This fellow has made his way to this debate.
Inasikitisha sana licha ya ukweli kuwa huko nyuma nimeeleza kwa kina vaccine zilianzaje na akina Dr Jenner and Robert K. I don't understand Mlenge hakuelewa nini ! hizi ni effort za nini? Kuna nini nyuma yake?
Here's the thing. He isn't helping anybody and probably he makes things worse. For me people who don't have expertise in medicine should shut up. It is simple as that.
Hiyo video ya #143 imetengenezwa na huyo jamaa ambaye hajui and simply stupid akaisambaza kwa kutojua madhara yake kwa watu na sasa madhara yake ni haya ya watu kusikiliza bila kutafakari.
Nitaonyesha upotoshaji ndani ya hiyo video na upotoshaji wa wanaoisambaza
Ni kweli anachosema kuwa vaccine inatengenezwa kwa virus. Kisicho cha kweli ni kuwa si kila vaccine inatengenezwa na virus hai. Kuna vaccine zinatengenezwa na toxins au stimulant zingine kutoka katika mdudu
Pili si kweli kuwa wanaingiza virus tu mwili hata kwa zile vaccine zinazokuwa live.
Virus zinazokuwa live huwa zinakuwa attenuated, hivyo kusema wanaingiza virus ni kupotosha
Dr Robert Koch ndiye aliyefanya kazi ya culture na kuweza ku isolate sehemu inayohusika na ku stimulate immunity. Kwa maana kuwa si virus mzima anasababisha immunity, ni sehemu tu.
Immunity ni tabia ya mwili kujifunza kuhusu mdudu na kutengeneza kinga.
Dr Jenner alitumia njia ya ku inoculate virus kwa watu wazima ili watengeneze immunity.
Njia hii ilikuwa na tatizo kwasababu kama immunity ni low mdudu alishambulia mwili na si kutengeneza immunity.
Hapa ndipo mwenye video anachanganya mambo
Vaccine zilitengenezwa kwa live attenuated virus kwa maana kuwa wanapunguza nguvu za virus kutoleta madhara kwa watu wenye tatizo la immunity, ili kuupa mwili namna ya kusoma virus huyo siku nyingine akiingia ashambuliwe.
Kwahiyo vaccines zilitengenezwa kwa ''live attenuated organism'' na kuna zingine walitoa sehemu tu mdudu ''toxin'' ili kusaidia immunity.
Uongo!
Vaccine ya Corona imetengenezwa kwa kuzingatia matatizo ya SARS(Rejea bandiko la
Zakumi).
Wanasayansi walibaini kuwa live attenuated pamoja na kupunguzwa nguvu ya virus bado kuna tatizo kwa watu wenye immunity zenye matatizo '' Immune compromised' kama HIV , Cancer, Diabetics, na long term illness.
Ndipo ikaonekana kuna uwezekano wa kutumia RNA na kuleta immunity.
Hii ni technology mpya iliyoku in the making for the last 10 yrs, wanasayansi hakujua kutakuwa na Corona.
Hivyo mwenye video anachanganya vitu, kati ya live attenuated ambayo ni technology ya zamani na hii ya RNA ambayo ni tech mpya.
Kwa mantiki hiyo, huwezi kupata corona kwa vaccine kwasababu kinachoingizwa mwilini ni protein tu (RNA) ya virus si virus kama anavyohorojoa mleta video na wasambazaji wasiojua.