Corona: Watakaopona walijipanga, Ukiona vyaelea Vimeundwa

Corona: Watakaopona walijipanga, Ukiona vyaelea Vimeundwa

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
34,775
Reaction score
46,063
Mabibi na mabwana moja kwa moja kwenye mada.

"Mficha ugonjwa kifo humfichua." Haya si maneno yangu, bali ya wahenga walioyaona hayo tangia zama za kale mno.

Hadi wa leo majina ya vigogo, makubwa na madogo, ndani na nje ya nchi yanajulikana kuwahi kuathirika vilivyo na ugonjwa huu wa Corona. Vipo vifo vingi tu ndani na nje ya nchi na hata vingine vilivyo kanushwa. Macho makavu kweli kweli kuwa, "huyu siyo Corona!" Lakini sasa nani asiyejua kuwa akili ya kuambiwa tena usipochanganya na ya kwako, labda kama unasubiria teuzi?

Mwangalie basi usoni huyo anayekanusha na kisha umtathmini angalau kidogo tu. Ndiyo ubinadamu huo.

Alisema hayati baba wa taifa (rip), "mtu anasema anachukia rushwa, lakini ukimwangalia usoni unajiuliza. Huyu?! Kweli anachukia rushwa huyu?" Mwisho wa kumnukuu.

Vinavyoelea, ama kwa hakika vimeundwa! Wala, dobi asilaumiwe, kaniki ni rangi yake! Ukipanda bangi utavuna bangi. Kama ambavyo ukipanda maharage utavuna maharage!

Tusitegemee mafanikio pasipo kuwa na jitihada za makusudi kuyasaka mafanikio hayo. Ni busara ya kawaida tu pale wenzetu wanapofanikiwa tunapokuwa tayari kujifunza kutoka kwao. Badala tu ya kujikita kumchochea vilivyo pepo wa husda dhidi yao!

New Zealand moja ya nchi beberu kama wafilisika mawazo sisi tunavyopenda kuziita, wamefanikiwa vilivyo kuushinda ugonjwa huu.

Je, tunacho chochote cha kujifunza kutoka kwao? Au ni yale yale ya kibongo bongo kuwa kila kitu tunajua hata kama ni wazi kuwa hatujui?

Corona: New Zealand siku ya 17 leo bila ya kirusi Corona nchini

Rwanda majirani zetu. Wanasemekana kuwa kwao pia wako vizuri zaidi kuliko nchi yoyote barani Afrika katika vita hivi.

Wao walianza mapema tu jitihada za kujizatiti kabla ya hatari. Hii ikiwa mapema sana hata kabla ya ugonjwa huu kuingia nchini mwao. Na wameendelea na msimamo huo huo wa kutoukimbia ukweli wala kuutafutia ukweli majina mengine:

Rwandan President Kagame hints at firing more ministers

Aliyekuwa waziri wa afya wa huko mapema miezi ya Feb alipoleta ongo longo kidogo tu, kuhusiana na huu ugonjwa hakuvumiliwa. Pale pale aliipokea stahiki yake sawa sawa na matendo yake.

Hali ni hiyo hiyo hadi leo na wanakoelekea sasa ni katika kurejea salama katika shughuli zao za kawaida salama na katika umoja wao.

Hawa nao je, tunacho chochote cha kujifunza kutoka kwao? Au yale yale ya hadithi tulizozizowea za manyani?

Poleni ndugu zetu wa Burundi. Kuvunjika kwa koleo si mwisho wa uhunzi.

Wahenga wanasema "Kawia ufike."

Tu pamoja nanyi ndugu zetu katika kumwombea Madame Nkurunziza. Mola amfanyie wepesi apate kurejea Bujumbura salama.

Ukapumzike kwa amani hayati Pierre Nkurunziza. Wewe umetangulia sisi tuko nyuma yako.
 
Unapata tabu na threads zako zilezile we endelea tu kupiga ramli,kuna wale unao waabudu wameanza na lockdown mwishoni waka maliza na maandano hamna cha barakoa,sanitizer wala social diatance hawa huwazungumzii.
 
