita kwenye kuzalisha na kusambaza dawa hizo wakati biashara ya Johnson ikiendelea.
Watu wanahitaji tiba kwanza kabla ya chanjo. Tiba iliyotusaidia, sasa hivi ukiizungumzia unakula ban. Kipaumbele ni chanjo ambayo hata haizuii maambukizi wala haitibu.
Kama serikali imetutelekeza hivyo, tupashane habari sisi wenyewe na kusaidiana namna ya kupeleka tib hata kwa wazee walioko vijijini.
Mungu aliyetusaidia, hata sasa atatusaidia. Tumtangulizeni yeye, na kisha tuungane bila ushaibiki wa kisiasa ama kibiashara. Kwa sasa tunahitaji tiba.