DEEP STATE, COVID-19: Nini Maana ya Uhandisi Jaamii Unaotokea Duniani?
#7
Ni nani yule pembemi ya James Clapper (aliyesimama nyuma ya Robert Gates).
Kwa nini Ikulu ya Marekani wamekataa kumtaja jina mpala leo hii.
Kama umewahi kusoma simulizi yangu ya Vipepeo Weusi mara kadhaa juu kabisa mwanzoni huwa naandika kwamba simulizi ile iko 'inspired by true events'. Simulizi ile ya Vipepeo Weusi ni Riwaya ambayo nimeitengeneza lakini ndani yake kuna matukio ambayo ni ya kweli yaliyo amsha hari ndani yangu na hatimaye kuandika simulizi ya namna ile.
Kwa hiyo next time ukiona nimeiweka simulizi ya Vipepeo Weusi hakikisha unaisoma maana kuna mambo mengi sana adhimu kuhusu nchi yetu ambayo namna pekee naweza kuyaandika ni kwa kuyaweka kwenye simulizi ya namna ile.
Mojawapo ya matukio haya ya kweli… kuna mahala kwenye 'Season One' ya ile Riwaya niliandika kwamba Ray kupitia Taasisi yake ya SOTE HUB alisaidia vijana kadhaa kupata ufadhili wa kuanzisha kampuni. Mojawapo ya vijana hao walioanzisha kampuni kulikuwa na kijana wa Kimasai ambaye alianzisha kampuni ya Ulinzi.
Katika maisha ya halisi ni kwamba… kipindi nasoma Chuo Kikuu Mzumbe, tulifanikiwa 'kunusa' dili fulani hivi. Kuna kampuni toka Australia waliingia pale Morogoro kufanya shughuli fulani maeneo ya Ifakara na Kilosa. Nilikuwa na rafiki yangu anaitwa George tukafanikiwa kuwashawishi wageni hao watupe jukumu la Ulinzi.
Hatukuwa na kampuni, tulikuwa wanafunzi tu.. usiulize tulifanikiwaje kuwashawishi, hakuna linaloshindikana chini ya jua ukiwa na 'motivation'.
Kwa hiyo tukaanza kuhaha kusajili kampuni ya Ulinzi. Kimbembe kikaja urasimu wa namna ya kupata vibali kwa ajili ya silaha za moto (kwa ajili ya vijana watakaokuwa wanalinda).
Kuna vitu vingi sana tulikuwa hatujivui kabla na mchakato ulikuwa ni mgumu kuzidi vile ambavyo tulidhani.
Ndipo kwa mara ya kwanza nikafahamihana na Mstahiki Naibu Meya Isihaka Sengo. Naam huyu Sengo Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro aliyefariki wiki jana akarushwa sana kwenye mitandao ya kijamii.
Huyu bwana ana kampuni kubwa sana ya Ulinzi pale Morogoro inaitwa Sengo Security. Tukamfuata ili atusaidie michakato ya kupata vibali vya vijana wetu kuruhusiwa kubeba silaha.
Hii ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuonana na nguli huyo na nilijifunza vingi sana toka kwake. Mara ya pili kufanya nae kazi ilikuwa mwala 2017 kwenye uchaguzi wa marudio Kata ya Kiwanja cha Ndege. Diwani wao Godi Mkondya alifariki.. mpwa akasema anautaka udiwani, na si udiwani tu bali Unaibu Meya na hatimaye 2020 Umeya kamili.
Mpwa akaniomba 'nichore mchoro'… mchoro ukachorwa, asubuhi tu saa nne tukatangaza ushindi.
Sasa kipindi kile niko chuo, nguli huyu kwa muda wa siku tatu akatupitisha kwa kila Idara zinayohusika kwa ajili ya vibali na leseni... lakini mwishowe mimi na mwenzangu tukafikia hitimisho kwamba haiwezekani kwa haraka hivyo tupate hivyo vibali.
Wanasema shida mgunduzi… ndio tukaja na wazo la Morani Security. Tuchukue vijana wa kimasai pekee wawe wanalinda na silaha zao za jadi wakiwa ndani ya mavazi yao yale ya asili.
La haula. .Wale wazungu walikoshwa roho kweli kweli na wazo hilo jipya.
Najaribu kusemaje.?
Waona hapa kwetu ni namna ni ngumu kweli kweli na mlolongo mrefu wenye urasimu kupindukia ili kupata leseni na vibali kwa vijana wa kampuni za ulinzi kubeba magobore tu (kama ndio unaanza) pengine kutokana na mazingira ya utete wa nchi zetu hizi..
Lakini wenzetu huko magharibi watu wanamiliki sio tu 'kampuni za Ulinzi'bali wanamiliki 'private military'.
Mara kadhaa kwenye makala hii nimetaja 'private military', nikiongelea private military kichwani usidhani kwamba labda ni kama hizi kampuni za ulinzi kama za kina Sengo. Hawa wa magharibi ninaowaongelea ni majeshi kamili yaliyokamilika ila hayako chini ya umiliki wa nchi.
Yamekamilika katika namna kwamba wana kambi zao kabisa za kijeshi, wana vyuo vyao vya mafunzo, wana ndege za kivita, boti za kivita, makombora, magari ya kivita, idara za intelijensia n.k.
Yaani ni jeshi kamili kabisa ambalo limekamilika lakini haliko chini ya nchi, linamilikiwa na watu binafsi.
Naam, kuna viti hawawezi kumiliki… silaha kama ICBM au nuclear warheads, biowepons… lakini majeshi haya ni majeshi kamilo kabisa. Wanaweza kuchakaza kabisa nchi zetu hizi za ulimwengu wa tatu kwa wiki tu.
Utamu zaidi majeshi haya binafsi mara zote wanaajiri watu toka majeshi ya serikali ambao wametumikia kwenye vikosi vya weledi kama vile Navy Seals, Delta, Rangers, Marine RECON, Air Force ST n.k. yaani wana ajiri wanajeshi ambao walikuwa 'cream' kwenye majeshi ya serikali.
Ndio maana majeshi haya binafsi PMC yamekuwa kiungo adhimu kwenye vita zote ambazo unaona Marekabi anapigana.
Kwa hiyo mara zote nataka ukiona naongelea majeshi binafsi pale Marekani ujue naongelea kitu adhimu na cha weledi wa kiasi gani.
Maana yawezekana wengine waliwaza iliwezekana vipi "ultimate security" wenye magobore wamlinde Obama siku ile ya April 30.
Hawa watu, PMC ni watu wa weledi wa juu kabisa lakini hawako chini ya serikali jambo ambalo huku kwetu haliwezekani abadani.
Sasa,
Yule jamaa pale kwenye picha Situation Room ni nani??
Tuanze kuunga nukta alafu tuelewe ni kwa jinsi gani Deep State inaendesha ulimwengu itakavyo.
Nakutambulisha kwa mtu adhimu mno anaitwa James Steele.
Siku ambayo picha hii inapigwa, yaani May 1, 2011.. kumbukumbu zinainyesha kwamba James Steele alikuwa ni CEO wa Kampuni inayoitwa Buchanan Renewables Energy (BRE).
Unajui hii kampuni iko wapi?
Uarabuni? Hapana..
Marekani? Hapana…
Ulaya? Hapana…
Kampuni hii ya Buchanan Renewables Energy Makao makuu yako 'barazani' kwetu hapa hapa Africa nchini Liberia.
Kwa mujibu wa taarifa zilizo kwenye tovuti ya kampuni hii (kipindi cha mwaka 2012 kurudi nyuma) wanajieleza kwamba wanazalisha umeme kwa kutumia biomass ya miti mikuu kuu ya mpira.
Sasa nianze kwa kukujuza mapema kabisa… kampuni hii ni 'front organisation' ya shughuli za ujasusi na waliingia pale Liberia miezi michache tu baada ta vita ya wenyewe kwa wenyewe kumalizika.
Nisizunguke sana… nikueleze, huyu James Steele ni nani? Hawa BRE walikuwa wanafanya nini Liberia… kisha tutaelewa kwa nini wengi tunaamini yule bwana mwenye suti nyeusi na tai jeupe ambaye haonekani kwenye picha ni James Steele.
Kama haujasoma simulizi yangu ya Geranimo nakushauri uisome maana kama haujaipitia kwente hivi vitu ambavyo naenda kuelezea hapa baadhi naweza kukuacha Chalinze..
Hapa nitawaeleza wote wawili kwa pamoja… kampuni ya Booz Allen na James Steele ili tusiache kipore chochote.
Ni kwamba..
Karibu nusu ya Intelligence Bugdet ya Marekani inaenda kwa makampuni binafsi ambayo vyombo hivi vya intelijensia vina 'out-source' shughuli na huduma muhimu toka kwao. Fahamu kwamba, mfano kwa mwaka huu 2020 Marekani wanatumia dola bilioni 62 kwa ajili Idara za Intelijensia za 'kiraia' (mfano Central Intelligence Agency CIA, National Security Agency NSA, Bureau of Intelligence and Research INR, Central Security Services CSS na kadhalika).
Pia Marekani kwa mwaka huu inatumia zaidi ya dola bilioni 23 kwa ajili ya idara za intelijensia za jeshi. Kwa hiyo wa jumla ya karibia kama dola bilioni 100 (kama Shilingi Trilioni 230 za Kitanzania) kwa ajili ya Intelijensia tu.
Sasa nusu ya hii bajeti ya intelijensia inakuwa out-sourced nje kwenye makampuni binafsi. Na papo hapo kwenye hiyo nusu ya bajeti ambayo inaenda kwa makampuni binafsi asilimi sabini (70%) inaenda kwa kampuni ya Booz Allen.
Sasa, ni huduma gani hasa Idara za Intelijensia za Marekani wanazipata toka Booz Allen.?
Hawa Booz Allen ni kama "CIA" inayojitegemea binafsi.
Yaani waona pale juu nilieleza juu ya uwepo wa majeshi binafsi PMC kama vile Triple Canopy na Blackwaters… sasa hawa Booz Allen wenyewe ni kampuni inayojihusisha na masuala ya ukusanyaji Intelijensia na Ujausi lakini hawako chini ya serikali.. inamilikiwa na watu binafsi.
Kwenye tovuti yao hawa Booz Allen wanajipambanua kama kampuni ya "Management and Information Technology Consulting Firm". Lakini hawa mabwana wana mkono wao kwenye karibia kila tukio kubwa unaloliona linatokea.
Yaani ni kama vile hapa Tanzania tuna Usalama wa Taifa pale Oysterbay… alafu papo hapo kuwe na kampuni fulani iko pale Victoria iwe yenyewe inafanya kazi kama ya Usalama wa Taifa lakini hawako chini ya serikali.. wanajitegemea.
Unaweza kujiuliza ni kwa namna gani serikali inaweza kuruhusu kuwe na kampuni ya namna hii?
Sababu ni kwamba kuna shughuli ambazo serikali hawawezi kuzifanya inabidi watu toka nje ya serikali wazifanye.
Nikupe mfano mdogo tu…
Unakumbuka lile sekeseke la Arab uprising?
Lile vuguvugu la mwaka 2010 na 2011 wananchi wakipindua serikali zao kwenye nchi za Kiarabu??
Tunaendelea..
Sent using
Jamii Forums mobile app