Bishop Hiluka
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 7,147
- 14,699
Wauguzi wanaofanya kazi katika wodi iliyotengwa kwa watu walioambukizwa virusi vya corona nchini Kenya wameanza mgomo baridi kulalamikia kile wanachodai kuwa ukosefu wa vifaa vya kujikinga na mafunzo ya kutosha.
Hospitali ya Mbagathi katika mji mkuu wa Nairobi, ni moja ya hospitali zilizo na wodi ya kutibu wagonjwa waliombukizwa virusi hivyo hatari.
Katibu mkuu wa muungano wa wauguzi nchini Kenya, Seth Panyako ameiambia BBC kwamba wauguzi watarejea kazini ikiwa watapewa mavazi maalum na mafunzo ya jinsi ya kuwashughulikia wagonjwa.
"Wahudumu wa afya wako katika hatari ya kupata maambukizi katika mazingira yao ya kazi," alisema Bw. Panyako.
"Bila ya kuwa na vifaa maalum,wanatarajiwa kujilinda vipiwakiwa kazini na wanaporejea nyumbani kutangamana na familia zao?"
Hospitali ya ya Mbagathi inawazuilia watu 22 ambao walitangamana na mgonjwa wa kwanza aliyeambukizwa virusi vya corona.
Watu wengine wawili walioambukizwa virusi hivyo wamepelekwa katika hospitali ya ya kitaifa wa Kenyatta - ambako mgonjwa wa kwanza aliyethibitishwa kuambukizwa anapewa matibabu.
Chanzo: BBC Swahili