Corona Virus tishio la pili kubwa baada ya 9/11 katika sekta ya utalii

Corona Virus tishio la pili kubwa baada ya 9/11 katika sekta ya utalii

Cvez

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2018
Posts
4,405
Reaction score
13,411
Katika mwaka ambao sekta ya utalii itapata msukosuko ni huu hasa ukizingatia utalii si basic needs. Baada ya 9/11 Corona virus ni pigo la pili kubwa kuikumba sekta hii.

Kutokana na takwimu za tovuti maarufu ya safari barani Afrika Safaribooking, kumekua na anguko la karibia 6% kutoka kipindi cha mwezi February na 10% kwa mwezi huu wa March kutokana na tishio la virusi vya Corona.

Mbali na kupungua kwa bookings pia watalii wengi waliofanya bookings kipindi cha nyuma kabla ya kuibuka kwa Corona wanahofia usalama wao hivyo wengi wao aidha wanacancel bookings au wanasogeza muda wa safari zao.

Ingawa Tanzania bado hakuna hata mgonjwa mmoja aliegundulika na ugonjwa huu bado tupo katika hatari ya kupoteza mapato kutokana na janga hili. Utalii huchangia 17% ya GDP ya Tanzania.

Ambapo utalii wetu kwa asilimia kubwa tunategemea wageni toka nje. Mpaka sasa ukiangalia zile nchi zinazoleta watalii (Tourist Generating Countries) nyingi zimeathiriwa na Corona.

Mbaya zaidi Tanzania haina direct flights kutoka nchi mbalimbali hivyo wageni husimama katika nchi nyingine kabla ya kufika, na moja ya maeneo hatarishi zaidi kwa sasa duniani ni viwanja vya ndege.

Ni jana tu serikali ya Zanzibar imepiga marufuku ndege kutoka Italy, na kutokana na takwimu wageni wengi wa Zanzibar ni kutoka Italy. Pia travel restrictions kwa wageni za China,South Korea, Iran na Saudi Arabia nazo zitaathiri kwa kiasi kikubwa.

Kwa upande wa Tanzania bara katika kipindi cha miaka miwili iliyopita serikali na wadau wengi wa utalii waliweka juhudi sana katika soko la China, ambalo ndio limeharibika zaidi.

Hivyo kwa kipindi hiki wale wote wanaohusika moja kwa moja na sekta ya utalii wapo katika hali tata zaidi tutashuhudia kupunguzwa kwa wafanyakazi ama kufungwa kwa hoteli, migahawa, kampuni za utalii, na maduka ya souvenirs (vinyago, shanga, vito n.k).

Endapo ugonjwa huu utaendelea kuongezeka kwa kasi hii iliyokua nayo itachukua miaka kwa wageni kua na imani ya kuanza kutembelea vivutio mbalimbali.
 
Hichi ndo kipindi tunahitaji kudra za Mwenyezi Mungu maradufu zaidi.
 
Hichi ndo kipindi tunahitaji kudra za Mwenyezi Mungu maradufu zaidi.
Hapo nimezungumzia utalii lakini uchumi wa nchi ni muunganiko wa sekta mbalimbali kuanguka kwa utalii kuna sekta nyingi tu nazo zitakua katika hali ngumu.
 
Again sasa yametimia tulikua tunahisi Tanzania ni safe haven... Ila kinachoendelea sasa ni cancellation ya bookings, kufungwa kwa migahawa na hotels, tour companies, dereva tax, na tour guides wote wapo out of jobs.
 
Back
Top Bottom