Tetesi: Corona inapukutisha watu Dar. Kuna wanaolalamika ndugu zao kuzikwa kinguvu na Mamlaka Dar huko Bahari Beach, Buza na Mbweni

Tetesi: Corona inapukutisha watu Dar. Kuna wanaolalamika ndugu zao kuzikwa kinguvu na Mamlaka Dar huko Bahari Beach, Buza na Mbweni

giphy.gif

Twafaa!! HAKUNA HAJA YA KUFICHA
 
Kwanza nitoe pole kwa vifo na maradhi haya yaliyoikumba dunia kwa sasa

Dunia iko kwenye wakati mgumu sana na wengine wamekufa kwa kupigwa kwenye baadhi ya nchi ambazo waliona kufungia watu ndani ni njia nzuri ila wengine tumekiona

Thailand walithibisha kuwa maiti inaambukiza Corona baada ya watu kuambukizwa na wataalamu duniani wakakubaliana wote kuwa maiti inaambukiza

Huku nilipo mtu akizidiwa akachukuliwa kutoka nyumbani kumuona tena ni vigumu sana na wakijua sasa zimekaribia wanakupigia simu kwa video call unamuona kwa mara ya mwisho

Anafungwa kama mzigo halafu kwenye mazishi wanaruhusu watu 2 tu
Hakuna kuaga mwili tena bali ni kufukiwa tu

Mungu atupe mwisho mwema ila hili gonjwa lisikieni tu

Kama yanatokea huko sina uhakika labda waje mashuhuda wengi waliokutana na masaibu haya

Maana kuna clip kwenye YouTube inaonyesha maiti ikichukuliwa na gari pamoja na watu waliovaa nguo za kujikinga tena kwenye nyumba na nafikiri ndugu akiwa anazunguka hapo sidhani hata kama aliwafuata

Hali ni mbaya tukubaliane tu


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Mkuu, wewe umeshuhudia watu wakizikwa kwenye hayo makaburi au ni hisia tu? Watu wangapi? How ndugu zao wamemlalamikia nani? Kwamba milio ya ambulance ni ushahidi watu 'wengi' wanakufa?

Ni kweli Corona ni tatizo, lakini hatutaishinda kwa kutishana na kujazana hofu. Tutimize wajobu wetu kuishauri Serikali juu ya hatua za kuchukua kwenye mapambano haya huku kila mmoja wetu akichukua tahadhari. Uongo na vitisho kwa wananchi havina tija, vina madhara makubwa zaidi.
 
Wamekufa kumi tu. Hizo picha na videos mtandaoni mzipuuze, ni za mabeberu wanaotaka nchi isitawalike.
Hata lile lory la manispaa lililoandikwa Dar City Council burial services sio la serikali, hata Kama Lina namba SU.
Mkiliona linaranda randa maeneo ya makaburi mlipuuze
😂 😂 😂 😂 😂
 
seedfarm,
Kwani wewe ulitakaje? Nahicho unahitaji si umejibiwa jana? Mbona mnapoteza muda wa watu kwa kurudia same quiz?
 
Jipe muda mkuu kabla hujafikia hitimisho anachokisema mleta mada kina usahihi mkubwa sana

Bahati mbaya wengi wetu ni kama samaki tuna mengi ya kusema ila ndio hivyo mdomoni kuna maji

Ndugu yangu kaondoka na keshafukiwa huko, kilichobaki ni kuanua matanga

Shida ni kubwa kuliko unavyodhani.
Mada kama hii yako ni ngumu mno kuiamini, na wala haiingii kabisa akilini.
Kukiwa na ukweli wowte juu ya haya uliyoandika hapa, basi hakuna serikali iliyowekwa madarakani na wananchi. Badala yake, kutakuwa na kitu kingine kabisa ambacho sina jina la kukipa.

Kuleta mada kama hii, halafu pasiwepo na aina yoyote ya ushahidi unaoipa mada uzito, angalau hata wa kimazingira tu, ni kulifedhehesha hili jamvi la JF.

Hii ni hatari sana kama kuna aina yoyote ya ukweli kwenye mada yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilipaswa kuwa hivyo. Wagonjwa "washughulikiwe" kimya kimya ili wasiambukize wengine.

Nchi zisizo na Ukimwi walidaganya hivyi.


Kuna maovu mawili, chagua dogo.

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: T11
Back
Top Bottom