#COVID19 Corona: Bila Makavu itaondoka na Wengi

Chanjo inakinga na hivyo kusaidia kutibu,,, acha upotoshaji.
Zamani hatukuwa na record yoyote zaidi ya kupigwa marufuku hata kujisema mtu binafsi kuwa anaumwa corona ,hivyo hatungeweza kujilinganisha na yeyote.
Hiyo mitishamba haijakatazwa kuitumia ,usilazimishe legacy.
Chanjo inakinga, na hivyo kusaidia kutibu. Tusipotoshe kienyejienyeji.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Il 'dawa' ya Madagascar Mwendazake alimtuma jamaa wa jalalani akailete ilikuwa dawa kweli? Ulitaka WHO waache sayansi waingie kwenye syrup za kichawi!
Hujui hata uchawi ndugu yangu.
 
Hivi hiyo Mitaa yenye misiba mingi iko wapi? au siishi mtaani!!!
 

1. Kwamba?

"...... Kuna dawa zetu zilitumika kutibu wagonjwa waliokuwa wanalazwa na pamoja na kwamba kweli tulipoteza ndugu na wapenzi wetu,"

Unamaana nyungu, mikaratusi, malimao, michai chai na matango pori mengine? Kuna mabingwa wa hayo kuliko hawa:





Umeshawauliza sasa hivi wanasema je?

Aisifuye mvua imemnyea!


2. Kwamba?

"lakini tulifanya vizuri kulinganisha na jirani zetu katika ukanda wetu."

Nani anakudanganya ulifanya vizuri kuliko nani? Kwa takwimu zipi? Kwani kulikimbia tatizo kuliwahi kuliondoa?



Kwetu tumepoteza hadi Rais na makamu wa rais. Tumepoteza Mawaziri, wabunge na vigogo wa kila aina. Tumepoteza watu wangapi? Wewe unajua?

3. Kwamba?

"Ninakumbuka Rasi alitangaza tuombe Mungu kwa siku tatu. Kweli tuliomba na ilipatikana dawa ambayo inasemekana kutibu vizuri zaidi Delta Variant ambayo inasambaa kwa kasi kuliko zilzopita."

Nani asiyejua kuwa ugonjwa huu hauna dawa? Hata mtoto mdogo anajua hilo. Dawa gani mliyopata baada ya maombi ambayo labda wewe ndiye unayeijua peke yako? Au ni hii hapa?



4. Kwamba?

"Watu wanahitaji tiba kwanza kabla ya chanjo. Tiba iliyotusaidia, sasa hivi ukiizungumzia unakula ban. Kipaumbele ni chanjo ambayo hata haizuii maambukizi wala haitibu."

Unadhani tatizo ni nini nani anahitaji kwanza? Tatizo ni nini kinawezekana sasa! Uliwahi kusikia TMDA au WHO kuhusiana na madawa ya binadamu?

😂😂😂😂 Elimu yako tafadhali.

5. Kwamba?

"Mungu aliyetusaidia, hata sasa atatusaidia. Tumtangulizeni yeye, na kisha tuungane bila ushaibiki wa kisiasa ama kibiashara. Kwa sasa tunahitaji tiba."

Mungu alikusaidia wapi mjomba? Unajua huu ugonjwa unakwenda kwa mawimbi? Moja baada ya jingine?



Kila lijalo ni kubwa kuliko lililopo? Unajua kupita kwa wimbi moja si kwisha kwa ugonjwa?
 
Hivi hiyo Mitaa yenye misiba mingi iko wapi? au siishi mtaani!!!

Ili usipate taabu sana kuijua mingine hii hapa:

1. Kwenye msiba na mwenziwe:



2. Kwa Keenja, Keenja asubuhi mke saa sita.

Hiyo ni nyumba moja moja. Kama bado huoni vya miwani ya mbao uliyovaa.
 
Aliendelea kutoa kikombe na serikali ikiendelea.

Hao waliokuwa wakiangalia wangalipo madarakani na wakituhamasisha dhidi ya ugonjwa huu.

Tutakuwa tumerogwa.
Wajinga ndio waliwao
 
Serkali ilianza kwa kuuchukulia poa huu ugonjwa
 
Wewe ni mjinga na usipochukua tahadhari stahiki ikiwemo kupiga chanjo utakufa.
 
Mi ni mnyakyusa lakini nathubutu kusema msiwaamini manabii wa kinyakyusa ni wapigaji tu... sijui kinamwamposa, Mzee wa Upako, Mwasapile Loliondo. MSITHUBUTU la sivyo you are all dead
Maweee!
 
Kama wazungu wametengeza ugonjwa, piga chanjo yao uishi, tengeneza ya kwako au usubiri ufe kibudu
 
Msisitizo wa corona unatoka ulaya. Haya magonjwa mengine tufanye wenyewe. Sigara ni starehe huwezi kataza watu,, unawapa tahadhari inatosha.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Magonjwa yote, dawa zote na chanjo zote zinazotolewa hospitalini zimegunduliwa na hao wazungu na hata wapinga korona wakiugua wanakimbilia hukohuko hospitali kutafuta tiba za kizungu. Ujinga mzigo sana!
 
Kama wazungu wametengeza ugonjwa, piga chanjo yao uishi, tengeneza ya kwako au usubiri ufe kibudu
Katika wale maadui watatu wa maendeleo yaani Ujinga Maradhi na Umaskini hili la ujinga kimeshika kasi nchi hii mpaka kwa wanaojiita wasomi. Bila ujinga kuondolewa kwenye jamii ya wasomi na wasiosoma maradhi na umaskini hayatakaa yaishe kwenye nchi yetu.
Kama unaamini kuwa virusi vya covid 19 wametengeneza wao basi amini pia kuwa wana uwezo wa kutengeneza dawa ya kuutibu ugonjwa huo. Hivyo wahi ukachanje au kama umri wako ni mdogo washauri wazazi wako wakachanje haraka.
 
Msisitizo wa corona unatoka ulaya. Haya magonjwa mengine tufanye wenyewe. Sigara ni starehe huwezi kataza watu,, unawapa tahadhari inatosha.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Mkuu hata madawa ya kulevya ni starehe tena kubwa sana ila yamekatazwa kwa sababu ya madhara yake ni makubwa kwenye jamii, sasa na sigara nazo sina madhara sana kwenye za afya za watu kuliko faida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…