Sasa kama ni hivyo basi hakuna tofauti kati ya TZ na KE. Hata huku Kenya, serikali ikitaka shamba inaichukua na kukulipa fidia kama ilivyofanya wakati wa ujenzi wa SGR.
Tofauti ni kwamba, Tanzania ardhi yote ipo Chini ya Serikali, hata kama inamilikiwa na mtu binafsi lakini sheria na taratibu za matumizi yake zinaratibiwa na kudhibitiwa na Serikali, kwa mfano japokua ardhi ni yako lakini lazima uitumie, usipoitumia kwa zaidi ya miaka 3 sheria inaruhusu Serikali kuichukua na kumpa mtu mwengine bila kulipwa chochote, pia ukitaka kuiuza lazima ufuate sheria za nchi, kwamba huwezi kumuuzia mtu ambaye sio raia wa Tanzania.
Mi hata nashangazwa na huyu jamaa, pale mwanzo mwanzo alitutusi sana kwavile Kenya ilikua ishapitisha kesi 100 za corona wakati Tanzania ilikua na kesi kama 11 tu... Alafu ghafla kesi za Tanzania zikapanda hadi 87 jamaa akahepa akashindwa kujitetea, mda si mwingi Tanzania ikaishinda Kenya kwa kesi za corona, jamaa kapotea karibu mwezi mzima akificha aibu, alafu hivi Tanzania imeacha kutangaza Kesi zake mpya wakati Kenya inatangaza kila siku, sasa inakaa kana kwamba Kenya imechukua tena uongozi wa kuwa na kesi nyingi, jamaa linajiregesha tena na kuanza kutusi wakenya wakati Tanzania ina siku nane(8 days- yani zaidi ya wiki) sasa haijatangaza kitu!