Cost comparison SGR Kenya vs SGR Tanzania


Hiyo ni kweli kabisa kama hakuna shida kwenye time table ya train ata hiyo nusu saa ni nyingi. Kama utaratibu wa ticket nao ukiwa mzuri kama wa card za mwezi au mwaka basi unaitaji dakika 5 tu mambo mswano.
 
It's been close to 3 years since SGR Kenya became operational and is finally profitable against all the odds. Majirani ni 'mwakani' tu [emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Exactly. Japo wasiwasi wangu utashi mdogo kwenye halimashauri zetu. Mipango mingi huwa initiated na serikali kuu, halmashauri zimelala kabisa.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijazusha mkuu. Kuna siku Kadogosa alidokeza hii kitu alipokuwa akizungumzia future plans ambazo zimelenga population prospects za 2035. Alikuwa akizungumzia pheasibility study ya commuter trains km 266 iliyofanywa kwa ushirikiano na kampuni moja ya SA.

Sina utaalamu sana ila nafahamu hivyo. Kwa maelezo yake route ya commuter trains itaanzia Pugu (zinapoishia passenger train za upcountry) ila main commuter station itakuwa hii DSM station ya SGR.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leta evidence! treni za abiria zitaenda central station miaka 100 ijayo as long as viaduct itakuwapo soma ESIA report!

Ripoti hiyo 👉
 
Project delays ziko hata nchi zilizoendelea. Kikubwa hakuna sababu za kipuuzi zilizopelekea delay. Kwa hali (ya mvua) ilivyokua kwenye maeneo ya madaraja na culverts nyingi ambayo ni very swampy hasa Ruvu, ilikuwa nafuu kuchelewa kuliko kurush na kujenga madaraja ya biskuti.
It's been close to 3 years since SGR Kenya became operational and is finally profitable against all the odds. Majirani ni 'mwakani' tu [emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
See a reason why according to IFC an associated facility as Transmission Line for 220kV line btn Dar and Moro does not count in the cost of SGR!

CC: Bantugbro n Simon
 

Attachments

See a reason why according to IFC an associated facility as Transmission Line for 220kV line btn Dar and Moro does not count in the cost of SGR!

CC: Bantugbro n Simon
I don't know what you wanted me to see there but , that document you have given is a summary of the ESIA full report which I have been using...

To cut this argument short, Uganda's electric SGR includes the cost of the TL plus locomotives. Now, when you are comparing the costs of building the UG vs Tz rail, do you think it would be fair to exclude adding the costs of associated facilities for the TZ line???
 
Hapo uko na point, ingawaje unajua sio kila mtu atafika dakika 5 kabla treni inondoke, mimi nimeshuhudia watu wengi sana wakiachwa na treni na walifika dakika kumi kabla treni iondoke, Si unajua vile tuna dili na alshabaab huku? Utapitia security check points kama nne hivi kabla uingie ndani ya stesheni, ya kwanza unaangaliwa kitambulisho au pasport kama wewe uko kenya kihalisi, ya pili unapanga mizigo kwa sakafu alafu umbwa ana nusa nusa, alafu baada ya hapo unaenda kwa ofisi ya tiketi, unatumia 'code' ulio tumiwa kwa simu wakati uli book safari kwa mpesa ussd au mtandaoni, hio code ndo unatumia ku chapisha ticketi yako kutoka kwa automated ticketing machine, alafu ndo sasa unaeenda kwa security checkpoint nyengine ambapo mizigo itafanywa x-ray scan alafu we mwenyewe utafanyiwa search juu hadi chini... pia utaambiwa utoe kitambulisho pamoja na ticketi walinganishe kama jina kwa kitambulisho na kwa tiketi linafana kwasababu hauruhusiwi kutumia ticheti ya mtu mwengine....baada ya hapo ndo unaingia mahali pa kukaa........kabla kuingia kwa treni yenyewe bado tena utaitishwa uonyeshe tena ticketi yako.... Kumbuka kama mko wengi, hio line ya security pekee itakuchukua kama 20-30 minutes! Alafu unaelewa vile waafrica tunapenda kuchelewa kwahivyo nyote mtapatana hapo kwa gate dakika ya mwisho .... Kwahivyo ili usichelewe, panga kufika kwa stesheni angalau lisaa limoja kabla.



Anyway, stesheni yoyote ya abiria iwe in airport,train station, bus station, capacity yake hua inapigiwa hesabu kulingana na maximum throughput.... Yani hauangalii best case scenario, unaangalia worst case... Ni abiria wangapi wanaeza pitia hapo na wafanyiwe kila kitu kwa dakika au lisaa limoja au kwa siku nzima.... Kutoka hapo sasa ndo anaeza ukapiga hesabu za abiria wa ngapi kwa mwaka... Kwa mfano kwa stesheni ndogo za Kenya ile ndogo kabisa zinaweza kuhudumia abiria 300 kwa siku. na zile kubwa kubwa kidogo kama Voi na mariakani maximum kwa siku ni abiria 600.... Hio ndo nambari ya wateja wanaotarajiwa mwaka wa 2035...

hio maximum capacity hawakuiokota tu, walichukua data ya kutoka kwa reli ilojengwa na mkoloni na uhusiano wake na ukuaji wa miji kama Voi, Nakuru Eldoret iliopanuka kwasababu ya reli, alafu waliangalia intergrated economic plans za kila county ambapo SGR itapita, tena wakapiga hesabu za economic potential za hizo county.. Kwa mfano ukosoma hizo feasibility studies na ESIA reports utapatahesabu za mambo mengi sana...

Kwa mfano hii hapa inaangalia economic returs za route tofauti ambazo SGR ingepitia

 
Kuchambuliwa kwa SGR ya Kenya na kina David Ndii na wenziwe ni kwasababu media ya Kenya ina Ujasiri na kuna uhuru wa wanahabari..... Hebu nionyeshe uchambuzi wowote ambao ushawahi fanywa na mwanahabari yeyote wa Tanzania, Nionyeshe Uchambuzi wowote wa reli ya Ethiopia ?????

Hapa eastern Africa, ni reli ya Kenya pekee tu ndo inajulikana inje ndani kwa technical details, economic analysis, etc... Hizo reli zengine kama ya TZ hakuna lolote linalo julikana nje ya Initial cost... Na hakuna mwanahabari yeyote jasiri ashawahi kutubutu kuuliza maswali kwa serekali... Yote tunayoyajua kuhusu SGR ya TZ ni kutokwa kwa mdomo wa CCM!!!!
 
Investors setting shops at the Naivasha Special Economic Zone will be charged 5cents per KW of power; this according to the KAM Chairman Sachen Gudka. The park will host a public utility area to help process cargo transported from Mombasa Port through SGR.


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…