joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
- Thread starter
- #101
Tofauti ni kwamba, Tanzania ardhi yote ipo Chini ya Serikali, hata kama inamilikiwa na mtu binafsi lakini sheria na taratibu za matumizi yake zinaratibiwa na kudhibitiwa na Serikali, kwa mfano japokua ardhi ni yako lakini lazima uitumie, usipoitumia kwa zaidi ya miaka 3 sheria inaruhusu Serikali kuichukua na kumpa mtu mwengine bila kulipwa chochote, pia ukitaka kuiuza lazima ufuate sheria za nchi, kwamba huwezi kumuuzia mtu ambaye sio raia wa Tanzania.Sasa kama ni hivyo basi hakuna tofauti kati ya TZ na KE. Hata huku Kenya, serikali ikitaka shamba inaichukua na kukulipa fidia kama ilivyofanya wakati wa ujenzi wa SGR.
Sent using Jamii Forums mobile app