Kwhyo new model electric inakimbia kw speed ya 160[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Sent using
Jamii Forums mobile app
Umeona ulivyo na tatizo, unachofikiri reli kuwa ya umeme ni speed tu, ngoja nikupe somo kidogo:
Ukitumia Reli ya umeme (Stima) inapelekea kupunguza matumizi ya Diseli ambayo unaagiza kutoka nje ya nchi kwa fedha za kigeni na badala yake unatumia umeme unaozalishwa ndani kwa vyanzo vyenu na hivyo kupelekea kuongeza mzunguko wa fedha ndani ya nchi na sio kutoa hizo peza kwenda nchi za nje kwa ajili ya diseli.
reli ya umeme (stima) inalinda mazingira, kutumia reli ya diseli inapelekea kuzalisha greenhouse gases ambazo zinaenda either kusababisha ozone layer depletion au kusababisha ongezeko la joto duniani ndo maana ujenzi wa reli ya diseli haitakiwi kwenye karne ambayo dunia inapambana na mabadiliko ya tabia ya nchi na kupelekea nchi zilizoendelea kuanza kutumia teknolojia zinazotumia umeme (stima) kama magari na mitambo mengine na sio mafuta. Hivyo dunia inaenda mbele nyie wakenya mnairudisha nyuma mwisho wa siku mtabaki peke yenu nyuma.
Mafuta yanakwisha, hivyo kama mumejenga reli ya diseli na siku mafuta yakafiga omega ina maana nyinyi mtasimama wapi maana hilo deni la mchina itachukua miaka mingi kulimaliza. Ila mngetumia umeme (stima) basi mambo yangekuwa poa maana maji lazima yawepo or upepo au chochote kile maana umeme (stima) una vyanzo vingi tofauti na hiyo diseli yenu.
Reli ya umeme (stima) ina mvuto wa kipekee ambao unaleta faida kwa watalii, pia inapendezesha mji au nchi na kuipandisha hadhi na sio diseli ambayo mlioweka nyinyi.
Gharama za uendeshaji wa Reli ya Diseli ni kubwa maana bei tu ya ayo mafuta haupangi wewe bali wanapanga wengine hivyo siku diseli ikipanda basi mnaanza kuangaika na kuwaumiza wananchi kwa kupandisha bei ili msipate hasara wakati reli ya umeme (stima) ni nyinyi nchi kama nchi ndo mnafanya maamuzi.
Reli ya umeme (stima) iko more automated kuliko ya diseli, kuna systems nyingi sana za safety (usalama) ambazo zinafanya kazi kwenye reli za umeme (stima) tu kama vile kuzima treni kutokea headquarters endapo ikionekana inahatarisha usalama wa abiria kama vile mwendokasi mkubwa. Mtu wa headquarter anabonyeza kitufe uku mzigo unazima.
Sent from my iPhone using JamiiForums