COVID-19 & DEEP STATE: Nini maana ya Uhandisi Jamii unaotokea Duniani!?

COVID-19 & DEEP STATE: Nini maana ya Uhandisi Jamii unaotokea Duniani!?

"Tarehe 26 January mpaka tarehe 25 February mtumiaji wa device hii ilionekana kwamba alikuwa nchini Kenya kwa muda wa mwezi mzima. Naam, Kenya hapa hapa 'nyumbani'.
(Aambapo Tarehe 11 January mtumiaji wa Device hii alisafiri kwenda Dubai na kisha kurejea tena Kenya)."

Kenya mpo??
 
It might be..

There must a hidden political agenda over the on going 12th straight day protesting against police brutality..[emoji848]

Even american knows; see the attached pic with comment on Deep State..

Hii comment nimekutana nayo leo nikiwa naperuse news Dailymail..

Huyu jamaa akitoboa November ni bahati sana.

US Top profiled politicians wemshaanza kuonyesha mwelekeo wao kuwa hawatamuunga mkono Trump..kama Bush, kina Romney, Obama .

Sasa jiulize Republican kama Bush wanamgeuga jamaa [emoji23][emoji23] Tena katika kipindi hiki yaani ..

Mzee wa Ku~Tweet ana kazi sana [emoji23]View attachment 1470898
Mitty Romney hajawahi kumunga mkono Trump, Obama ni Democrat kindaki ndaki. Kuhusu Bush sijui, ila hongera kwa ku-peruse the Dailymail mkuu. Muda huo mi nlikuwa na-peruse page ya Kigogo Twitter
 
Hatimaye tumefika Ijumaa kwa ajili ya Episode Mpya...

Baadae kidogo nitaiweka hiyo Episode ila kwanza niwashukuru kwa wote ambao mmenitumia hii inbox maana ningechelewa sana kuiona hii tweet.
(Nimeambatanisha screenshot ya tweet hapo chini)

Kwa wale ambao hawamfahamu huyu aliye-tweet hii habari ni Kenneth Roth ambaye ndiye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Haki za Binadamu Duniani (Human Rights Watch).
Huyu bwana pia ana ufahamu mzuri sana wa masuala ya siri na sarakasi za ulimwengu uliojificha sababu huyu muheshimiwa enzi za utawala wa Rais Regan wa Marekani, ni yeye huyu Kenneth Roth ambaye alikuwa 'federal prosecutor' kwenye skandali maarufu ya Iran-Contra ambayo mpaka leo tunaihesabu kama moja ya skandali kubwa na mbaya zaidi kuwahi kutokea ulimwenguni.

Kwenye haya maoni yake anapita mule mule kwenye "telemetry data" ambako tumekuwa tunachambua kwa Episode kadhaa sasa. Hivyo naamini sasa tunaona umuhimu na upekee wa taarifa ya MACE na wasiwasi wa vyombo vya intelijensia kwamba kuna jambo ambalo si la kawaida lilitokea mapema kabisa mwaka jana mwezi wa kumi kwenye maabara ya Wuhan Institite of Virology.

Stay tuned kwa Episode mpya... nitaiweka baadae kidogo nikiwa nyumbani nimetulia.
Screenshot_20200611-083206_Twitter.jpeg
 
Bold asante mkuu story zako sio tu story kwa ajili ya kuburudika bali pia ni mwanga ktk kuijua dunia tunayoishi, ni halali tu ukichelewa kupost japo wengi tunalalamika hadi kutishia kuandamana (jokes) lakini haya madini mkuu hata google mengine hayapatikani labda deep web na staki kujua huwa unazipata wapi hizi info ila nikuambie tu usichoke usichoke kutuelimisha hata kama "tutakutukana" kiasi gani just keep it up, naamini tupo wengi sana nyuma yako tunaozikubali kazi zako na hatucomment chochote kuliko haters wanaopenda kucomment offenses juu ya kazi zako. Ubarikiwe mkuu.
 
Pamoja sana chief..
Bold asante mkuu story zako sio tu story kwa ajili ya kuburudika bali pia ni mwanga ktk kuijua dunia tunayoishi, ni halali tu ukichelewa kupost japo wengi tunalalamika hadi kutishia kuandamana (jokes) lakini haya madini mkuu hata google mengine hayapatikani labda deep web na staki kujua huwa unazipata wapi hizi info ila nikuambie tu usichoke usichoke kutuelimisha hata kama "tutakutukana" kiasi gani just keep it up, naamini tupo wengi sana nyuma yako tunaozikubali kazi zako na hatucomment chochote kuliko haters wanaopenda kucomment offenses juu ya kazi zako. Ubarikiwe mkuu.
 
DEEP STATE, COVID-19: Nini Maana ya Uhandisi Jaamii Unaotokea Duniani?





#14



Tunaimaliza hii ili tuanze Deep State. Kuna angle tukiziingia hapa kwenye makala hii tutarudi kule kule ambako baadhi walikuwa wanasema hawaelewi.



Sasa,


Ile Device ambayo ilikuwa imeonekana ikitumika mara kadhaa Kenya, Beijing, Dubai na baadae kuibukia Wuhan katika kipindi ambacho kuna ushahidi kwamba kituo cha utafiti cha WIV kilifungwa ina tupa kiashiria gani?



Mara ya mwisho kwenye mfululizo niliacha swali… ni jambo gani lakujia ukiona mtiririko wa mahala ambako mtumiaji wa ile Device alionekana kutembelea?
Umepata jawabu?
Kama haujapata, sitaki kukupa jawabu kwa urahisi, endelea kusoma hapa…


Hiki kitu (data) ambazo MACE walikuwa wanakusanya kama ambavyo nimekuwa nazichambua kwa Episodes kadhaa sasa, kwenye ulimwengu wa ushushushu twaitaje hii?
Hii ndio yaitwa "Signal Intelligence"… sababu ndani ya Signal Intelligence kuna 'Communications Intelligence na Electronic Intelligence'. Kada hizo mbili za ujasusi kwa pamoja ndio twaziita Signal Intelligence.

Sasa kuna nchi kadhaa ambazo zina makubaliano kwa zaidi ya miaka hamsini sasa kushirikiana kubadilishana intelijensia za "signal".
Mkataba huu ulianza hasa miaka ya 1940s ambapo ulianza kama UKUSA ambayo yenyewe ulikuwa ni ushirikiano wa kiintelijensia kati ya Marekani na Uingereza. Baadae zikaongezwa nchi za Canada, Australia na New Zealand na kufanya jumla ya nchi tano chini ya mkataba huu wa Ujasusi ambao kwa sasa ushirikiano huu wa kishushushu tunaufahamu kwa jina la "THE FIVE EYES".
Kama umewahi kusikia habari kuhusu masuala ya Mtandao wa 'Stoneghost' basi mtandao huo wa kiintelijensia uko chini ya hii 'THE FIVE EYES'. Nadhani mwaka jana niluwahi kuandika kidogo kuhusu hili suala.

Sasa, nchi hizi ambazo ni washirika wa "THE FIVE EYES" sababu ya ushirika huu wakashirikishwa na idara za Ujasusi za Marekani kuhusu uchunguzi ambao ulifanywa na MACE juu ya mwenendo wa kutia shaka wa kituo cha Wuhan Institute of Virology. Na hapa ndipo unapokuja uadhimu wa suala la 'intelligence sharing'. Sababu wewe waweza kuwa na kipande kimoja tu cha fumbo na mwenzako ana kingine ambapo na mkiviunganisha mwaweza kutegea kitendawili lakini kama mtu angebaki na kipande chake kamwe abadani msingetegua kitendewili.

Hizi nchi ambazo twaziita "The Five Eyes" wana namna maalumu ya kushirikishana hizi intelijensia. Ndio kuna huo mtandao wa 'stoneghost' pia kuna kitu chaitwa 'intelink-C'. Pia kuna mwongozo wa idara gani za ujasusi ambazo ndizo mahusui zinahusika na ushiriki huu wa kubadilishana intelijensia. Nishawahi kueleza vitu hivi huko nyuma kama kuna ulazima basi nitaeleza tena wakati mwingine siku za usoni.

Sasa, pale Australia wana idara ya Ujasusi inaitwa ASIO (Australia Security Intelligence Organisation). Kuielewa kwa urahisi shughuli zake unaweza kuifananisha na idara kama vile MI5 ya Uingereza au FBI ya Marekani.
Sasa hii ASIO walikuwa na taarifa za kutosha zaidi kuhusi wanasayansi muhimu ndani ya kituo cha WIV sababu wanasayansi hao kipindi wanafanya masomo ya fani zao waliwahi kufadhiliwa na shirika linaloitwa CSIRO waende wakajionoe zaidi kwenye tafiti za Kisayansi huko Australia.

Kwa mujibu wa idara ya Ujasusi ya Australia ya ASIO wanathibitisha kwamba Dr. Shi Zhengli, Dr. Peng Zhou na Dr. Huan Yan Ling kwa nyakati tofauti toka mwaka 2006 mpaka mwaka 2015 wamekuwa kwenye maabara za Level 4 (BSL-4) za nchini Australia kwa ajili ya kujinoa katika tafiti za virusi.

Huyu Shi Zhengli mpaka sasa hivi ninapoandika yeye ndiye anasimamia kurugenzi ya 'Emerging Infectious Diseases' pale kwenye kituo cha WIV.

Kwa miaka mingi tangu alipoenda kujinoa nchini Australua Dr. Shi amebobea kwenye kutafiti "SARS-like coronaviruses"yaani virusi bya corona vyenye kufanana na SARS.
Fahamu kwamba SARS iko kwenye kundi moja la mfanano wa RNA na virusi vya MERS na COVID-19.
Yaani kwamba virusi viko vya aina nyingi. Kwa mfano kuna virusi kwa pamoja vyaitwa "retroviruses" ambavyo vyenyewe tofauti yake kubwa ni vile kwenye mzunguko wake wa maisha kuna muda muundo wake unakuwa na DNA (mfano kama virusi vya HIV-1 na HIV-2) ambavyo kwenye classification viko kwente Group VI ya Baltmore Classification. Wakati kwa upande huu mwingine tuna hizi 'RNA Viruses' ambavyo vyenyewe genetic material yake ni unyuzi mmoja (single stranded) wa RNA (ssRNA) na hata pale ambapo baadhi yake vikionekana na 'nyuzi' mbili huwa si DNA bali ni 'double-stranded RNA' (dsRNA). Virusi hivi vyenyewe viko kwenye group la III, Group IV na Group VI ya Baltimore Classification.

Nimesema haya ili kuelewa sawa sawa kile nilichosema pale juu kwamba Dr. Shi alikuwa amebobea kutafiti "SARS-like coronaviruses".
Ripoti ya Idara ya Ujasusi ya ASIO inazidi kueleza kwamba masomo haya ya hawa wanasayansi wa China ambao walipelekwa huko kwa programu maalumu inayosimamiwa na shirika la CSIRO walikuwa wanatafanya kwenye kituo cha 'Australian Animal Health Labaratory' ambako kuna maabara ya Level-4 ( BSL-4).


Taarifa ya ASIO ambayo imewasilishwa kwa "The Five Eyes" inaonyesha kwamba wanasayansi hawa wa China wakiwa pale Australia 'foundational research' ambayo waliifanya ilihusu 'deadly pathogens in live bats' (tafiti kuhusu vijidudu viwezavyo kusababisha kifo/madhara makubwa ambavyo vyapatikana kwenye popo (utafiti wao waliufanya kwa popo walio hai)).
Hiyo ni ilikuwa mwaka 2006 wakiwa wanajionoa kwenye maabara ya Australian Animal Health Labaratory.

Katika kuchunguza zaidi, idara ya Ujasusi ya Austtalia ASIO wakagundua kwamba baada ya Dr. Shi na wenzake kurejea China waliendelea na tafiti hizi (virusi vya corona vyenye kufanana na na Virusi vya SARS).
ASIO wanaeleza kwamba kati ya mwaka 2015 mpaka 2017 Dr. Shi na timu yake walikuwa wanafanya tafiti kwa popo kwenye mapango yaliyoko jimbo la Yunnan hapo nchini China. Katika tafiti hizi ASIO wanasema kwamba Dr. Shi na timu yake waliweza kupata sampili zipatazo 50 ambazo ukizilinganisha 'sequence' zake zinafanana kwa asilimia 96% na sampuli ya Covid-19 ambayo inaisumbua dunia kwa sasa.

Hivyo kwa muda wote huo toka 2015/2017 mpaka 2019 Dr. Shi na timu yake wamekuwa wakifanya synthesis ya virusi hivi ambavyo kuna uwezekano mkubwa walitumia kuunda virusi vya Covid-19.

Sasa hapo ndio mvutano unakuja…


Taarifa rasmi ya WHO inadai kwamba wanasayansi wamefanya utafiti kwa virusi vya Covid-19 na kuisoma 'sequence' yake na kufikia hitimisho kwamba kwa 'sequence' ya DNA ya Covid-19 haiwezekani kuundwa maabara. Kwamba namna pekee ya 'sequence' hiyo kutokea ni njia ya asili (kwamba kirusi kimetoka kwa mnyama na kurukia kwa binadamu).
Lakini ukakasi unakuja ni kwamba taarifa hii (utafiti huo) imetolewa na WHO wale wale ambao mwezi wa kwanza tu walituambia kwamba wamefanya utafiti na kugundua kwamba kirusi cha Covid-19 hakiwezi kuambukizwa toka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.
Tunaweza kuwatetea kwamba WHO walitulisha hilo 'tango pori' hilo sababu labda kwa kuwa kirusi kilikuwa kipya na isingewezekana kukifahamu kwa muda mchache.
Lakini.. hapana! Hilo sio tatizo… tatizo ni kwamba WHO wamekuwa wanatoa taarifa kwa ulimwengu kuhusu Covid-19, taarifa ambayo wamelishwa kwao na China. Hawafanyi uchungizi wao binafsi. Hilo tatizo kubwa… na ndio maana kila taarifa kubwa ambayo wanaitoa kuhusu Covid-19 baadae inakuja kuthibitika kwamba ni urongo. Loh.!!

Tuache hapo.. turejee pale kwa Dr. Shi.

Kwa hiyo kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya Ujasusi ya Australia ASIO ni kwamba watafiti hawa Dr. Shi na wenzake baada ya kupata sampuli zipatazo 50 za virus toka kwa popo kwenye mapango jimboni Yunnan hapo China ambazo zina mfanano wa asilimia 96% na virusi vya Covid-19 tulivyonavyo sasa ambapo tangu mwaka 2017 Dr. Shi na timu yake wamekuwa wakitafiti virusi hivyo katika maabara ya level-4 iliyoko pale WIV (ni kipindi hicho pia wakaomba kupandisha hadhi maabara ya WIV kutoka BSL-2 kwenda BSL-4).
ASIO wanashuku kwamba kuna uwezekano Dr. Shi na timu yake walifanya synthesis kuunda virusi vya Covid-19 (ambapo si kosa wao kuunda virusi hivyo sababu kwenye hizi maabara za ngazi ya BSL-4 duniani kote kuna virusi vingi na vya hatari mno vingine hatari kuzidi hata Cibid-19 vinahifadhiwa… kosa ni namna gani virusi hivyo vimeingia kwa jamii?? Kuna 'ajali' ya kisayansi ilitokea pale maabara? Au vilivujishwa makusudi? Au viliibwa?)

Wapaswa kufahamu kwamba Dr. Shi na WIV hawakatai kuchukua sampuli za Virusi kule mapangoni wanachokataa ni kwamba waliunda kirusi hiki kilichozua kizaa zaa duniani.
Ubaya ni kwamba kuna ushahidi mwingi kuthibitisha kwamba kauli yao si ya kweli.


Let's back up a little bit… turudi nyuma kidogo…


Hapo juu mwanzoni nimeeleza kwamba wanafunzi ambao walipewa ufadhili na CSIRO kwenda kujinoa kwenye tafiti za virusi nchi Australia mwaka 2006 walikuwa ni Dr. Dr. Shi Zhengli, Dr. Peng Zhou na Dr. Huan Yan Ling.
Hawa wote waliporejea China wakaajiriwa Wuhan Institute of Virology.
Si hivyo tu, katika ule utafiti na synthesis ya sampuli toka mapangoni ambao ulikuwa pale WIV ulikuwa unaongozwa na Dr. Shi pamoja na Dr. Huan Yan Ling ambao walisoma wote Australia kwa ufadhili wa CSIRO.

Lakini katika uchunguzi wao idara ya ASIO wakagundua jambo la ajabu sana na la kutia shaka… kwamba tangu mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana 2019 mpaka leo hii huyu Dr. Huan Yan Ling hajulikani mahala alipo na 'profile' yake kwenye tovuti ya WIV imefutwa.
Tuelewe… hapa simuongelei yule daktari wa kwanza wa China aliyerekodi video iliyosambaa duniani kuhusu corona mwezi January alafu serikali ikampoteza, wala simuongelei yule mwanahabari wa China ambaye naye alipotezwa baada ya kuanza kuripoti kuhusu uhalisia wa Corona ndani ya China… hapana siongelei hao. Huyu ninayomueongelea hapa ni mwanasayansi mwajiriwa wa kituo cha Wuhan Institute of Virology na moja ya manguli wao wa tafiti za virusi. Hajulikani yuko wapi na profile yake kwenye website ya WIV imefutwa.

What happened?


Hapa ndio twapata mwanga na jawabu kuhusu zile safari na ile device ambayo ilikuwa imeonekana WIV lakini pia imeonekana Kenya, Dubai na Beijing.


Nitaeleza…



Habib
To infinity and Beyond
20200610_154558.jpeg
 
Idara ya ujasusi ya Uchina inaitwaje?
Watakuwa teyari wameshampoteza
Nalog off
 
Back
Top Bottom