Tetesi: Corona inapukutisha watu Dar. Kuna wanaolalamika ndugu zao kuzikwa kinguvu na Mamlaka Dar huko Bahari Beach, Buza na Mbweni

Tetesi: Corona inapukutisha watu Dar. Kuna wanaolalamika ndugu zao kuzikwa kinguvu na Mamlaka Dar huko Bahari Beach, Buza na Mbweni

"Dar es Salaam lazima kuwe na wagonjwa wengi na vifo vingi kutokana statistically kuna Population kubwa".Hii kauli ni ya Mamlaka

Ukweli huogopesha lakini bora usemwe,Corona maeneo ya Dar es Salaam inamaliza watu, Hakuna mwandishi au gazeti ambalo linaweza kuhoji familia hizi zinazolia kila siku kwa kutowaona wapendwa wao wanaozikwa kimya kimya na Mamlaka

Kauli za kupeana Morali kuwa watu wachape kazi waongeze pato la Taifa Dar es Salaam litamsaidia nani? Hizi familia ambazo ndugu zao wanazikwa kwa kuugua corona zina mateso makali sana.

Watu maarufu na wenye ushawishi kwenye mamlaka na jamii ndio hao wanazikwa na watu wasiozidi ishirini au kumi, Je wewe kabwela ambae hutambuliki na mamlaka omba yasikukute

Uchunguzi ufanyike nini kinachoendelea maeneo ya makaburi ya huko Bahari Beach eneo la kondo,Buza na Mbweni

Uchunguzi ufanyike ongezeko la kelele za ambulance kwa wingi maeneo ya Dar es salaam kutoka hospital kuelekea maeneo hayo ni wangapi wanazikwa kwa janga hili

Tunakubaliana vita inahitaji umorali na nguvu lakini hili ni gonjwa sio vita linahitaji tiba tahadhari na ukweli

Leo hii kuna malalamiko makubwa watu wakifuatilia ndugu zao hospitali waliolazwa wanajibiwa alishafariki na kuzikwa na mamlaka kimya kimya,

Mamlaka imeamuru wizara ya afya ijibu kuwa sio kila mgonjwa hufa kwa corona ni kweli.Je kwanini wanazikwa na mamlaka bila hata ndugu kuhusishwa bali hujibiwa ndugu yenu alishazikwa amefariki

Wizara ya afya ni bora mkaongea ukweli ili watu wachukue tahadhari kuliko sasa mnapojaribu kuuma na kupuliza,

Paul Makonda alikuwa anapuliza na kufariji watu wachape kazi lakini visa vya watu kupukutika na corona sasa amebadili kauli na kuamua kuwa mkweli kuwa Dar corona inamaliza watu

Mamlaka kila siku inakuja na kauli kinzani kama corona sio ishu kwanini mnafunga shule Tanzania nzima, Ruhusuni baadhi ya mikoa elimu iendelee isipokuwa Dar na Zanzibar

Wanakijiji wasiojielewa na baadhi ya wapiga pambio wao hawachuji kauli za mamlaka, Hii itapelekea watu kuwa na morali na kupukutika zaidi

Update
kwa wanaoishi hapo kondo Bahari Beach soma ushahidi wa member hapa aliyefiwa na ndugu yake kinachoendelea tarehe 25/4/2020

Happening now at Kondo bahari beach; merehemu wa watu tofauti kama 10 wanakuja kuzikwa hapa Kondo - JamiiForums

Update 2
Ushuhuda leo tarehe 26/04/2020 soma
Tuliokuamini na kukutetea kwenye janga la Corona umetuangusha. Nimepoteza rafiki na ndugu kwa janga la Corona. Serikali chukueni hatua - JamiiForums
Una hamu ya kusikia taarifa mbaya za vifo

Dar ina watu karibia 6m, unaposema watu wanapukutika unamaanisha watu wangapi??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mada kama hii yako ni ngumu mno kuiamini, na wala haiingii kabisa akilini.
Kukiwa na ukweli wowte juu ya haya uliyoandika hapa, basi hakuna serikali iliyowekwa madarakani na wananchi. Badala yake, kutakuwa na kitu kingine kabisa ambacho sina jina la kukipa.

Kuleta mada kama hii, halafu pasiwepo na aina yoyote ya ushahidi unaoipa mada uzito, angalau hata wa kimazingira tu, ni kulifedhehesha hili jamvi la JF.

Hii ni hatari sana kama kuna aina yoyote ya ukweli kwenye mada yako.
Mkui huoni kinachoendelea ...hakuna taarifa zozote rasmi huku tunaskia watu wanakufa...Serikali yetu naona imebobea kwenye ujenzi tu lkn masuala ya kudeal na majanga..ni hopeless kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Issue ni muda Wa maziko au aina ya ugonjwa inachangia aina ya maziko?


Jikinge na uwapendao hizi porojo hapa hazimalizi ugonjwa, watu wanakufa na kuugua sana tu.
Sijaelewa hata umeandika nini madame
 
Mkui huoni kinachoendelea ...hakuna taarifa zozote rasmi huku tunaskia watu wanakufa...Serikali yetu naona imebobea kwenye ujenzi tu lkn masuala ya kudeal na majanga..ni hopeless kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
Ninakubaliana na wewe mkuu.
Hilo sio nililolenga kulijibu kwenye bandiko hilo, ingawaje inaonekana kama ninaitetea serikali.
Kama waTanzania hawalioni hili kwenye serikali yao hii, basi tunalo tatizo kubwa sana kama taifa.
 
Ninakubaliana na wewe mkuu.
Hilo sio nililolenga kulijibu kwenye bandiko hilo, ingawaje inaonekana kama ninaitetea serikali.
Kama waTanzania hawalioni hili kwenye serikali yao hii, basi tunalo tatizo kubwa sana kama taifa.
We hujaona jana kwenye page za Mange na wengine imepostiwa video hakuna ruhusa ya picha?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una hamu ya kusikia taarifa mbaya za vifo

Dar ina watu karibia 6m, unaposema watu wanapukutika unamaanisha watu wangapi??

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata mgonjwa mmoja akifa kwa dalili zote zinazoonyesha kauliwa na corona, halafu serikali ikaamua kuficha habari zake zisijulikane, tukisema 'wanapukutika' ni yaki yetu kusema hivyo.
 
Hata mgonjwa mmoja akifa kwa dalili zote zinazoonyesha kauliwa na corona, halafu serikali ikaamua kuficha habari zake zisijulikane, tukisema 'wanapukutika' ni yaki yetu kusema hivyo.
Mmmh
 
Tatizo teknolojia tunayotumia inahitaji muda mrefu kujua chanzo cha kifo, ivyo kuna wakati serikali inalazimika kuzika kabla haijapata majibu kama ni corona ama la, na ivyoivyo inalazimika kutoa taarifa kila baada ya siku 3.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom