Moja kwa moja kwenye mada:
Majirani zetu Kenya, Rwanda na DRC tayari wamesha ripoti kuwapo kwa wagonjwa wa corona katika nchi zao.Kwa hali hii ni wazi kuwa hapa kwetu ni suala la muda tu sasa.
Wenzetu, katika nchi nyingi kutegemeana na ukubwa wa tatizo wame kuwa wakichukua hatua kadhaa katika kusaidia udhibiti wa ugonjwa huu. Baadhi ya hatua zilizoishachukuliwa ni:
1. Kuwekwa quarantine kwa wageni wote tokea nchi zenye kufahamika kuwa na wagonjwa kwa takribani siku 14 kabla ya kuruhusiwa kuingia katika nchi nyingine wanakotaka kwenda.
2. Ndege za moja kwa moja tokea nchi zenye wagonjwa zimesitishwa kuelekea nchi zingine.
3. Mikusanyiko ya watu: kwenye mashindano ya mpira, matamasha, makanisani, misikitini nk imesimamishwa.
4. Taratibu za mambo ya kodi kwa wananchi zimecheleweshwa kuwapa wananchi ahueni kwenye kujikimu kuhusiana na mdororo wa uchumi kwani takribani shughuli zote za uzalishaji mali zimesita.
5. Sehemu za wazi kwa ajili kunawa kujiweka salama zimewekwa katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu.
6. Namba za simu za kupiga mtu anapojishuku kuwa na dalili za ugonjwa zimewekwa wazi.
7. Nk
Hapa kwetu ninaamini pamoja na #4 serikali ingepanga kusimamisha kwanza shughuli zote za miradi mikubwa hasa ya SGR na stigglers gorge.
Hatua hii itatupa nafasi kutambua udharura uliopo kuhusiana na ugonjwa huu.
Tuachane na makesi kesi, chuki na magomvi yasiyokuwa na vichwa wala miguu. Tutambue sote kwa umoja wetu sasa tumekabiliwa na adui mmoja hatari mno anayetishia uwepo wetu kama taifa.
Ni heri tukawa hai bila ya SGR au stigglers gorge kuliko kuwa navyo hali tumeangamia sote kwa Corona.
Nawasilisha.