Corona: Kama Taifa, inafurahisha Busara inapoendelea kutamalaki

Corona: Kama Taifa, inafurahisha Busara inapoendelea kutamalaki

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Serikali ya awamu ya sita imekuwa kitulizo kikubwa kwetu tusiopenda kujidanganya au kudanganywa kwa hoja nyepesi nyepesi. Ifahamike kuwa njia ile iendayo uzimani ni nyembamba na yenye dhiki kuu.

Kwamba andiko la kujiunga COVAX liko kwenye hatua za mwisho mwisho, apongezwe sana rais wetu na mbeba maono halisi kipenzi chetu Mama Samia Suluhu Hassan. Kwa kweli Mama yetu huishi kutupa raha. Hakika unaiongoza nchi kwa niaba yetu.

Unaidhihirisha dhana kamili ya kuwa wewe ni kiongozi wala si mtawala. Kwenye hili tuko nawe Mama yetu.

Wito wetu kwako endelea hivyo hivyo. Usiache kuyasikiliza mahitajio ya haki kutokea kwa wananchi wako, ukayatafutie ufumbuzi nasi tutakuunga mkono kwa dhati ya mioyo yetu yote.

Kwa hakika hayupo kama wewe na Mola akakujalie afya na ujasiri zaidi wa kuthubutu kuyakabili yaliyokuwa yamewalemea wengine.

Nimalizie kwa kukusalimia kwa jina la JMT.

===

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imeandaa andiko kwa ajili ya kuomba chanjo za ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona kupitia mpango wa chanjo wa Covax Facility.

Hatua hiyo imekuja siku 81 tangu Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuunda kamati ya wataalamu watakaochambua kwa kina ugonjwa huo na kuishauri Serikali jambo la kufanya.

Ikikabidhi ripoti hiyo Mei 17, 2021 kamati ilipendekeza njia ya kupata unafuu ikiwa Serikali ya Tanzania itajiunga na mpango huo kwa kuwasilisha andiko la kupatiwa chanjo kwa kutumia fursa inayotolewa na taasisi ya uzalishaji wa chanjo duniani (Gavi).

Hayo yamesemwa jana Alhamisi Juni 24, 2021 na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Dorothy Gwajima wakati akizindua mpango mkakati wa sekta ya afya (HSSP V, 2021-2025) utakaotumia Sh47 trilioni katika kipindi cha miaka mitano ya utekelezaji wake.

Amesema kwa sasa Wizara ya Afya inaandaa andiko maalumu litakalowasilishwa kwenye kikao cha baraza la mawaziri kuhusu ugonjwa huo.

“Nichukue fursa hii kuwafahamisha kuwa Serikali ya Tanzania imekwishaandaa andiko la kupata chanjo za ugonjwa wa Covid-19 kupitia ‘Covax’ ambayo ni fursa inayotolewa na Gavi,” amesema Dk Gwajima.

Amesema hatua hiyo ni baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuteua kamati maalum ya wataalamu kumshauri na kutoa mapendekezo ya kukabiliana na ugonjwa wa corona nchini ambayo iliwasilisha taarifa na mpango kazi wa mapendekezo 19 yanayotakiwa kufanyiwa kazi na Serikali.

Waziri Gwajima amesema katika kukabiliana na wimbi la tatu la mlipuko wa ugonjwa huo, tayari Serikali imeanza kujipanga.
“Serikali kuanzia Julai mwaka huu itahuisha vikao vya kitaalamu (National Task Force) chini ya uenyekiti wa mganga mkuu wa Serikali na uenyekiti wenza wa mwakilishi mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO),” amesema.

Mwananchi
 
Tuliongozwa kama wajinga, tunamshukuru Mungu enzi za ujinga ule zimepita.
 
Tuliongozwa kama wajinga, tunamshukuru Mungu enzi za ujinga ule zimepita.

Hitajio letu la katiba mpya ni la msingi sana katika kuhakikisha zama zile hazirejei tena. Ikiwezekana kuyanusuru hata wana wa wajukuu zetu.
 
Back
Top Bottom