JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa(WHO) linaeleza hatari hiyo inachochewa na upungufu wa vifaa vya kujilinda kwasababu baadhi ya Wahudumu katika Sekta ya Afya hupata maambukizi ya #COVID19 wakiwa katika maeneo yao ya kazi
Aidha, wapo waliothibitika kupata maambukizi ya #COVID19 wakiwa nje ya vituo vyao vya kazi
Ushahidi uliokusanywa na WHO kutoka katika Mataifa mbalimbali umetaja sababu zifuatazo kuwa chanzo cha maambukizi kwa Watumishi wa Sekta ya Afya
1) Kuchelewa kutambulika kwa dalili za ugonjwa wa #COVID19 pamoja na kukosekana kwa uzoefu wa magonjwa yanayosababishwa na Virusi vinavyoathiri mfumo wa upumuaji
2) Kuwepo kwa idadi kubwa ya Wagonjwa na kuwafanya Wahudumu kukosa muda wa kutosha wa kupumzika
3) Kutokana na uhaba wa vifaa vya kujilinda
4) Kukosekana kwa njia madhubuti za kuzuia kuenea kwa maambukizi katika maeneo ya Hospitali
Tuendelee kujilinda dhidi ya maambukizi ya #COVID19 na tuwape ushirikiano mkubwa Wahudumu wa Afya
Upvote
0