#COVID19 Covid-19 hii ni vita ya kiroho zaidi kuliko ya kimwili

#COVID19 Covid-19 hii ni vita ya kiroho zaidi kuliko ya kimwili

ukombozi101

New Member
Joined
Sep 3, 2021
Posts
1
Reaction score
0
Kuna kitu hapa, hii ni vita ya kiroho zaidi kuliko ya kimwili.

Kuna video na picha za matukio mbalimbali tutakua tunayajadiri humu kuhusu hili swala na kuzifafanua kwa ajili ya afya ya kwenu, watoto wenu na WAJUKUU wenu.

Vijana wengi hawakubaliani na maamuzi ya wazee na hawana nguvu na mali ya kuwaambia wazee kuwa wanachezewa changa la macho ambalo halotiweza safishwa baada ya mchezo.

Tuweni makini na vita za kizawa, hasa wazee, rangi ya ngozi ni nzito kuliko damu na machine za kutengenezea maji.

Wazee chonde chonde msituuze vijana wenu kama walivyotufanyia wazee wa kipindi kile. Busara haiuzwi.

Tunapoelekea ni vijana tutaogopa hata kuwapeni wajukuu sababu ya uwoga wenu.

Tunachoona vijana ni tofauti na mnachoona nyie ambao mnatumia muda mwingi katika majukumu na kutulea sisi. Sisi muda wakuangalia kwa jicho la tatu tunao ninyi hamna, adui hatakuja na kukupa shikamoo Atakuja utampa shikamoo, sisi tunaowapa shikamoo zinaishia kudharauriwa busara zetu na kumezwa sababu kama ile ambayo tajiri au kiongozi wa dini anapata nayo shida katika ulezi wa wanae. Lakini haimaanishi hatujaona kitu, kitu kilichojificha kwa mitego dhidi yetu Na maongezi yetu.

Ukubwa mali, sio dawa.

Pa kuanza kabla hujakimbizwa na wazungu, au mzungu, asie mungu, tafuta maswali yenye majibu kinyume na unachoambiwa alafu tumia ujasiri kufanya maamuzi, hii dunia sio sehemu Nzuri na unalijua hilo, hasa kwenye maswala yanayohusisha pesa na rangi ya ngozi, maisha ya kuchezewa yapo kuliko unavyodhani. Sio kila chakula unachopewa unakula sababu umeambiwa ule, God doesnt make dogs.

Dunia ikivunjika na mifumo yake huvunjika Pia.

Wazee Wetu ambao kutumia smartphone shida lakini wanawajua watangazaji wa CNN au BBC kimajina usukani hauendeshwi kwa masikio tu.

Laana mnayotusukumia Vizawa vyenu ni nzito haijawahi tokea katika historia ya uwepo wa binadamu duniani Angalau mfungueni dirisha la majadiliano kuhusu maamuzi yenu.

Na Kama ni vita ya ukimya sawa, tumeshindwa lakini tusitoe kafara kushindwa mazima kwa ajili ya kushinda kidogo. Vijana tutawalisha tu msituvunje moyo kwa kutetea kifo tunao tetea maisha sababu mmekikaribia. Haya maamuzi mnayoyafanya bila fikra zetu yatatuhusu Sana sisi na wajukuu zenu.

Elimu ilivunjwa makusudi. Ata madaktari pia elimu yao saa nyingine ni ya kutatanisha, mfano mzuri ni mahusiano ya madaktari wa meno na Biashara ya sukari. Kumbukeni pia janga La sigara, majanga ni mengi sana, lakini yote haya hayapo kwa nia nzuri, na sio kwamba waliohusika wote ni wabaya, ni kwamba walikosa elimu ya kutosha na wakatuchunga Machinjoni badala ya mbugani bila Wao kujua.

Elimu pia inaweza kua kikwazo, endapo hio elimu sio sahihi.

Msikie kizazi Chako akiteketea sababu ya maamuzi yako.

Kumbukeni technolojia nyingi za binadamu huuzwa kama akili ya binadamu ina nguvu kuliko akili iliomtengeneza binadamu na viumbe na mimea, kihistoria kuna maeneo mengi sana hilo swala hua ni kosa la kujutia baadae.

Unafundishwa Subira, sio tamaa ya muda, atakae kuja kukufundisha tamaa ya muda sio.

Kuna Mengi sana hamjajifunza na mmezuiliwa msifundishike, naombeni mtupeni moyo ili tuendelee kuwafungulia kurasa mbali mbali zitakazowabeba na kuwapandisha.

Tumeshindwa kuwasiliana na akili zenu basi Uti wa mgongo wenu Unatuhusu.

Mlipuko wa habari ndio umetutengenezea ngazi.

Tupo tuliotangulia wapo wengi pia watakaofwata, na Tunajua tunapoangukia hapatutaki sababu hatutataka njia zao ziendelee kutuumiza kwa manufaa yao. Tufungulieni milango tuwafundishe jinsi ya kufunga milango ipaswavyo.

Mtulinde, msituangamize.
 
Imekaa vzr, mungu jalia aione akaipasulie pale madhabahuni leo
 
Back
Top Bottom