Kingereza hukijuwi vizuri halafu unataka kulazimisha tu.
Kitu nilichogundua kwenye hizi nyuzi za Wakenya na Watanzania ni kuwa Wakenya wengi wako vizuri katika lugha zote mbili kwa kuandika, Kingereza na Kiswahili, kuliko Watanzania wengi.
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
Tatizo la Kenya kwenye hii miradi mikubwa ni wapigaji sana.
Tanzania pia tatizo hilo tunalo lakini katika hii miaka mitatu Magufuli anajitahidi sana kuwabana. Mungu asaidie afanikiwe, maana dah.
Watanzania wezi si mchezo, wameiba mashirika yote ya umma.
Halafu wengi walioiba mipesa mingimingi ni wajinga, wanaiba halafu wanaipeleka kuificha Ulaya. Au wanaiba halafu wanawapa wahindi na waarabu wafanya biashara wawazalishie.
Wengi wao wanaiba halafu wanalewea tu. Michango mikubwa kwenye harusi na vifo.
Kuna siku nilihudhuria maziko ya ndugu wa rafiki yangu mmoja yalifanyika Sinza. Basi hiyo catering service, vinywaji kila aina ya vya kilevi vilivyokuwepo siku zote za maziko (zaidi ya wiki) nilishangaa sana.
Nikamwambia yule rafiki yangu, inaonesha kwenu ni matajiri sana lakini wewe hujioneshi. Akanambia ahh wapi, mambo yote haya yanafanywa na mjomba anafanya kazi bandarini. Nikashangaa sana, vipi mfanyakazi wa badarini anamudu pesa zote zile? Estimation yangu ya ghafla ilikuwa si chini ya
million 20 kwa siku zilizotumika kwenye mazishi tu.