Corona: "Media tunakufa kizungu na tai shingoni!", asante Waziri Mwakyembe kutambua mchango wetu. Serikali/jamii please do something, tutakwisha

Diversification siyo mbaya! Sioni kosa la Pascal Mayalla .
 

Big up and kudos!
Mimi huwa nacheka sana ninapomsikia Jiwe akidai kuwa watu wasiwe na HOFU maana hofu ndo inaua kuliko hata Covid-19....!!!
Lakini huyu Jiwe Leo ana zaidi ya mwezi kakimbilia Chattle kwa hofu ya Corona....!!!Mbona hajata?
Jemedari na Amiri Jeshi Mkuu anawahamasisha Wapiganaji wasiwe na HOFU risasi na mabomu zikiwapiga wasonge mbele tu ilhali yeye yuko ndani ya Handaki amejificha! This is purely Kenjikitile policy of confronting the enemy!
What kind of a Commander-in-Chief?
 

Mkuu johnthebaptist unadhani tumechelewa sana kumshauri Pascal Mayalla ajikite kwenye taalum yake ili angalau alete ahueni kwenye sekta hii ya Habari ambayo kwa sasa wapiganaji wake wameingia mitini?. Wamebakia wanachungulia kwa Mbali, wakiona hata jani linapeperushwa na upepo wanatimua vumbi.

Nimemkumbuka Mwangosi
 
Well said bro.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatujachelewa bwashee..... Na vile kwa sasa yuko na Dotto Bulendu anaweza kumakinika zaidi!
 
Nimependa argumet yako, perfect!
 
Tundu Lissu aliwahi kusema "Hakuna aliye salama", yani huu utawala huu sijui hata unajihisi uko kwenye karne ya ngapi, Mayalla tatizo lenu waandishi wengi mmekuwa upande wa serikali zaidi mkijua watawalindia taaluma yenu. No One Is Safe.
 
Kaka yangu Paskali,
kwa muda mrefu toka JKN ameondoka sekta ya huduma imekuwa kwa kasi sana pasipo uwiano sawa na sekta ya uzalishaji kupitia viwanda.

Sekta ya huduma ni kama real easte, banking, insurance, media, legal, port, logistics ni vitu kama hivyo
Sekta ya ulazima wa uzalishaji (manufacturing) kwa viwanda kukidhi uhitaji wa soko ndani na nje ili service sector ambayo ni suppotive kwa manufacturing ifanye vyema.

Fikiria kidogo kwa mifano mitatu, kama sukari ingezalishwa kwa walau tani laki 7 wakati mahitaji ya ndani ni tani laki 5; bila shaka sekta ya habari na matangazo ingefanya promotion ya kwanini ununue sukari ya "kilimatinde" kwa ujazo wa gm100, gm 250, gm 500.

Sekta ya logistics na distribution watu wangekuwa wanapambana kwanini uwe wakala wa kilimatinde sugar.
Say, tungekuwa na stable sector kuzalisha maziwa na products za maziwa kama maziwa fresh, mtindi, butter, yogurt wingi. Lots promotion za products za maziwa zingefanyika hata kama Covid ingekuwepo; maana bado watu wanakula na kunywa.

Kuna maziwa kama haya toka Oman yanaingia na hayana promotion kwenye any media. Na kuna wakati unayasaka madukani huyapati. Kuna hela inapotea kwa imports kumbe ujanja ni kuzalisha kwa wingi.




Mzigo hii hapo juu kwa uchache tu, tuna import yote na kuna products katika hizo hakuna kabisa of promo kwa radio, tv, magazeti, twita, instagram au facebook kwa waandishi wa Tanzania.

Sasa basi, JPM anaposema lazima twende kwenye kujenga middle class kwa kutumia viwanda; hata waandishi wa habari wanakosa depth ya analysis maana kuna mambo yanafanyika nchini; media inachukulia poa including ku-import penseli, toothpick.

Hayo mambo yangeshadadiwa sana na media, hata kwa BOT kutoa bank guarantee kwa investments ambazo right away soko lake lipo.

Najua kwa ujumla services sector ita-suffer including media. Ila ili tutoke kwa haraka, chonde chochonde, tumtafuteni huyu mzee wa Chato ili suala la viwanda hasa kwa consumables liwe top priority.

Your browser is not able to display this video.


















Wakati Paskali mko Ikulu ninyi wana habari, huyu mzee alisema hivi... Hapa Pasco niambie uko wapi ili tumtafute Msigwa walau tuje na investment ya Sukari kwa kutumia sugar beet kama raw material. Walau tuzalishe hata tani kadhaa.

