Corona ipo,tuchukue tahadhari

Hili gonjwa mpaka lichomoke na mawaziri 6 hivi, manaibu waziri 9, wabunge 20, na makatibu wakuu 8. Ndio serikali yetu itapata akili.

Nchi hii raia akipiga kelele jambo lolote linalokandamiza, kama vile kodi kubwa, wale wenye misamaha ya kodi utawasikia wanapiga domo TULIPENI KODI KWAAJILI YA KUJENGA NCHI YETU, tulipe kodi vipi wakati nyinyi mna msamaha wa kodi? Huu si uboya.

Raia wa hali ya chini wasio na bima ya afya wala hela ya kununua panadol wakipiga kelele Corona ipo mtaani na inamaliza ndugu zetu, wale wenye bima za afya za kiserikali na misafara ya ulinzi, utasikia wanapiga domo CORONA NI GONJWA LA KISHETANI, TANZANIA HALIPO. Wakati serikali imejaa mashetani.
 
Korona ipo, korona ipo, korona ipo nmerudia mara tatu




Nipo katika chuo kimojawapo hapa nchini,,asee kwanzia hii wiki malecture nmewaona wapo siriaz san kuhusiana na njia za kujikinga na korona ,,nmeanza kuona wanavaa mask,,,social distance imeanza kuzingatiwa vikali,,kusanitize vitu mbali mbali kama meza,kiti,ubao,,mpka laptop!


Hii kitu ipo viongozi wetu wameliweka kisiasa sana naona mkulu amewafunga midomo wasiweke ukweli anaona atakua ameonesha udhaifu san kwan yeye nd anaona ni kitu cha kumpa sifa kua ameimaliza korona


Mficha maradhi kifo humuumbua! Inasikitisha sana
 
^Chuo kimojawapo hapa nchini^!????
 
Jihadhari sana na mtu yeyote anayeshinda kutwa kuchwa akieneza hofu isiyomantikifu (unreasonable fear) --- hakuna mchawi yeyote hata angekuwa na digrii 33 za freemason ama ugonjwa wowote hatari wa kufisha unaopaswa kuogopwa zaidi ya mtu wa sampuli hiyo. We don't want ^hofumen^ kwenye nchi yetu; but rather ^hopemen^
 
Wewe una Corona?
Watu tunapiga kazi na story za kutosha vijiweni kama kawaida.
Mungu yupo.....hizo ni njia tu za kutamani kuwekwa lockdown.
Eti sikuhizi magonjwa mengine yamejiuzulu kuua.
Acheni hizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…