Corona: "Media tunakufa kizungu na tai shingoni!", asante Waziri Mwakyembe kutambua mchango wetu. Serikali/jamii please do something, tutakwisha

Hii ndio comment yangu na mimi kwenye huu uzi.
 

Paskali,
Ulimhola bhabha ja mirimo?
Hizo ni salamu za wa kukaya Mwanza- Geita-Chatto.
Kwanza kabisa nianze na hayo malalamiko yako yote yalipaswa kuelekezwa kwa 'homeboyz' wako ambaye amejichimbia Chattle zaidi ya mwezi Sasa na haijulikani yuko likizo ya ugonjwa au amekimbia Covid-19. Tunajua Ikulu rasmi za Head of state Tanzania kwa Sasa ni Dar-es-salaam na Dodoma(Ikulu mpya).
Lakini la pili ni la kuhusu Waandishi wa Habari kukosa UHURU wa kuandika UKWELI wa Covid-19 tangu ianze kuwa reported Tanzania. Kumekuwa na usiri usioeleweka kuhusu janga hili kuhusu idadi Halisi ya Waathirika wa Covid-19, Vifo vingapi na Waliopona wangapi. Hapa ndipo penye tatizo.

Mimi kwanza ndo naskia toka kwako kuwa Kuna Wana media 10 wametangulia mbele za Haki tokana na gonjwa la Covid-19.Lakini homeboy wako hataki hizi habari zijulikane kwa Watz! Hii manake nini kama siyo mbinu ya kuficha udhaifu wa Serikali kwa kushindwa kukabiliana na Covid-19?

Kama ni kweli kuna wanahabari 10 wameondoka kwa Covid-19 unaowajua wewe peke yako, manake ni kwamba the death magnitude ni kubwa sana kuliko hizo Takwimu za Ummy Mwalimu (Vifo 16 tu!) Unless uniambie kuwa Kati ya hivi vifo 16 na hao 10 ni katika idadi hii kitu ambacho siyo kweli.
Kuna Wabunge 3, Kuna Wakuu(W) 2, Kuna masheikh 2 na Kuna Wachungaji 2 na kuwa wale waliokuwa Wanazikwa usiku kwa Ambulance nchi nzima.

Leo ni zaidi ya wiki hatujasikia any Update toka Serikalini! Si Ummy Mwalimu, si Majaliwa, si Suluhu Hassani wala Jiwe mwenyewe!! Wote kimya na huu ukimya una walakini!!
Kuna Hoja dhaifu sana ya ATI M MAABARA YA TAIFA INAFANYIWA MAREKEBISHO....!Hili linashangaza sana. Kigezo kuwa Test Kits za Covid-19 Zina kasoro ni kujaribu kupoteza malengo na kuhamisha mawazo ya Watz kwenye focus ya Covid-19!

Madai ya Jiwe kuwa Kits ni mbovu au zinatumika na Mabeberu kuihujumu Tanzania hazina mashiko! Hizi Kits ziligawiwa kwa nchi zote za Afrika Kama msaada toka kwa Bilionea Jack Maa(China). Nchi za Waafrica wenzetu wanapima kila siku na wanatoa Takwimu every after 24 hours kinyume kabisa na Tanzania Bara. Kwa ndugu zetu wa Tanzania Visiwani wanatumia the same Test Kits na wanatoa update every after 24 hours.

Sisi Tanzania Bara badala ya kupima watu wanaodhaniwa Wana Covid-19 tumeacha na KUANZA kupima Kondoo, Mbuzi, Kware, Mapapai na Mafenesi na sijui nani alimwambia Mkulu kuna Covid-19 mpaka kwenye Mapapai na Mafenesi. Utasema Papai limekutwa na Covid-19. Is it logical? Yawezekana kabisa huyu mtu aliyekwenda kununua hayo mapapai na kuandaa hizo samples alikuwa na Virusi au mwuzaji wa Mapapai Ni mwathirika wa Covid-19, how can you draw a conclusion kuwa Kits Ni mbovu?
But we can put the test the other way round. Kwamba huyu aliyechukua sample za Mapapai na Mbuzi yeye alikuwa amedhamiria kwa maksudi kuonesha kuwa Kits hazifai hivo akapandikiza virus wa Covid-19 ili apate kisingizio kuwa Kits hazifai ili apate hoja ya kukwepa lawama?

