kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Tanzania sio kisiwa, kila tunachokifanya kwenye mapambano dhidi ya Covid 19 kinavuka mipaka na kuonekana duniani kote.
Ni wazi kuwa sasa tumekubaliana kuwa maambukizi ya COVID-19 yapo hata Tanzania, na kuna wenzetu wameugua, wanaugua na waliokufa na wanaokufa kwa ugonjwa huu. Katika hali hiyo haiwezekani Serikali ikaruhusu watu kusafiri kutoka pembe zote za Tanzania na nchi jirani kwenda kukusanyika Kigoma kwa maelfu kuangalia mpira kwenye kakiwanja kadogo namna ile.
Hii inaonyesha kuwa hii mikakati ya kupiga marufuku mikusanyiko kunakotangazwa na serikali hakulengi hasa kupambana na Covid-19 bali mkakati wa kisiasa tu. Hata mataifa mengine hayatatuelewa kama wakiziangalia picha za matukio yoote ya mchakato wa mechi kati ya Simba na Yanga kule kigoma, lazima watakubaliana na mimi kuwa dhamira ya kuzuia mikusanyiko hailengi kupambana na Covid 19 bali kuna jambo lingine linalozuiwa.
Pale Kigoma watu hawakuchanjwa dhidi ya COVID-19 lakini walibanana sana mitaani na uwanjani bila barakoa wala maji ya kunawa, yaani ilikuwa zero distance na mamlaka zote ikiwemo Wizara ya Afya, Wizara ya michezo, TAMISEMI, Wizara ya mambo ya ndani zilibariki kusanyiko lile litokee na liendelee kama vile hakina corona. Itashangaza kuona polisi wanakamata watu 20 waliovaa barakoa waliokusanyika kufanya mkutano wakati waliruhusu watu 22,000 ambao hawakuwa na barakoa kukusanyika kwa raha kule Kigoma. Ni mjinga tu atakaetuelewa.
Hatuwezi kuwadanganya watu wote kwa kwa wakati mmoja mara zote. Tumsadie Rais katika dhamira yake ya kurudisha mahusiano na nchi za ulimwengu huu, maana wao sio wajinga kama sisi.