Tutarejesha mkopo wa uwekazaji na ku-share model kwa wengine nao waingie, kwa soko ambalo lipo wazi kuziba pengp la imports, tutatoa room ya media ku-promote sukari yetu etc etc etc

It breaks my heart baadhi ya biashara including viwanda vingi zinaendeshwa na "wa kuja" na wana roho mbaya kwa jinsi walivyow wabaguzi. Hawana hata nia ya kukupa PPR tangazo maana wanaona utafaidi sana.

Kama vip, twenzetu Chato na project yetu mkononi (ha haaa)
Fred
 
Hili tukio la mkuu wa nchi kukimbizwa kwenda kijijini ni kutangaza kuwa kuna gonjwa la hatari sana.

Tukio la kukimbia toka mjini kutokana na gonjwa ni marudio katika historia ya binadamu katika harakati ya kujiokoa.

Katika muhadhara wa public health katika chuo Kikuu maarufu cha Yale, Prof. Snowden anasimulia.

Hivyo tulioachwa mijini tukio hili tusilichukulie kwa urahisi bali ni ujumbe tosha tuchukue tahadhari kwani mkuu wa nchi ameshauriwa ahame kwa muda toka Dar es Salaam na Dodoma ktk mawe kwani kuna hatari kubwa ya gonjwa hili hatari.
00:00 - Chapter 1. Responses to the Plague and Miasmatism 09:05 - Chapter 2. Individual Measures of Self-Protection and Scape-Goating 18:52 - Chapter 3. Religiosity 25:51 - Chapter 4. Organized Public Health Measures 37:25 - Chapter 5. Did the Public Health Measures Succeed?
Source: Yalecourse
 
Duh, mbona kama hili lina ukweli

Ila umenivunja mbavu hapo kwa mwanajeshi.

Anyway, mkuu Pascal unazungumziaje hii hoja ya kada mwaminifu 'Joni?

Sent using Jamii Forums mobile app
 


Poleni sana na mlipwe kwa kazi zenu na tuombee kampuni ziwape matangazo kwenye kazi zenu. Sio vizuri kutoa kazi bure kila siku
 
Mimi si walaumu waandishi wa habari bali system ya nchi. Naamini waandishi wana uwezo mkubwa wa kutafuta habari na kufanya analysis lakini kwa hali halisi ya nchi yetu hilo ni gumu. Kwa vile bado demokrasia hatujaweza kuifuata kikamilifu waandishi endeleeni hivyo hivyo kusifia musizitafutie familia zenu matatizo. Hawa viongozi ni makatili sana wao wanawaza matumbo yao tu hivyo hawaoni tabu kutoa uhai wenu. Si tumeona waandishi mahiri walipojaribu kutafuta habari ama kufanya analysis nini kimewapata. Wengine wamepotea na wengine kusweka rumande na sisi wananchi tulibweka wiki mbili tukawasahau. Paskali wewe angalau unatumia real id ila hao wanaokulaumu humu wanatumia fake id.
 
24 May 2016
Public Health Care Communication and Advocacy Systems - Prof. Dr. John Kabudi, Ph.D. AUSN

Public Health Care Communication and Advocacy Systems - Prof. Dr. John Kabudi, Ph.D. AUSN Visiting Professor of Indigenous Knowledge Systems (Faculty of Law, University Dar es Salam, Tanzania) - Public Health Care Communication and Advocacy Systems. Explore scholarships for postgraduate study at American University of Sovereign Nations

Source : American University of Sovereign Nations
 
Pascal Mayalla,

Prof. P. Kabudi : Mtu ni Afya, Mitishamba, Dawa Asili, Tiba-Lishe, Mahali pasipo Daktari ktk muda huu wa Covid-19

Unaona video clip hapo juu Prof. Palamagamba Kabudi ambaye pia ni mwandishi wa habari mstaafu akielezea umuhimu wa kitu kinachoitwa Afya ya Jamii ambayo kazi kubwa wenzetu mabwana / bibi Afya wa halmashauri, wilaya na miji wanaifanya kuhakikisha makaazi yeti hayawi hatari kwetu sisi wenyewe na jirani zetu pia.

Ningependa kuona waandishi wa habari kuwahoji hawa wataalamu wa Afya ya Jamii (Public Health) wanavyopanga na kutekeleza mikakati hii ya kupambana na Covid-19 wakishirikiana na matabibu, waganga, wanasiasa na wadau kama sekta ya Uandishi habari ili tuishinde vita hii.

Hivyo kama Prof. Palamagamba Kabudi kila siku anatukumbusha tusome historia na kuacha kulaumu mfano mbona Prof. Palamagamba Kabudi kenda Madagascar wakati Ummy Mwalimu yupo n.k kumbe Prof. Palamagamba Kabudi ana mambo mengi zaidi ya fani ya sheria na ndiyo maana tunamuona mstari wa mbele ktk hata masuala ya Public Health kupambana na Covid-19
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…