Corona, Katiba - Hatujishangai Wenyewe?

Corona, Katiba - Hatujishangai Wenyewe?

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Mkapa anapoelekea kutimiza mwaka 1 tangu kututoka yafuatayo ni baadhi ya mawaidha kutokea Mkapa foundation:

1. Wanathamini msukumo wa Mama Samia kupambana na janga hili la Corona kisayansi
2. Wanathamini msukumo mpya wa serikali kuelekea chanjo
3. Wanaelezea umuhimu wa chanjo
4. Wanaelezea manufaa ya chanjo
5. Nk

Ikumbukwe wengi wa wanaopinga msukumo mpya wa serikali kuhusiana na Corona ikiwamo chanjo, pia ni katika wengi wa wale wanaopinga uwapo wa katiba mpya.

Tusaidiane kujua kinagaubaga. Hivi:

1. hawa wanaopinga jitihada za serikali kuhusu Corona zikiwamo kuchukuliwa kwa hatua kisayansi, hoja zao hasa ni zipi?
2. hawa wanaopinga uwepo wa katiba mpya hoja zao hasa ni zipi?

Kusema kweli ndugu zetu hatuwaelewi labda mtueleze wenyewe.

Ni kweli kabisa kwa dhati yenu kuwa hamjishangai?

Hoja zenu tafadhali.
 
Hakuna wakati ambao wajinga, wabishi, wehu, wendawazimu na wanafiki waliwahi kukosekana katika jamii yoyote ile. Hawa wanaokataa mbinu za kukabiliana na corona kwa mbinu za kisayansi, wapo kwenye haya nakundi.

Tangu kuumbwa kwa Ulimwengu matatizo ya kiafya na mengije mengu yameshughulikiwa kwa mbinu za kisayansi ambazo zimekuwa zikiboreka mwaka baada ya mwaka. Hivyo ndivyo Dunia ilivyoweza kuikabili ndui, tetekuwanga, surua, kipindupindu, malaria, tauni, dysentry, kifua kikuu, n.k.

Dunia hii ipo hivi ilivyo kwa sababu ya Sayansi. Unamshamgaa mjinga, anapinga kukabiliana na corona kisayansi huku mtandao wa internet, kipaza sauti, gari anayotumia, nyumba yake, pikipiki yake, nguo zake, n.k. ni zao la Sayansi. Sasa mtu wa namna hiyo, utasema ana akili timamu?
 
Kwahiyo Chadema ndio mnataka chanjo na katiba?

Palikuwa na uzi hapa mkuu:

Hao Chadema unawaona wapi wewe?

Acha maneno weka Muziki!

Hoja zenu ni zipi nyie mnao pinga Corona au katiba?
 
Hakuna wakati ambao wajinga, wabishi, wehu, wendawazimu na wanafiki waliwahi kukosekana katika jamii yoyote ile. Hawa wanaokataa mbinu za kukabiliana na corona kwa mbinu za kisayansi, wapo kwenye haya nakundi...

Ngoja tuwasubiri kina johnthebaptist wanaojitanabaisha kuwa wao ni CCM.

Ni kweli kabisa tokea kwenye dhati za mioyo yao kuwa:

1. Kupambana na Corona kisayansi ni upuuzi?
2. Kutaka katiba mpya nayo ni upuuzi?

Kwamba hawajishangai na wanaona wako vizuri?

Kwamba wote hawa tutaishia nao leo katika karne ya 21 hapa hapa Tanzania?
 
Pia kwao wanakataa uwepo wa wazee.

Ni muhimu wakatambua uelekeo wetu ni

(1) kushughulikia Corona (priority) kwa mustakabala mwema wa maisha yetu sasa
(2) katiba mpya kwa mustakabala mwema wetu sisi, watoto tu na watoto watoto wetu.

In that order.
 
Naona kuna kuna tofauti ndogo kati ya wale wanaopinga Corona na Katiba Mpya.

Hawa wote wanatoka chama kimoja cha siasa, tatizo lao, wapo wanaopinga hatua dhidi ya Corona ili kulinda "legacy" ambapo hili ni kundi dogo ndani ya lile kundi kubwa linalopinga Katiba Mpya kwa maslahi ya chama chao wote.

Hawa jamaa ikizungumziwa Katiba Mpya wote huipinga, coz wanalindwa na hii Katiba mbovu iliyopo, lakini ikizungumziwa habari ya kujikinga na Corona, wana - divert, kama ni mto unatengeneza tawi, hawa wanalinda legacy hawataki tujikinge, huku wale wengine wanataka tujikinge hawa ndio wale wa "mama"
 
Ninakubaliana nawe:

1. CCM wote wanapinga katiba mpya. Hii ni kwa sababu ya ujinga, unafiki na pia kutokana na kunufaika binafsi na kama kundi kutokana katiba iliyopo.
2. Wanaopinga vita dhidi ya Corona ni CCM wote kuondoa wale walioko kwa Mama. Hawa wa mama ni wachache zaidi kuliko wale wa yule bwana wa legacy.

