joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Ni ukweli kwamba jina la Magufuli limezidi kufahamika zaidi duniani tangu ulipozuka ugonjwa wa Corona na kuingia hapa Africa na hususan Tanzania. Magufuli aligonga vichwa vya habari duniani kwa uzuri na ubaya katika viwango vyenye kukaribiana.
Mwanzoni tu ugonjwa ulipoingia Tanzania, Magufuli alianza kupata shutuma na kurushiwa kila aina ya kebehi na matusi pale alipoamua kuruhusu ibada na kukataa kufunga mipaka ya ndani na nje ya nchi yake.
Kikomo cha kukashifiwa kilifika kileleni pale Magufuli alipokwenda kanisani na kurudia kusema kwamba, hatozuia wala kufunga nyumba za ibada kwa sababu anaamini virusi haviwezi kuishi na kuwadhuru watu Mungu.
Mara tu ya kumaliza kusema hivyo, dunia nzima ilimshukia na kumlaani Magufuli kwa kuchukua misimamo tofauti na nchi zote duniani, kwa kweli haikua rahisi sana kuvumilia kwa jinsi dunia ilivyomgeukia Magufuli, inahitaji mtu mwenye ujasiri wa pekee kuvuka bila kubadilisha msimamo baada ya kulaaniwa na dunia nzima.
Wakati dunia haijamaliza kulaani misimamo ya Magufuli ya kuruhusu nyumba za ibada na kutofunga mipaka ya nchi, Magufuli akaibuka na hili la kutilia shaka kuhusu vipimo vya Corona, ghafla jina lake likazidi kuwa gumzo duniani kote, ila safari hii sio kwa kukashifiwa na kukejeliwa, ila kwa kusifiwa na kupongezwa, sasa nchi, watu na makundi mbalimbali yamesahau jinsi yalivyomkashifu na kumuona mtu wa ajabu, sasa wanamuita ni mtu jasiri, makini na mwenye misimamo isiyoyumbishwa.
"Negative Energy"
Vyovyote vile iwavyo, ama kwa kusifiwa au kwa kupongezwa, kwangu ninahisi hayo yote aliyofanya Magufuli ni Mapungufu zaidi katika mapambano dhidi ya Corona kuliko kuimarisha na kuboresha mapambano.
1)Kuwaruhusu watu kuendelea kukusanyika katika Nyumba za ibada bila kutoa maelekezo na mifumo ya kufuatilia kuhakikisha kwamba maelekezo yanafuatwa, huo ni upungufu mkubwa has a ikizingatiwa kwamba, huko Rome na Makka kwenye vitovu vya dini hizi mbili, wamesitisha ibada baada ya kupoteza waumini wao.
2)Kitendo cha kuweka nguvu kubwa katika imani ya dini na dawa za asili na kutotilia mkazo katika maelekezo ya kitaalamu ya kuzuia maambukizi, ni kosa na Mapungufu makubwa.
3)Kuzuia na kukejeli unyunyiziaji wa dawa mijini na sehemu mbalimbali zenye mikudanyiko kwa madai ya kwamba haziui Corona, sio sawa kwa sababu zilisaidia kuua Mbu wanaosababisha Malaria na Dengue, alipaswa kuwashauri waongeze dawa yenye kujua virusi vya Corona (Sabuni au Alcohol).
4)Kutafuta na kujua ukweli dhidi ya Mapungufu ya vipimo vinavyotumika kupima Corona bila kutoa maelekezo ya nini kifanyike katika hiki kipindi ambacho vyombo mbalimbali vinachunguza, ni kuiacha nchi hewani huku wananchi wakiwa hawaelewi hali ya maambukizi inavyokwenda nchini.
Sent using Jamii Forums mobile app