Corona yapunguza wasafiri mabasi ya mikoani Ubungo

Joined
Apr 4, 2020
Posts
16
Reaction score
7
1586526161449.png

KATIKA kipindi hiki cha kuelekea Sikukuu ya Pasaka, idadi ya abiria katika Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam, imepungua tofauti na miaka mingine inavyokuwa. Kipindi cha Pasaka katika miaka mingine kuanzia Alhamisi Kuu na kuendelea kunakuwepo na abiria wengi wanaokwenda mikoani kutokea jijini Dar es Salaam hali inayosababisha wenye magari madogo kuomba ruhusa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA).

Karani wa basi la Capricon lenye namba za usajili T 146 DCL, Emily Swai alisema mwaka huu kipindi kama hiki cha kuelekea Sikukuu ya Pasaka hali ni tofauti kutokana na mlipuko wa maambukizi ya virusi vya corona. Swai alisema kufungwa kwa shule za msingi, sekondari na vyuo mapema kumesababisha wanafunzi kukaa nyumbani badala ya kwenda kula sikukuu mikoani, hivo hali ya uchumi imekuwa ngumu.

Alisema basi hili lilikuwa lianze safari yake majira ya saa tatu asubuhi jana lakini litalazimika kuondoka saa tano kutokana na uchache huo wa abiria. Naye wakala wa basi hilo la Capricon, Salim Athuman alisema kipindi hiki hali ya usafiri sio nzuri kwa sababu watu hawana fedha kwani shughuli nyingi zimesimama. “Msimu kama huu wa sikukuu tiketi huuzwa kati ya shilingi 30,000 hadi 32,000 na zinakwisha, lakini kipindi hiki zinauzwa kati ya shilingi 20,000 hadi 25,000 lakini hamna abiria,” alisema na kuongeza kuwa hivi sasa kituoni hapo kungepaswa kuwa na Coaster zinazopakia lakini hakuna,” alieleza Athuman.

Wakala mwingine wa basi la Dar Express lenye usajili wa namba T 360 DCN, Steven Towo alisema maambukizi hayo ya corona yamewapa mtihani wasafirishaji kwa kuwa hakuna biashara. Alisema msimu kama huu miaka ya nyuma walikuwa wakiondoa gari tano lakini sasa wanaondoa gari mbili tu tena kwa kusuasua.

Akizungumzia hali hiyo, Meneja wa Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo, Maira Chirosa alisema alichokibaini kipindi hiki tofauti na miaka mingine ni kwamba wananchi wamepunguza safari zisizo za lazima kama viongozi wa nchi wanavyosisitiza ili kujiepusha na maambukizi ya corona. Kwa upande wake, Katibu wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa), Enea Mrutu amekiri kipindi hiki hali ni mbaya kwani biashara hiyo imeshuka kwa asilimia 80
 
View attachment 1415276

89ac0662-e947-4f50-a67b-d1c81ab1eb3b.jpg

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
.... Labda Ubungo..... Binafsi leo nimekaa Mbezi Stand kuanzia saa 1 mpk saa 2½.... Asubuhi hakukuwa na BASI LA MAANA lililoingia Mbezi kuchukua abiria wa Morogoro2! Abood na BM zilipita juu kwa juu!

Mabasi machache yaloingia Mbezi muda huo yalitangaza kubeba abiria wao wenye tickets tu... kwenda DOM, IR na MBY!

Abiria wa Morogoro, Mbezi leo hapakuwa stand rafiki! Pia leo kulikuwa na zile COASTER PRIVATE zinaitilia MOSHI, zilikuwa zinajaa km bure!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Emirates wamesimamisha madege Yao itakuwa hizo Kimbinyiko hapo Ubungo?
 
Back
Top Bottom