Wanabodi (kwa sauti ya paskali),
Leo tarehe 4 nimefanya uzinduzi wa kupanda treni yetu pendwa ya SGR. Kwa bahati mbaya leo asubuhi kulikua na shida kwenye gridi ya taifa hivyo kujikuta treni karibu zote kuchelewa kwa angalau saa moja, na vyombo vyote vya habari vilitangaza.
Baadae umeme ulirudi na safari kuendelea kama kawaida,ila around mida ya saa 11 jioni safari zikasimama tena kwa zaidi ya masaa manne mpaka muda huu ninapoandika (na tukaendelea kusubiri huenda ikazidi masaa manne).
Tofauti na asubuhi ambapo uma ulitangaziwa kuwa tatizo ilikua umeme kwenye gridi ya taifa,hii ya sasahivi hatujaambiwa ni nini hasa tatizo zaidi ya kuambiwa mafundi wanaendelea kushughulikia tatizo la kiufundi/kimfumo.
Na hata hivyo hakuna chombo chochote cha habari kilichotangaza hadi sasa.
Cha kusikitisha ni kuwa hizi SGR hazina huduma ya chakula kama zile treni za zamani,hivyo kila mtu analia njaa hapa (japo mi silii njaa maana najua njaa ya siku moja haiui), ila shida ni kwa watoto ambao zaidi ya zile bites, korosho na chai hakuna kingine kinachouzwa humu.
Najiuliza hivi zile tumbuatumbua zingekuwepo haya mambo yangekua yanajirudia kiasi hiki? Mbona kama hawa jamaa wanakazi kubwa ya kufanya ila wamerelax sana?
Na hapo ni mvua ya siku moja tu kwa mikoa ya morogoro na Dodoma, je masika ikikolea kutakua na safari za uhakika kweli?
Nadhani watu wakianza kuwajibishwa akili zitarudi aisee uzembe pia unachangia kwenye hili na tutaishia kulaumu kuhujumiwa na wenye mabasi.
Wanabodi (kwa sauti ya paskali), Leo tarehe 4 nimefanya uzinduzi wa kupanda treni yetu pendwa ya SGR. Kwa bahati mbaya leo asubuhi kulikua na shida kwenye gridi ya taifa hivyo kujikuta treni karibu zote kuchelewa kwa angalau saa moja, na vyombo vyote vya habari vilitangaza. Baadae umeme...
www.jamiiforums.com