Tatizo la Watz wengi kukosa Critical Thinking za kuweza challenge hoja dhaifu toka kwa Watawala. Hapa ndipo Media inapotakowa kuingilia Kati kwa kuhoji issues,kudadavua na kuweka Mambo hadharani. Waandishi Habari wengi wa Kitanzania hawanaga ile kitu inaitwa Critical Analyis au Investigative Journalism na badala yake Waandishi wengi wamebakia kuwa Wapiga Filimbi wa Harmelin tu.
 
Pascal waandishi wetu hamjafanya lolote na hata mkifanyiwa au kuwezeshwa lolote hamuwezi kufanya lolote.
Ona wewe uliye nguli na unaweza kupata nafasi ya kuongea Live katika TV na waziri bado unajua idadi ya waandishi 10 mmewazika kwa ugonjwa huu na bado takwimu za Taifa zinasema jumla ni 16 na hamumbani waziri inakuwaje?
Yaani amongst 55 millions wanakufa Watanzania 16 na kati yao 10 ni waandishi na 6 ni aina zingine za wananchi! Hapo eitha waandishi ndio kundi hatari sana kupata maambukizo kuliko hata wahudumu wa afya au idadi ya vifo imedanganywa kwa kiwango kikubwa sana na serikali Bali iko kwa maelfu.
Sasa mumehoji?
Hivi kesho asubuhi vyombo vyote vya habari vikifungwa Tanzania tutaathirika kweli? Maana kwa sasa habari za kiuchunguzi hazifanyiki imebaki mitandao tuu kupiga story na watu wanajua kinacho endelea badala ya waandishi kufuata majibu na kuhoji.
Magazeti, redio na TV wamekuwa Praise team na hawahoji lolote kama enzi zile zilizopita.
Ukiacha korona, mambo mengi yanatokea lakini hayahojiwi. Hivi hakuna mwandishi wa kula sahani moja na mkurugenzi Ubungo kumuuliza ukipokea barua hata ya kugushi unaifanyia kazi tena ya kumuondoa bosi wako meya? Anakomaa mpaka apate jibu. HAKUNA.
AG bungeni akaulizwa jee hiki alichofanya Spika kiko sawa kikatiba? Hakuna mwandishi.
Kabudi akaulizwa, toka lini tumefuata madawa nje ya nchi kwa gharama kisha kuja eti kuyapeleka NIMR kwa utafiti? Kwa nini tusisubiri WHO watoe ithibati yao? Na mbona Rais alisema dawa hiyo iko tayari na Kabudi aliinywa ikiwa bado sample?
Waandishi (I mean wenzako) waendelee na habari za udaku na kusifia sifia maana hakuna jipya na hayo haya hitaji kuwezeshwa.
Majuzi nilikuwa nazungumza na msomi mmoja akaniambia VYOMBO VYA HABARI VINA MCHANGO MKUBWA SANA KUDIDIMIZA DEMOKRASIA na KUKWAMISHA MAENDELEO kwa ushabiki wao.


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Chakaza,
Nakubaliana na hoja zako kwa 100 pc!
Mfumo wa Habari Tanzania umevurugwa na Wanasiasa. Ni kweli media Tanzania is just a Praise& Worship team to the 5th Term CCM ruling Party under Magufuli!
Hakuna kuhoji ukiukwaji wa Katiba, Sheria wala Kanuni tulizojiwekea Watanganyika!

Kwa sasa inaonekana Tanzania Zanzibar imeanza kuipiku Tanzania Bara kwene Mambo mengi sana ya msingi! Hili la Covid-19 limeonesha rangi na udhaifu mkubwa sana kwa TZ Bara chini ya Magufuli and yet people just keep on Praising & Worshipping! Kama Taifa kwa Hakika tumepoteza mwelekeo!
Nimemsikia Barack Obama Rais wa Marekani(rtd) akimlaumu Rais Trump kwa kutochukua hatua madhubuti kuzuia Covid-19 Marekani kiasi Cha kuathiri mamilioni ya Wamerekani na vifo zaidi ya 70,000 mpaka sasa!

