Corona imekuwa mradi wa Serikali au Mradi wa watu? Wanaowekwa karantini walalamikia bei kubwa ya hoteli wanazopelekwa

Corona imekuwa mradi wa Serikali au Mradi wa watu? Wanaowekwa karantini walalamikia bei kubwa ya hoteli wanazopelekwa

1585059036960.png
 
Mnyororo unaoweza kusababisha maambukizi

Hawa waliowasili kutoka nje wanawasili na kuwekwa ktk hoteli za binafsi mfano hoteli ya Peacock mtaa wa Lumumba kulipo ofisi ndogo ya CCM makao makuu Dar es Salaam .

Scenario 1 :Mfanyakazi wa Peacock Hotel anaenda kupiga soga na Polepole ktk mitaa ya Lumumba jijini Dar. Baadaye Polepole anakwenda kikazi Dodoma. Ana mkutano na mawaziri kupima utekelezaji wa sera za CCM zilizomo ktk ilani ya ahadi za CCM.

Mawaziri wanaitwa na Waziri Mkuu katika kikao na mawaziri wake kupanga mikakati ya kupambana na coronavirus.

Scenario 2: Wanaowasili toka nje wanapelekwa shule ya Mgulani JKT. wanawekwa karantini siku 14 chini ya ulinzi wa kijeshi wa SUMA. Askari wa SUMA wenye nidhamu hakuna kutoka nje ya kambi korona imedhibitiwa kisawasawa isisambae.
 
Duh and you are a Dr?! Kwamba wachague tu mimi Kariakoo mwingine Machi Machi guest house kinondoni sio?
Waliambiwa ukija huku unakaa karantini siku 14 kwa gharama zako. Wangebaki huko huko wangeokoa nauli yao na wangekaa hotel za $5

Usidhani wote wanaorudi, wanarudi kwa kupenda.. Kuna wengine walikuwa wamemaliza muda wa kukaa nje na masurufu yao pdiem yakaishia siku hiyo ambayo walirudi.. Sasa unasema wangebaki huko huko, wangebakia wapi kwa mfano..? Wangeishi vpi na wangepata wapi fungu la kujikimu muda wote huo ambao wangekuwa wamekaa huko..? Ni watanzania hao, na hapa ndo kwao..
 
Baadhi ya Wasafiri waliofika Uwanja wa Ndege wa Dar na kutakiwa kujiweka Karantini kwa gharama zao wakilalamika kuwa wametakiwa kukaa hoteli zenye gharama

Wasafiri hao wameomba msaada kwa Mamlaka hususan Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kwani wametakiwa kukaa katika hoteli za Southern Sun, Rungwe, Dar Palace na Peacock Hotel
HIVI MPAKA HAPO SI AMESHAWAAMBUKIZA WATU KADHAA CORONA KAMA ANAYO? SERIKALI YA BASHITE NA MSHIKAJI WAKE HAIPO SERIOUS
 
March 24, 2020
Kilimanjaro International Airport
Tanzania

Karantini ya hiari kwa muda wa siku 14

Kamati ya korona, ulinzi na usalama ikiongozwa na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro alifika KIA Airport kukagua zoezi la kuhakikisha gonjwa la coronavirus halisambai

ABIRIA 15 walioingia nchini kupitia uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa kutumia mashirika yenye miruko ya kimataifa ni Qatar Airways, Ethiopian airlines, PrecisionAir wakitoka nchi mbalimbali Duniani yaani abiria raia wa Tanzania, Russia, Germany, Canada, Japan wamewekwa katika Karantini ya hiari kwa muda wa siku 14 ikiwa ni njia ya kupunguza maambukizi mapya ya ugonjwa wa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona.

Source: cloudsmedia
 
Hii video inayomuonesha mama aliyetoka nje ya nchi akilalamika kupelekwa hotel za ajabu zenye gharama kubwa ina ukweli?

Hivi kweli hizo ndo karantini zilizotengwa na Serikali? Rais umepataje nguvu ya kutalii juu mawe ili hali nchi haina karantini na tunategemea mahotel ya mabepari?

Mimi ninaisi huu ni mchongo wa baadhi ya watendaji wa Serikali. Dada njoo manzese ukae guest.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani wewe ulipoombiwa watawekwa quarantine tena kwa gharama zao ulihisi ni nini? Ulidhani serikali inawajengea nyumba enhee? Watu pekee wanaogharamiwa na serikali ni wale waliogundulika wana maambukizi tayari.
 
Usidhani wote wanaorudi, wanarudi kwa kupenda.. Kuna wengine walikuwa wamemaliza muda wa kukaa nje na masurufu yao pdiem yakaishia siku hiyo ambayo walirudi.. Sasa unasema wangebaki huko huko, wangebakia wapi kwa mfano..? Wangeishi vpi na wangepata wapi fungu la kujikimu muda wote huo ambao wangekuwa wamekaa huko..? Ni watanzania hao, na hapa ndo kwao..
Hata kama ni Watanzania, ukirudi nchi yoyote sasa hivi unakaa karantini siku 14.
 
Kwani wewe ulipoombiwa watawekwa quarantine tena kwa gharama zao ulihisi ni nini? Ulidhani serikali inawajengea nyumba enhee? Watu pekee wanaogharamiwa na serikali ni wale waliogundulika wana maambukizi tayari.
Kwahiyo waliogundulika tayari na wao wanawekwa karantini kwenye hayo mahoteli?
 
Baadhi ya Wasafiri waliofika Uwanja wa Ndege wa Dar na kutakiwa kujiweka Karantini kwa gharama zao wakilalamika kuwa wametakiwa kukaa hoteli zenye gharama

Wasafiri hao wameomba msaada kwa Mamlaka hususan Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kwani wametakiwa kukaa katika hoteli za Southern Sun, Rungwe, Dar Palace na Peacock Hotel
Walisema ni siri hawatazitaja majina ili watu wasienfe kuwaangalia, imekuwaje siri ya sirikali kuwa si siri?
 
Back
Top Bottom