Ingawa posti yako
Mkuu Trimmer Ahsante kunivuta shati. Academically ndivyo itakiwavyo.
James J. Angleton. Kama binadam wote tulivyo mapungufu hayakosi hakuna aliekamilika. Huyu Mzee Hana sifa nzuri Marekani kwa wanafuatilia. Nafasi aliodumu nayo ya Jasusi Mkuu wa Counter Intelligence, nafikiri inahitaji hekima ukizingatia Mamlaka ya Top CI officer kifedha (bajeti yake Ni ile inayoitwa blank check andika numba mwenyewe), amri, watumishi, teknolojia na muundo wa taasisi alioyotumikia CIA. Kwa uchache alikua na nguvu nyingi kiasi akataburi na pia alikua mkurupukaji. Mambo mengi ya hovyo aliyafanya bila hata kupewa ruhusa na Taasisi au Kamati zilizowekwa Kuitazama CIA. Na Ndio kilichopelekea William Colby Director wa CIA kumfukuza kazi Desemba 1974. unaweza kugoogle "who fired James Angleton" kupata hii habari. Nitanukuu sources zangu mwisho wa Mantiki au repoti hii. Ni-ukurupukaji wake ambao Umeigharimu Africa Viongozi mahodari na maisha kama yalivyo. Ukizingatia Mauaji ya Patrice Lumumba 1961, kupinduliwa kwa Kwame Nkurumah 1965 wote wawili bila James hajapewa ruhusa na Wala hawakua na Nia mbaya na Marekani. Nkurumah graduated from Massachusetts Institute of Technology, kukamatwa kwa Nelson Mandela 1962 makaburu washashindwa kumnasa Mandela akiwatoka all the times, Hadi walipopata zawadi toka CIA.
Operation/Project MKULTRA au kwa kina lingine Mind Control Program. Ni jitihada zilizoanzishwa kabla James Angleton hajaaza kazi. Marekani waliitwaa toka kwa Wanazi Ujerumani ya Adolf Hitler baada ya Kushinda Vita 1945. Nazi Ndio walikuwa wakifanya experiment ya binadam. Baada ya vita Marekani ikachukua Wanasayansi na kuwapeleka Amerika. Kwa hiyo MK ULTRA ikaendelezwa, Jeshi wakawapa CIA (inawezekana waliona ni upuuzi si unajua majeda hawapotezagi muda). Hata hivo haikufanikiwa, iliishia kuua wamarekani wawili na kilichobaki Ni mbinu za kutesa watu. Lakini, Mzee Angleton aliing'ang'ani kwa Siri hadi iliposhtukiwa na kufishwa. Soma kitabu Operation Paperclip by Anne Jacobsen.
Operation MKCHAOS, ambayo ilianzishwa chini yake, ndiyo iliokua kijipu uchungu Hadi Akatumbuliwa baadha ya New York Times kufichua Siri ambapo Bunge ikabidi wafanye uchunguzi ukiongozwa na Seneta Frank Church na kugundua madudu Ya CIA ikiwemo kifo cha Lumumba, chaos, na kadhalika. William Colby akamtumbua.
CHAOS ilikua Ni program ya kuchunguza raia wa Marekani Activists. CIA ilikua haturuhusiwi kufanya kazi yake ndani. Hadi wapate ruhusa. Basi kwa hii CHAOS wenye maroho mabaya ndo wakapata Sababu ya kugandamiza wanyonge hasa hasa Black Americans ambao walikua Wanapambana juu ya Ubaguzi wa rangi (Ukaburu) enzi za miaka ya sitini 1960s kwa kuwa Neutralized ikiandikwa hivo ujue Ni kuwadedisha. Imprisoned, public humiliated, na Mashtaka ya uongo, katika walikumbwa na UHANDISI JAMII wa Bwana mkubwa ni Mchungaji Martin Luther King Jr, Fred Hampton, Mark Clark, Zayd Shakur, Gerenimo Pratt (Vietnam Green Barret) ambae nadhani kazikwa Arusha Tanzania 2011. listi Ni ndefu Ikiwemo Mumia Abu Jamal
Pia Kuleta Mara kibao tani na tani za Cocaine na Opium kutawanya mitaani hasa mitaa ya Watu weusi
KWA HIO UKISIKIA "UHANDISI JAMII" NDO IVO Wakuu. Baadae Wakawa wanagawa Bunduki kwenye mitaa ya Black Amerika. piga esabu. Mwanangu, Vijana Weusi wasiraruane kama machizi kwa nini
Skando yake nyingine ni failure ya Operation Bay of Pigs Cuba 1961. alikusanya wakyuba karibia 1500 wakafundishwa kutumia silaha na mbinu kidogo wakapewa vifaa na kushushwa sehemu inayoitwa Bays of Pigs (ghuba ya Nguruwe). Castro kashitukia ngoma wote mbaroni. Aibu kubwa. Na kilichoteka baadae hakiwezi kusahaulika. Hadi leo Amerika haivamii cuba Ni maili 280 tu. Matokeo ya ukurupukaji wa Mzee James
Yani kwa kifupi kwa navoona kwa rekodi nafikiri Aliiathiri Taasisi ya CIA kuliko kujenga. na inawezekana alipata kazi Sababu baba yake aliwahi kuwa stesheni chifu Italy. Ukiritimba upo Kila sehemu.
Angleton sie Aliebuni mbinu za hadaa. Mtu alitoa mbinu za hadaa anaitwa JOHN MULLHOLAND aliekua mfanyaji Mazingaombwe kabla ya afisa wa CIA. Yeye Ndio alietunga kitabu Cha Ujanja na Upotezaji) Manual. (Trickery and Misdirection). baadae kikaitwa Kitabu Cha Ujanja na Hadaa (Trickery and Deception). Sasa ikiwa bwa mzee alibadilisha jina la Manual sidhani inampa wadhifa wa Mtungaji.
Ok Kuhusu shehe Ponda. Shehe sio gaidi Wala hahusiani na magaidi wa aina yoyote.
Ponda umaarufu wake umetokana na kukutetea Mali za Waislam ambazo zinahujumiwa na Waislam hao hao waliomo ndani jumuiya yao. kiwastani anatetea haki za kukatiba ya nchi. mfano. Yusuf Manji aliwazuga Viongozi wa kiislam Wamuuzie prime land Mali kinyume Cha sheria Kama alivonunua Bahari Beach Zanzibar. au angetakiwa kutokana na Elimu yake ajue,. nafikiri Ana MBA. Sasa Sheikh Ponda akang'amua na akafanya watu wote hata wasio waislam wajue dhuluma hii (Advocacy). Huyu shehe alekamatwa Italy yeye ngoma yake umeiyona? malengo yao tofauti na visa vyao tofauti. Mtu asiemjua Ponda akisoma mfano ule basi atadhani Ponda gaidi au anata Serikali ya kidini. Hakuna Mtanzania mwenye akili hiyo. Ponda anatetea haki za kikatiba. Soma Katiba ujue haki za Raia. Serikali inakumbushwagwa mjomba na ndo wajibu wa raia. Mchungaji wa Southern Babtist Church Nobel Peace Prize Winner Martin Luther King Jr. alipokua jitahidi kuomba usawa dhidi ubaguzi wa Rangi, James J. Angleton alimuona Kama anahatarisha Amani.
Kwa Waafrika sio tu Usingetakiwa Usimsifie kabisa. Ikiwa wewe sio Mwafrika, I understand. Na Kama ni cut and paste hapo pia I can understand
Ndo maana wanzio wanakuuliza habari umepata wapi. huandiki source ilhali most materials are in public Domain. Yani sio Tena Siri.
bibliography
FIRED DEC. 1974
Documents Reveal the Complex Legacy of James Angleton, CIA Counterintelligence Chief and Godfather of Mass Surveillance/
OPERATION MKCHAOS
Documents Reveal the Complex Legacy of James Angleton, CIA Counterintelligence Chief and Godfather of Mass Surveillance/
HE WAS INSTRAMENTAL ON ASSASSINATION OF PATRICE LUMUMBA, MLK, BLACK NATIONALIST
James Jesus Angleton, the spy whose nightmares propelled the Cold War — Coorabell Ridge
KUMPINDUA KWAME NKURUMAH FEB. 1966. BILA KUIDHINISHWA NA TAASISI HUSIKA. TAYARI TAASISI SIMAMIZI TAYARI ZILIKWISHA KATAA WAZO LA KUMPINDUA
C.I.A. Said to Have Aided Plotters Who Overthrew Nkrumah in Ghana
Four more ways the CIA has meddled in Africa
DRUGS TO AFRICAN AMERICAN LOS ANGELES AND THEN GUNS
Allegations of CIA drug trafficking - Wikipedia
MKULTRA CIA MIND CONTROL PROGRAM
KILLED AT LEAST TWO AMERICANS
Inside the Archive of an LSD Researcher With Ties to the CIA’s MKUltra Mind Control Project/
SOMA KITABU BY ANNE JACOBSEN
OPERATION PAPERCLIP
Operesheni ya Marekani Kuchukua wanasayansi wa Nazi Germany baada ya Kushinda Vita