Corona ipo,tuchukue tahadhari

Corona ipo,tuchukue tahadhari

Hili gonjwa mpaka lichomoke na mawaziri 6 hivi, manaibu waziri 9, wabunge 20, na makatibu wakuu 8. Ndio serikali yetu itapata akili.

Nchi hii raia akipiga kelele jambo lolote linalokandamiza, kama vile kodi kubwa, wale wenye misamaha ya kodi utawasikia wanapiga domo TULIPENI KODI KWAAJILI YA KUJENGA NCHI YETU, tulipe kodi vipi wakati nyinyi mna msamaha wa kodi? Huu si uboya.

Raia wa hali ya chini wasio na bima ya afya wala hela ya kununua panadol wakipiga kelele Corona ipo mtaani na inamaliza ndugu zetu, wale wenye bima za afya za kiserikali na misafara ya ulinzi, utasikia wanapiga domo CORONA NI GONJWA LA KISHETANI, TANZANIA HALIPO. Wakati serikali imejaa mashetani.
Makatibu wakuu8??? Mnyika na mtoto wa mzee Ally hawapon
 
Corona yenyewe kama mafua tu.....idadi ya wanaopata na wanaokufa ni tofauti kabisa.
Wanawezaipata wa 1000,wakafa 10.....sifurahii watu kufa..ila haitishi kama baadhi ya watu wanavyotaka tuamini kuwa inatisha.
Cha ajabu hapa Tanzania,ni kikundi kidogo tu cha watu wanaotaka dunia ihamie Tanzania kuwa tunaisha na corona na serikali imekaa kimya.

Zito,na Chadema ndo wanataka nchi isimame. Ndugu zangu,lazima tujiulize kwanini kuna watu wanataka kufurahia kila baya ndani ya nchi yetu?
Kwanini kuna watu wanafurahia mambo ya hovyo kuliko ya msingi?
Watu hao bado tunaishi nao,tunakutana nao,wengine ni watumishi ndani ya serikali,why wasiende kuishi kwenye hizo nchi ambazo wao wanaamini tahadhari dhidi ya corona inachukuliwa vya kutosha?

Mh.Rais alituasa,corona ipo,na nilazima tujifunze kuishi nayo. Na watanzania tulimuelewa. Ni rai yangu.....tuendelee kuchukuwa tahadhari za magonjwa yote ikiwemo Malaria,UKIMWI,TB,Kipindupindu na mengine. Yota haya yanaua.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom