Waafrika tunafanya kosa kubwa sana kuhusisha dawa za kitaalamu zinazotumika Hospitalini na wazungu, hizi sio dawa za wazungu ila ni dawa za kitaalamu zilizofanyiwa utafiti na watu wote wakiwemo wachina na wajapan japo wazungu ni wengi waliochangia na ndio waliozileta huku Africa kwa Mara ya kwanza.
Tofauti na hizi dawa zetu za asili ambazo Magufuli anazipigie debe ni kwamba hazifanyiwi utafiti wa kina, tunazitumia kienyeji mno, nilitegemea angeimarisha vitengo vya utafiti wa dawa zetu za asili ili ziweze kufanyiwa utafiti na kuboreshwa kabla ya kuzipigia debe.
Kwa kifupi Magufuli PhD yake, tena ya Sayansi haijamsaidia sana kumtoa katika mawazo ya kubahatisha maisha kwa kutegemea nguvu za kinadharia ambazo hazijathibitishwa ki-sayansi, kumbuka tupo katika karne ya sayansi na Teknolojia.
Kitendo cha Magufuli kwenda Loliondo na kushiriki kunywa kikombe cha babu ilikua dalili tosha ya kudhihirisha Mapungufu ya Magufuli katika eneo hilo la kuamini mambo ya hovyo.
Rais ni kiongozi wa nchi ambayo haina dini, kuna raia wenye kuamini dini na wasioamini dini, ni kosa kubwa kwa rais kusisitiza na kutenga siku maalumu za kumuomba Mungu, kazi ya kutangaza Mungu na dini angepaswa kuwaachia viongozi wa dini, mbona viongozi wa dini wanapozungumza siasa, Serikali inakataza na kusema wasichanganye dini na siasa, vipi yeye anachanganya uongozi na dini?.
Yeye lazima ajifunze kutofautisha imani yake na uongozi wa nchi, kuna watu ambao hawaamini Mungu, ukitaja Mungu wanasikia kichefuchefu, lakini katiba inawapa haki ya kutobughudhiwa, vipi rais anakuwa chanzo cha kuwabughudhi kwa kutajataja Mungu kila Mara?.
Sent using
Jamii Forums mobile app