Ukija Tanzania Marais Wastaafu wote kina Mzee Mwinyi, Mkapa na J.Kiwete ni kama vile hawapo duniani! Ni aibu sana kwa Utawala huu wa CCM.
 
The problem is that the media society is not properly organized in Tz. Who officially represents the media group? Which is the spokes-body?
 
Kumbe @johnthebatist kuna wakati unafikiri vizuri namna hii mkuu!? Huko usukuleni unafanya nini!?
Zaburi 1:1 - 6 inakuhusu.
e
 
Jemedari wa vita kajificha kwao ndio maana mambo mengi hayaendi vyema. Pia waandishi msijikite sana kwenye kusifia mtaumia sana, semeni waziwazi mnachotaka badala ya kusifia sifia watu wasiofanya kazi zao vizuri.
 

nakumbuka last time ulituambia umeacha kazi ya journalism na umegeukia siasa...vipi bado haujampata polepole tu...
 
Nchi hii imejaliwa kuwa na wanasiasa wasio na aibu kabisa.

Huyo mzee pamoja na kwamba ni waziri lakini anaona fahari kusifia tu hali ngumu ya waandishi wa habari na vyombo vya habari.

Anyway mimi nikupongeze Paschal Mayalla kwa kujitoa kwa nguvu zote kama mwanahabari kutoa elimu juu ya janga hili la corona.

Ila mfikishieni ujumbe Mwakyembe awamu ya tano pamoja na yeye mwenyewe Mwakyembe wameshiriki kwa mikono yao kuhujumu tasnia ya habari ambayo ilianza kuimarika sana na kuwa na mchango chanya kwa jamii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanahabari kwa sasa ni Mange, Kigogo na Haule.

Takataka nyingine zote ZIKO zinasikilizia TEUZI
Ni kweli kabisa.
Ila jamani mie sasa sina hofu tena, baada ya ndugu yangu kupata,na sasa yupo fit, na ajaenda hospital, Kwa kuwa alikuwa na hofu ya huduma, na aliniambia kuwa nikienda hospital nitakufa. Aliendelea kutumia mchanganyiko wa abdalasini, vitunguu swaumu, tangawizi na limau , anasaga kwenye blender na kuchemsha, anakunywa baada ya kuchuja na joto kama juice, alipobanwa na pumzi alitumia kitunguu maji alisaga na kuchemsha anakunywa ikiwa ya vuguvugu,.
Pia aliendelea kujifukiza kwa alovela, mwarobaini na majani ya mpapai.
Ila nashauri tumia na pen-v, kwa kuwa kunakuwa na vidonda kooni kukufanya kupata tabu wakati wa kula. Baada ya siku nne ya matibabu yake nilimshauri atumie na pen -v, ila kama wewe anza mapema pen-v.
Hivyo kwa upande mwingine maelezo ya mh. Rais ni sahihi pia. Maji baridi usitumie!
Covid-19 tunaweza kuishinda tukipeana na mbinu mbalimbali,
-taadhali usiniulize alipimwa wapi kwa kuwa dalili zinajulikana na ikikushika ni mafua, kukosa nguvu, kuuma koo, kuuma kichwa, chafya, mwili kuuma.
 
This is rubbish! Total rubbish from Jemedari Mkuu! (not you, pascal) Issue ni kuwa unaweka lockdown kuzuia kusambaa. Ukifankikisha hilo, then unakuwa umejenga uwezo wa hospitali zetu ku handle cases chache zitakazojitokeza. Ukishafika hapo kuwa sasa virus hawasambai, then una ease lockdown. . .. maisha yanaendelea. Kuna some states in the US zimelegeza masharti na LEO maambukizi na hospitalization zimerudi kupanda!
Huondoi woga wa raia kwa kuwa expose kwenye mizinga. Unawaambia kuwa kuna mizinga, itapigwa msiogope, ukisikia mingurumo kimbilia handakini! Tumefundishwa hivyo wakati Id Amin. hapakuwa na taharuki. Tuliambiwa kuna vita fanya moja, mbili, tatu! Hatukuachwa na kuambiwa kuwa hakuna vita!
Mbona woga upo maana watu wanaona watu wanakufa sana! Kila kaya inakwenda kuguswa kama ukimwi ulivyogusa kila kaya, sasa utasemaje hakuna woga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…