Corona Virus: Watanzania hawata wasamehe ugonjwa huu ukifika nchini

Tatizo ni kuwa hatujaambiwa wala kuonyeshwa vituo vilivyopangwa kwa ajili ya kutibu waathirika.. na je mtu akihisi kuwa na dalili afanye nini? aende hospitali au atoe taarifa afuatwe alipo?na vipi kuhusu wale raia wanaopanda daladala? Utaratibu ukoje kuhusu kutogusana? Na vipi kuhusu mask za kukinga pua, zinapatikana wapi? Maelezo ya kina ni muhimu sana... walau kenya.wao wameshaandaa vituo ya kuwatibu wale watakaoathirika..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rwanda wameweka mpaka sanitizers mtaani badhi ya sehemu.

Hapa kwetu nashangaa Rais alikuwa anataka kupeleka madaktari huko china?
Sio futuhi hii kweli?
 

Ni kweli kabisaa, huko mipakani ndio kabisaaa, maaana huwezi elekeza macho ktk viwanja vya ndege tu bali hata ktk mipaka yetu ambayo inaonekana hakuna uthibiti wa kutosha, hii inatia wasiwasi kama tutabaki salama!
Kwa kweli serikali yetu inapaswa iongeze jitihada ktk maeneo ya viwanja vya ndege Na mipakani. Haswa mipakani,
Kila siku tunaona wahamiaji haramu wanakamatwa wakiwa katikati ya miji....sasa kama wana corona sitayri wamesha tuletea?!! Jamani vyombo vyetu vya ulinzi Na usalama ongezeni umakini haswa ktk kipindi hiki CHA tishio la virusi vya korona.
Mungu ilindwe Tanzania Na majirani zetu
 
Sasa umejuaje kama ipo wakati inachelewa kuonyesha hivyo viashiria...?

Kuna case yeyote iliyorepotiwa kuonyesha huo uwepo wake hapo Tanzania?




Sent from my iPhone using Tapatalk
Kama watu wanaingia nchini na hawapimwi unategemea miujiza ama na wametoka kwenye zone ambazo zina waathirika ....nunua sanitizer zako na mask epuka direct contact acha ubishi mkuu.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inawezekana corona ya TZ ikawa na dalili tofauti kama zinazoonekana kwa bashiru manake sio kwa pumba zile....



______________[emoji36][emoji2958]_______________
" With or without religion, good people can behave well and bad people can do evil; but for good people to do evil - that takes religion.
 
We've bullshit leaders.God have mercy on Tz. For sake of My God and my country we believe these diseases corone will never exist in..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeogopa sana pale niliposoma eti Italy wamegundua wagonjwa wapya ambao wame test positive lkn wote hawana dalili yeyote ya ugonjwa kwakweli ni hatari

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Ukiisema au kuikosoa serikali ya ccm unahitwa kibaraka wa mabeberu na polisi, viongozi wa chama na serikali wote macho, masikio na nguvu zote zinaelekezwa kwako.
Kwenye hili la Corona, watu wanaleta siasa na kuona kama anayesema madhara ya korona ni wa chama pinzani.
Siku likitibuka hata huyo anayetaka kuwa kiongozi wa malaika hatasalimika.

Mimi nashauri tu, waache siasa kwenye mambo ya msingi na yatakayoigharimu nchi na wananchi.
 
Mkuu

Huwezi kutoa hoja zako bila Matusi?

Nina mwaka wa 12 hapa jukwaani bila kupewa BAN,

chonde chonde usitafutie matatizo.




Sent from my iPhone using Tapatalk
Mkuu, MPUUZI sio tusi, ni cheo, ni kama vile DIWANI, MWENYEKITI, MKURUGENZI n.k.
Jina mbadala la mpuuzi ni MJINGA. Na mara zote MJINGA hukasirika anapoitwa MJINGA.
Kuliko kuanza kulia lia kwamba umetukanwa ni bora ungethibitisha kuwa wewe sio MPUUZI/MJINGA.(natanguliza samahani)
 


Sawa umeshinda.

Shukrani!


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Hivi Nyie wenzangu huwa mnadhani serikali za kiafrica zinafanya kazi ...

Sent using Jamii Forums mobile app

Unajua sisi huku kwetu watu hasa viongozi wanajipa moyo kwamba hili tatizo haliwezi kufika. Au kwamba likifika halitawaathiri wao. Kwahiyo wanapuuzia. Pia kuna ile mentality yetu kwamba dawa itapatikana kabla hatujaathirika.
Lakini kiuhalisia ukijaribu kuchunguza utagundua kwamba nchi kama ya kwetu ipo katika hatari kubwa sana ya kupatwa na hili janga kuliko tunavyoweza kufikiri kutokana na muingiliano mkubwa wa watu. Na kiukweli kama janga hili litafika, madhara yake yatakua makubwa maana nina wasiwasi sana kama tuna uwezo wa kupambana nalo kama nchi nyingine wanavyofanya.
We fikiria mfano leo hii corona itue dar. Dar kuna watu wapatao 6.5 milion, niambie kuna vituo vingapi vya kuhudumia waathirika? Kuna mask ngapi? Hao wahudumu wenyewe wako wapi na je wana vifaa? Utazuiaje ugonjwa unaoenezwa kwa hewa usienee dar? Kwenye daladala, mwendokasi, mitaani? (Chukua mfano wa mtaa wa kongo pale)? Haya, je unaweza ku quarantine mkoa kama dar, useme watu wasiingie wala kutoka? Leo hii ukitangaza kwamba hakuna mtu kuingia wala kutoka dar, nini kitatokea?
Sisi tungekua na akili, tungefanya kila liwezekanalo kuzuia huu ugonjwa usiingie, maana ukiingia sidhani kama kuna mtu atabaki.
 
Naamini Mungu atauruhusu uingie ili iwe kipimo cha Utovu wa nidhamu kwa kushindwa kuzingatia hatua za tahadhari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…