Paragraph ya mwisho umekosea ni (shetani pekee ndiye awezaye kuwa nyuma yake).
 
Ukapumzike kwa amani hayati Pierre Nkurunziza. Wewe umetangulia sisi tuko nyuma yako. Paragraph ya mwisho umekosea ni (shetani pekee ndiye awezaye kuwa nyuma yake)

Kazi kweli kweli.
 
umenipa sifa za Fieldmarshal
Paragraph ya mwisho umekosea ni (shetani pekee ndiye awezaye kuwa nyuma yake)

Wewe mwalimu wa shule ya UPE, ipi mkuu? Shule zimefungwa muda mrefu eeh, kazi za kusahihisha sahihisha ulizokuwa umezizoea hazipo tena na sasa unawashwa washwa?

Bandiko hili sikukuletea wewe kwa ajili ya masahihisho. Utaweza kulisahihisha wewe hilo? Acha mkuu. Bandiko limeshiba hilo siyo saizi yako hilo.

Jikite kwenye mada mkuu, mengine hayo huyawezi. Ila tu kama ndiyo ulikuwa na mpango tu wa kututaarifu kuwa ulikuwa Dodoma hivi karibuni, basi sawa tumekusikia.

Vipi mkuu majacket mliyovaa jana lako lilikuwa la rangi gani?[/QUOTE]
 
umenipa sifa za Fieldmarshal

Wewe mwalimu wa shule ya UPE, ipi mkuu? Shule zimefungwa muda mrefu eeh, kazi za kusahihisha sahihisha ulizokuwa umezizoea hazipo tena na sasa unawashwa washwa?....

Mkuu nimekusoma ila kiungwana mtu akishatangulia mbele za haki, si uungwana tena kuongelea mabaya yoyote ya marehemu bali mazuri yake.

Mengine huachiwa yeye na Mungu wake. Sisi nani kuyajua hayo kwa ukamilifu?

Ilikuwa ni katika kuzingatia uungwana tu mkuu.
 
Unapata tabu na threads zako zilezile we endelea tu kupiga ramli,kuna wale unao waabudu wameanza na lockdown mwishoni waka maliza na maandano hamna cha barakoa,sanitizer wala social diatance hawa huwazungumzii.
Kaajiriwa na mabeberu huyu
 
Kaajiriwa na mabeberu huyu

Twamlilia ndugu yetu Nkurunziza tu mkuu. Asingeyapuuza ya kuachia mikusanyiko ambayo haikuwa ya lazima nani ajuaye?

Tulipo sasa. Majuto ni mjukuu. Waungwana hujifunza kote. Kwa maana msumeno hukata kwa mbele na kwa nyuma pia.
 
Habari kuwa mama yake Nkurunziza naye amefariki dunia na kuwa hata mkewe na pia dada yake ni wagonjwa kitandani kuwa bado ingekuwa heri kama tungegutuka.

Kama bado haitugutui si bure kama ilivyo kuwa kwa Farao mioyo yetu itakuwa imefanywa kuwa migumu ambapo anguko letu linaweza kuwa baya zaidi.
 
Wao wanarejea leo na shughuli za kawaida? sie kitambo tunaendelea na shughuli zakawaida na hatujpata vifo kama walokaa karantini. Saivi uko New york waanza kurudi na shughuli zao wakati bado wana kesi kibao za korona. Lakini wakifanya wao ni swa, ikifanywa TZ inakuwa nongwa!
 
Mkuu New York wana cases ngapi? Na sisi tuna sase ngapi kukufanya udhani sisi cases ni chache zaidi?

Burundi nao walikuwa na taarifa kama hizo hizo sana hata wakajiridhisha kuwa ilikuwa salama na muafaka kufanya uchaguzi mkuu. Matokeo yake:

1. Rais sasa ni marehemu.
2. Mama wa Rais naye ni marehemu
3. Mke wa Rais hoi hospitali
4. Dada wa Rais hoi hospitali

Anayekwambia kuwa cases kwetu hazipo wakati hapimi nawe unamkubalia? Kesho atakwambia yeye Messiah na bado utamkubalia.
 
