Nguruvi3.
Ulipokuwa unatetea kila takwa kuwa HAKI ulikuwa unalinda maslahi ya nani? Sasa unahamisha magoli tena, kuwa kuna Takwa la Kutaka tu, na Takwa lililojengwa katika misingi ya maridhiano na mafungamano yetu. Hiki ndicho nilichokuwa nakuambia, bado ukashupaza shingo yako.
Nilipotetea takwa la haki nilikuwa nalinda maslahi ya wanaotaka chanjo , wanaonyimwa bila sababu za msingi.
Hoja usiotaka na wasiotaka kuijibu watetezi wa 'vita ya uchumi' ni hii;
Mtoto afikishapo miaka 5 mwili wake unachanjo za kutosha nimeorodhesha, kipi kinachunguzwa katika COVID-19?
Kuhusu takwa, hili nilidhani linaeleweka kwamba takwa linalohitajika ni lile lililojuu ya misingi ya ufungamano wetu. Kwamba, kuna takwa la dawa asili basi takwa la chanjo ni sehemu ya haki kama haki nyingine.
Mtu mmoja kwa fikra zake hawezi kufikiri kwa niaba ya watu wote. Hatuwezi kuishi katika udwanzi wa kudanganyana hii ni vita ya uchumi tukiwanyima haki wanaotaka kuzisalimisha nafsi zao kwa hiari na haki zao
Sasa bado nitakufafanulia vema zaidi kuhusu hili, ili usiwe unabebabeba tu mambo usiyotaka kuyaelewa kiundani na kuyasema hovyo kwa watu.....
Nitasema kwasababu kukemea upotoshaji ni sehemu ya msaada kwa jamii.
Hatuwezi kuambiwa Virus wa mapafu wanaondoka mwilini kwa mapambio.
Hatuwezi kuambiwa chanjo inatoka kwa mabeberu wakati mikononi mwetu tukiwa tumebeba Biblia zilizoandikwa na mabeberu. Hatuwezi kukaa kimya tukiambiwa virus wanaotafuna mapafu eti ni vita ya uchumi.
Unapotosha kufikiri Haki haiombwi Bali ni Kudai tu, unajikanganya tena kwa mfano wako wa mwajiriwa na mwajiriwa. Kwamba Nyongeza ya mshahara ni haki yake, wewe unayedaia haki haiombwi unataka mwajiriwa akae katika majadiliano, na mwajiri wake kujadili haki yake!
Haki haiombwi, inadaiwa. Period
Kwanini Asiichukue tu, kwanini Asiidai tu mahakamani kwa sababu ni Haki na haipaswi kuombwa?
Unaweza kututofautishia majadiliano ya mwajiri na mwajiriwa, juu ya nyongeza ya mshahara na maombi ya haki ya nyongeza ya mshahara?
Je, huo unatafakari vema unachoandika au unachojali ni kuwasilisha hisia zako tu hadharani?
Kukaa meza moja kati ya mwajiri na mwajiriwa ni takwa na ni haki.
Si haki au takwa kwasababu tunasema, ni kwasababu imeanishwa katika miongozo yetu ya kijamii chini ya sheria.
Kulipa fedha kwa vyama vya wafanyakazi ni wajibu, lakini wajibu unaambatana na haki . Kazi ya vyama vya wafanyakazi ni kukaa meza moja na mwajiri kujadiliana kuhusu masilahi ikiwemo mishahara.
Ikiwa hakuna maafikiano kuna haki ya mwajiriwa kuchukua hatua zaidi dhidi ya mwajiri, ima kwenda mahakamani au kugoma au kufanya jambo litakalomlazimu mwajiri kurudi mezani. Hiyo ni Haki na haiombwi inadaiwa
Ututusa kwamba haki inaombwa upo Tanzania tu, na kwa haya ninayosoma safari bado ni ndefu.
I can imagine yule 'commoner' sijui upeo wake utakuwaje ikiwa 'at least elite hawajui haki ni takwa si ombi' Sad
Nikujuze tu... Dhana nzima ya HAKI ni Batili, ni KIINI MACHO, ni Upofu....Ndio maana mnapata tabu kuitetea. Mmelishwa Ubatili, mnajivunia hadharani, ni Wanafiki na Wasaliti.
Haki haina ubatili isipokuwa tu inadaiwa wapi. Huko duniani haki ni takwa la mtu, Tanzania ni ombi
Kupata chanjo ni takwa na ni haki, kama ile ya mapambio na kuchemsha nyasi
Serikali kutojishughulisha na kilichomo chumbani, ni hoja ya kitoto ambayo ulipaswa kuionea aibu kuitamka. Hili mdsnganyane wenyewe huko katika harakati za upofu wa kiitwacho Haki.
Ni hivi serikali ina mipaka yake! kuna mambo yapo katika level tofauti kabisa. Kwa wenzetu walioendelea serikali ina miapaka kuanzia serikali kuu, serikali za majiji na na manispaa, serikali za mitaa hadi kwa '' serikali ya mtu'
Kuna mipaka ya maisha binafsi na maisha ndani ya jamii kwa ufungamano wa serikali. Usichanganye
Hoja zote zinaishia katika swala moja, tueleze kwanini chanjo ya COVID-19 inapigwa danadana?
Je, bado unaamini Corona ni vita ya uchumi au umeungana nasi kuamini ni Virus wanaoshambulia mapafu!
Je, bado unaamini uchemshaji wa nyasi ni dawa ya Corona au umeungana nasi kuijali sayansi!
Je, bado unaamini kazi ya serikali ni kuhamasisha mapambio , sala na maombi au umeungana nasi kuamini kuwa imani ni suala binafsi na linaanza na kuishia kwa mtu nyumbani na chumbani kwakwe na si wajibu wa serikali!
Tukatae unajisi dhidi ya akili zetu! tunaweza kufikiri vizuri na kwa mantiki ! Tulipotezwa sasa turudi katika mstari