seedfarm
JF-Expert Member
- Feb 9, 2020
- 260
- 2,655
"Dar es Salaam lazima kuwe na wagonjwa wengi na vifo vingi kutokana statistically kuna Population kubwa".Hii kauli ni ya Mamlaka
Ukweli huogopesha lakini bora usemwe,Corona maeneo ya Dar es Salaam inamaliza watu, Hakuna mwandishi au gazeti ambalo linaweza kuhoji familia hizi zinazolia kila siku kwa kutowaona wapendwa wao wanaozikwa kimya kimya na Mamlaka
Kauli za kupeana Morali kuwa watu wachape kazi waongeze pato la Taifa Dar es Salaam litamsaidia nani? Hizi familia ambazo ndugu zao wanazikwa kwa kuugua corona zina mateso makali sana.
Watu maarufu na wenye ushawishi kwenye mamlaka na jamii ndio hao wanazikwa na watu wasiozidi ishirini au kumi, Je wewe kabwela ambae hutambuliki na mamlaka omba yasikukute
Uchunguzi ufanyike nini kinachoendelea maeneo ya makaburi ya huko Bahari Beach eneo la kondo,Buza na Mbweni
Uchunguzi ufanyike ongezeko la kelele za ambulance kwa wingi maeneo ya Dar es salaam kutoka hospital kuelekea maeneo hayo ni wangapi wanazikwa kwa janga hili
Tunakubaliana vita inahitaji umorali na nguvu lakini hili ni gonjwa sio vita linahitaji tiba tahadhari na ukweli
Leo hii kuna malalamiko makubwa watu wakifuatilia ndugu zao hospitali waliolazwa wanajibiwa alishafariki na kuzikwa na mamlaka kimya kimya,
Mamlaka imeamuru wizara ya afya ijibu kuwa sio kila mgonjwa hufa kwa corona ni kweli.Je kwanini wanazikwa na mamlaka bila hata ndugu kuhusishwa bali hujibiwa ndugu yenu alishazikwa amefariki
Wizara ya afya ni bora mkaongea ukweli ili watu wachukue tahadhari kuliko sasa mnapojaribu kuuma na kupuliza,
Paul Makonda alikuwa anapuliza na kufariji watu wachape kazi lakini visa vya watu kupukutika na corona sasa amebadili kauli na kuamua kuwa mkweli kuwa Dar corona inamaliza watu
Mamlaka kila siku inakuja na kauli kinzani kama corona sio ishu kwanini mnafunga shule Tanzania nzima, Ruhusuni baadhi ya mikoa elimu iendelee isipokuwa Dar na Zanzibar
Wanakijiji wasiojielewa na baadhi ya wapiga pambio wao hawachuji kauli za mamlaka, Hii itapelekea watu kuwa na morali na kupukutika zaidi
Update
kwa wanaoishi hapo kondo Bahari Beach soma ushahidi wa member hapa aliyefiwa na ndugu yake kinachoendelea tarehe 25/4/2020
Happening now at Kondo bahari beach; merehemu wa watu tofauti kama 10 wanakuja kuzikwa hapa Kondo - JamiiForums
Update 2
Ushuhuda leo tarehe 26/04/2020 soma
Tuliokuamini na kukutetea kwenye janga la Corona umetuangusha. Nimepoteza rafiki na ndugu kwa janga la Corona. Serikali chukueni hatua - JamiiForums