New york hadi sasa wakati naandika wameripoti kesi 355,808 ambazo ni active cases, na hakuna aliepona hadi sasa, na wameripoti vifo 24,348.

Sasa wao wamepanga kufungua jiji shughuli ziendelee, sasa kwanini iwe nongwa kwako Tanzania shughuli zikiendelea?

Cases zingekuwa nyingi kwetu na jinsi tunavyosongamana kwenye mihangaiko, basi kifo kingetuumbua. Nipo Zanzibar, kisiwa kidogo, mtu akifa Nungwi na kama upo mjini unajua, mbona hatuoni vifo vya jumla kama vilivyotokea kwa wenzetu? Na hasa Zanzibar tunapeana mikono, watu wanakaa maskani kama kawaida, mirando isio ya lazima kibao.

Kwani kila anaekufa sasa anakufa kwa Corona? Mmerogwa kweli kweli!
 
Muonege aibu basi.korona imewaaibisha bado mnaombea watu njaa tuu
 
Mkuu hizi takwimu zako unazipata wapi? Haipo format ya namna hiyo labda kama hii uliyoweka hapa inapatikana Lumumba kwa mahitaji ya propaganda mufilisi.

Takwimu za mataifa yote ziko hapa mkuu:

Coronavirus Update (Live): 7,389,280 Cases and 415,818 Deaths from COVID-19 Virus Pandemic - Worldometer

Tambua kuwa ndani ya saa 24 zilizopita katika marekani yote kulikuwa na maambukizi mapya 8,189 na vifo 266. Hiyo ni marekani yenye states 52.

Katika kipindi kama hicho weka takwimu za Tanzania hapa ili tulinganishe. Huwezi kulinganisha kuku 13 na bata 13 kibongo bongo ili kusema nani ni zaidi.

Leta takwimu hizo ili kujiridhisha ni nani baina yetu aliyerogwa.
 
j5.PNG

Vipi hizo zinatoka Lumumba? Halafu hio format haipo sio? Mnashikiwa akili tatizo na kuburuzwa.

Sasa mimi argument yangu nasema kuwa, Jiji la New york lishaanza mkakati wa kufungua shughuli ziendelee, tena vipi Tanzania iwe nongwa tukiendelea na shughuli?

Halafu lete wewe takwimu za Tanzania ambazo unasema kuwa tunaficha.
 
Muonege aibu basi.korona imewaaibisha bado mnaombea watu njaa tuu

Hakuna wa kukuombea njaa. Huko ni kudai kutishwa na kinyago unachokichonga mwenyewe.

Pana nchi 3 hapa. 2 ni success story. 1 imepoteza rais na mama ndani ya siku 2. Hawajazikwa bado Hali katika kipindi hicho hicho mke na dada wa Rais wako hoi hospitali.

Hatuwezi kuona kuwa tunaweza kujifunza kitu popote ila visingizio vya kijinga jinga?
 
View attachment 1474484

Vipi hizo zinatoka Lumumba? Halafu hio format haipo sio? Mnashikiwa akili tatizo na kuburuzwa.

Sasa mimi argument yangu nasema kuwa, Jiji la New york lishaanza mkakati wa kufungua shughuli ziendelee, tena vipi Tanzania iwe nongwa tukiendelea na shughuli?

Halafu lete wewe takwimu za Tanzania ambazo unasema kuwa tunaficha.

Takwimu hizo bila maelezo yoyote kuainisha kilichopo hapo ni upuuzi:

1. Namba zipi ni nini?
2. Namba hizo ni za muda gani?
3. Watu wangapi walipimwa?

Hivyo hivyo bila kuwa na za Tanzania kwenye scale hiyo hiyo ni upuuzi mwingine wa kiwango cha PhD.

Hapo ndipo u Lumumba unapokuja.
 
Jamaa bado anaendelea na issue za kutiwa watu hofu za corona wakati huko marekani kwenyewe watu wanaandama bila barakoa na wala hawana hofu na wao ndio wamekufa kama kuku huko,hofu haina nafasi tena maisha yanaendelea.
 
Back
Top Bottom