Corona: Sudan ya Kusini hali ni tete, tuwasaidie. Uzoefu tunao

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Hali ni mbaya sana Sudani Kusini kuhusiana na huu ugonjwa. Kama ilivyokuwa kwetu na kugongelewa vilivyo na Mh. Makonda: "Watu huko wanapukutika kweli kweli." Hii siyo siri ya kuficha tena.

Ndani ya mwezi mmoja tu hali iko hivi:

Horror as South Sudan Loses 35 Generals, Senior Officials in one Month

Sembuse kina ka*amba nani wa huko?

Kama ilivyo ada, wale wenye kubarikiwa mioyo ya ajabu hakuna kinachoweza kuwastua. Lakini ni wazi kuwa hali hizi si za kawaida.

Kwa vile stage hii tulishakuwemo na hatimaye kuipita salama, ni wazi kuwa tunao uzoefu wa kugawana na hawa wenzetu. Hawa ni wa matumbi tu na ndugu zetu wa damu.

Kutoa ni moyo si utajiri.

Tungeweza kuwakaribisha wagonjwa wao ili kuwapigisha nyungu vilivyo. Ikibidi, tungeweza kuwazukia huko huko juu kwa juu na kwenda kuwafanzia yale mambo yetu.

Kuwatelekeza wenzetu katikati ya janga kama hivi wakati sisi dawa tunayo haitakuwa sawa. Tukumbuke kuwa japo tulikuja kuwa na mashaka, Madagascar walikuwa tayari kutusaidia dawa iliyokuwa imethibitishwa vilivyo.

Mungu ibariki Afrika.
 
Ukisomaaaa

Historia ya CORONA lazima waende wakubwa kama hawaa baadaye Jamba NANII inaishia kwa matajiri hapo utasikia imepunguaaa sasa usiVae baraK
uone mnazKana kimyakimya
 
Hali ni mbaya sana Sudani Kusini kuhusiana na huu ugonjwa. Kama ilivyokuwa kwetu na kugongelewa vilivyo na Mh. Makonda: "Watu huko wanapukutika kweli kweli." Hii siyo siri ya kuficha tena.

Ndani ya mwezi mmoja tu hali iko hivi:

Horror as South Sudan Loses 35 Generals, Senior Officials in one Month

Sembuse kina ka*amba nani wa huko?

Kama ilivyo ada, wale wenye kubarikiwa mioyo ya ajabu hakuna kinachoweza kuwastua. Lakini ni wazi kuwa hali hizi si za kawaida.

Kwa vile stage hii tulishakuwemo na hatimaye kuipita salama, ni wazi kuwa tunao uzoefu wa kugawana na hawa wenzetu. Hawa ni wa matumbi tu na ndugu zetu wa damu.

Kutoa ni moyo si utajiri.

Tungeweza kuwakaribisha wagonjwa wao ili kuwapigisha nyungu vilivyo. Ikibidi, tungeweza kuwazukia huko huko juu kwa juu na kwenda kuwafanzia yale mambo yetu.

Kuwatelekeza wenzetu katikati ya janga kama hivi wakati sisi dawa tunayo haitakuwa sawa. Tukumbuke kuwa japo tulikuja kuwa na mashaka, Madagascar walikuwa tayari kutusaidia dawa iliyokuwa imethibitishwa vilivyo.

Mungu ibariki Afrika.
Hawa hawana ujanja wa kuficha takwimu na kuzika usiku ndio maana yanawakuta madhila haya.
 
Propaganda hizi, nendeni mkawape pole Italy, Spain na USA, Afrika tuachwe kama tulivyo
 
Labda kama wewe ndiye pekee mwenye hati miliki ya uafrika. Lakini kama si hivyo ujasiri wa kuwasemea waafrika wote hadi kina Museveni, Kenyatta, Kagame, Ramaphosa nk bila ridhaa yao unaupata wapi mkuu?
 
Hawa hawana ujanja wa kuficha takwimu na kuzika usiku ndio maana yanawakuta madhila haya.

Wanahitaji ma consultants wa hii kadhia. CCM chama dume could be one.
 
Back
Top Bottom