Wale wa yule jamaa wa legacy sehemu kubwa ni machinga, wapiga debe, vibaka, sungu sungu nk. Pamoja na kuwa na elimu duni, ni brainwashed hawajui wanataka nini au hawataki nini.

Kufanikisha agenda zao za kupinga vita ya Corona na/au katiba mpya wanatumia sababu na mbinu zozote hata kama ni za kijinga au hata kipumbavu tu.

Hawa ni wa ku face head on.

Vita dhidi ya Corona ni priority. Katiba mpya ni next.
 
dunia ya binaadamu huru,ila ina wapumbavu wanaohubiri uhuru wa mitizamo,lakini hawataki kuona wala kusikia mitizamo ya wengine.

kuna wakati nyumbu mnatafakarisha sana.
kwanini mnaamimi mitizamo yenu ni sahihi wakati wote,na haitakiwi kupingwa wakati wowote!!!
hoja zao zipo makundi yote,labda useme huzipendi,unazidharau,hazikufurahishi wala huoni kama zinakufaa wewe.

kwenye swala la katiba kelele ni katiba mpya,ila wenye akili huru wanahoji ni katiba mpya ama katiba yenye maamuzi ya wananchi ambayo yataheshimiwa na biongozi!!!!lakini ajenda ya vibaka imeeendelea kubaki ile ile katiba mpya.

kwenye corona kelele zimekuwa ni chanjo na tahadhali,wenye upeo huru wanahoji ufanisi wa chanjo na tahadhali inayotazamwa kuwa ni barakoa na kunawa mikono,maisha yetu haya ya kila siku hakuna kiumbe angekuwa anatembea saa hizi.

wakati watu wanatumia akili za kawaida tu kuhoji mambo,nyinyi hamtizamii katika uhuru wao.huu nao ni upimbi.
 
Ninakubaliana nawe:

1. CCM wote wanapinga katiba mpya. Hii ni kwa sababu ya ujinga, unafiki na pia kutokana na kunufaika binafsi na kama kundi kutokana katiba iliyopo.
2. Wanaopinga vita dhidi ya Corona ni CCM wote kuondoa wale walioko kwa Mama. Hawa wa mama ni wachache zaidi kuliko wale wa yule bwana wa legacy.

Wale wa yule jamaa wa legacy sehemu kubwa ni machinga, wapiga debe, vibaka, sungu sungu nk. Pamoja na kuwa na elimu duni, ni brainwashed hawajui wanataka nini au hawataki nini.

Kufanikisha agenda zao za kupinga vita ya Corona na/au katiba mpya wanatumia sababu na mbinu zozote hata kama ni za kijinga au hata kipumbavu tu.

Hawa ni wa ku face head on.

Vita dhidi ya Corona ni priority. Katiba mpya ni next.
Nakubaliana nawe vita dhidi ya Corona ni priority, Katiba Mpya ni next, coz Katiba Mpya bila watu haitakuwa na maana.
 
Nakubaliana nawe vita dhidi ya Corona ni priority, Katiba Mpya ni next, coz Katiba Mpya bila watu haitakuwa na maana.

Vita vya katiba mpya tutashinda. Lakini inabidi tuwe hai. Kuyaweka maisha yetu hatarini haiwezi kuwa option hata kidogo.
 
Hivyi ni nchi gani imepona Sasa baada ya kutumia njia za kitaalamu mnazotolea mapovu?
Mnajua maambukizi ya UK ya Jana pamoja na kuchanjwa? Au kubwabwaja tu.
 
Hivyi ni nchi gani imepona Sasa baada ya kutumia njia za kitaalamu mnazotolea mapovu?
Mnajua maambukizi ya UK ya Jana pamoja na kuchanjwa? Au kubwabwaja tu.

1. Wewe hutaki vita dhidi ya Corona
2. Pia hutaki katiba mpya.

#1 na #2 zinakufanya wewe kuwa chawa wa yule bwana na kwenye red yanakuhusu:

IMG_20210711_205649_038.jpg

Bila shaka una ID ya KIMKAKATI pia:

IMG_20210711_212052_743.jpg

Kawaambieni wanaowatuma tunawajua kwa tabia zenu wala hamtupi taabu.
 
Vita vya katiba mpya tutashinda. Lakini inabidi tuwe hai. Kuyaweka maisha yetu hatarini haiwezi kuwa option hata kidogo.
Kama wakati ule wa uchaguzi 2020 priority ilikuwa ni Lissu kuingia Ikulu bila kujali kuhatarisha uhai wetu basi nadhani hata sasa inawezekana pia priority ikawa ni katiba kwanza kisha inafuata corona. Nadhani Katiba ikipatikana kila kitu kitakaa sawa maana matumaini yetu yote na shida zetu zote suluhisho ni katiba mpya.
 
Back
Top Bottom