Sifa moja ya matajiri feki huwa ni matanuzi ambayo lengo ni kujionyesha kuwa wana hela. Wanajulikana zaidi kwa matanuzi yao zaidi ya biashara zao. Na wakikuonyesha hizo biashara wanazodai ndizo zinazowaingia fedha utakuta ni biashara ambazo sio za uzalishaji bali ni investments, mara nyingi huwa ni real estate, you know? The type of businesses which one starts AFTER MAKING MONEY (or stealing money). Unakuta bwana mdogo anatanua kwenye instagram ukimuuliza anadai ni mfanyabiashara, biashara gani? anakuonyesha zinga la shopping mall au apartment buildings. Ukimuuliza zaidi ya hapo mtagombana tu. Huwa hawanaga CV inayoonyesha wameanzia wapi huwa wanaibukia tu straight to the top.
1. Michael ezra: Huyu bwana hajulikani hata alikuwa anafanya biashara gani, aliibuka tu from nowhere akaanza kuandikwa kwenye vyombo vya habari eti anataka kununua Leeds United ya uingereza kwa zaidi ya $100 milioni, mara anaandikwa anataka kununua PRIVATE Airbus, na makeke mengine kama hayo. Alikuwa anatanua tu kwa kununua Lamborghini, kufadhili timu za mpira za Uganda n.k lakini kwa fedha ambazo huku kwetu hata kina papaa msofe na King 'msukuma' wanazo.
Baadae mashtaka ndio yakaanza kumuandama, mali zake uganda zikapigwa mnada kwa kutolipa kodi ndogo tu ya $500,00, Kenya nako alishtakiwa kwa kudaiwa hela za kitoto kweli. Mtu anayejitamba kuwa na mali za $1.5bilion Dubai anakamatwaje kwa kudaiwa $200,000? Iligundulika kwenye makesi yake kuwa jamaa alikuwa anakopa kwa kutumia image yake feki kuwa ni successful business man halafu ile hela ndio analia bata! Mind you mpaka sasa hivi NOBODY KNOWS biashara hata moja huyu bwana anayofanya!
2. Meddy sentongo: Huyu naye aliibuka tu akaanza kutumia hela kama kichaa, akaanza kuandikwa na vyombo vya habari, mara aende marekani kununua escalade, mara alipe wanamuziki hela wamtungie track, na mbwembwe zingine. Biashara anayofanya HAIJULIKANI! Kumbe jamaa ana demu wake anaitwa 'bad black', yeye na huyu bad black walimtapeli mzungu millions of dollars (sikumbuki exactly but around $10million) wakaanza matanuzi. Imagine jamaa anamtoa demu wake kafara kwa mzungu ili wapate fedha! Demu asivyo na aibu alivyokuwa anajitetea mahakamani alidai yeye hajatapeli, ila ni kwamba eti mzungu alimpa mabilioni yoote hayo kwa sababu alikuwa anampa 'tigo'! You can't make this up soma mwenyewe:
I was paid billions for sex - Bad Black
3. Ivan semmwaga + zari : huyu zari ni yule 'mke' wa diamond, huyu ivan alikuwa mumewe. Ivan anakaa SA. ivan na zari walikuwa wanapiga misele na chopper huko kampala, wanafadhili timu za mpira za uganda, kila goli wanalipwa timu nzima! Pati kubwa kubwa, wanamiliki hotels na properties nyingi. Ukimuuliza ivan anafanya biashara gani huko SA unajua atakuambia nini? eti ni MGANGA WA KIENYEJI a.k.a Sangoma! I kid you not that is his alleged profession. Lakini ukishaona lifestyle yake ya lamborghinis na choppers unajiuliza huyu sangoma wateja wake ni kina zuma au?
4. Huyu bwana mdogo mwenye hilo crib wenzake wanadai walikuwa naye majuzi tu kwenye biashara ndogo ndogo za kwenda china kuleta mizigo na kuja kuuza uganda, wanashangaa mwenzao kawaje tajiri fasta namna hii. Baadae kaja kuwa linked na wizi wa $1.4m za benki ya equity, read here:
Inside Hamâs Multi Billion House, Speaks Out on Equity bank Heist | Red Pepper Uganda. Anajitamba kuwa ana net worth ya $200m hivyo hawezi kuwa ameiba $1.4mil. Lakini watu wazima tunajua hakuna tajiri wa kweli ambaye yuko comfortable revealing his net worth. Hiyo ni sifa ya matajiri feki. Ila dogo kwa vile kapiga shule dili zake anafanya kikubwa kama jamaa zetu wa fedha za mboga huku kwetu. Watendaji serikalini huwa wanastopisha madili yake ya kimagumashi e.g kujenga bila permit, jamaa akiona watendaji wanamzingua yeye anatinga straight kwa Museveni, museveni nalo linatoa oda, dili inapigwa.
Nakivubo board plead with Museveni over Nakivubo