Asante. Hizo vaccines za corona, wanasema ni zinatumia virusi vya
adenovirus; jambo ambalo linatajwa kuongeza hatari ya maambukizi ya VVU. "
Roll-out of an effective SARS-CoV-2 vaccine globally could be given to populations at risk of HIV infection, which could potentially increase their risk of HIV-1 acquisition." --
chapisho kwenye jarida la
Lancet. Hilo unaliongeleaje?
Kwasababu ya misinformation itabidi nirudi kuangalia kama kweli ni kutoka Lancent.
Nilitarajia kusoma mjadala katika British Medical Journal, New England Medical Journal au JAMA! Sijaona
Pili, nikutaarifu kuwa kuna kusoma kwa kusoma na kusoma kwa kuelewa. Hukusoma kwa kuelewa
Mwanzo mwa andiko hilo(kama ni kweli) limeanza hivi '' We are writing to express our concern''
Hapa maana yake kuna watu wameandika kueleza shaka yao hivyo ni maoni yao wala si facts.
Andiko hilo halihusiani na Vaccines zilizopo na ushahidi ni huu
Recombinant- Kwa vaccines zilizopo hakuna recombinants na hapa wameeleza ni katika study phase 1
Walichokiona ni increased risk ya wanaume kupata HIV tena wakieleza risk hiyo kama ile ya kutotahiriwa(uncircumcised).
Nikuache kwanza urudi kusoma andiko ukiwa na key words hizi
Recombinant, Phase 1, Increased risk, HIV acquisitions.
Kuhusu gene-therapy, hizi chanjo zimetajwatajwa kuwa zinatumia teknolojia ya mRNA. Hili nalo limekaaje?
mRNA protein like kama ilivyo DNA.
Kuna uwezekana ikatumika katika gene therapy kwasababu mechanism za gene therapy ni nyingi ikiwemo kutengeneza copy za gene ili kutibu maradhi au mapungufu.
mRNA ni possible kwasababu hii ni messanger RNA inaweza kutoa copy kwa njia nyingi.
Somo ni pana tuachie hapo kabla hujachanganyikiwa
CDC na FDA za Marekani
zimesitisha matumizi ya chanjo ya korona ya Johnson & Johnson. Wanasema, pameripotiwa "...
cases of a rare and severe type of blood clot in individuals after receiving the J&J vaccine. In these cases, a type of blood clot called cerebral venous sinus thrombosis (CVST) was seen in combination with low levels of blood platelets (thrombocytopenia)".
Yes kuna taarifa za AstraZeneca kusababisha blood clot ingawa hakuna uthibitisho rasmi. Hali hii imeripotiwa nchi za Ulaya na Jana kuna taarifa za tatizo hilo kutokea nje ya Ulaya.
Nafuatilia ingawa ''Bundle' za Tanzania zinanyima mawasiliano kutoka hapa Kicheba Muheza na DC , London n.k. Nikipata taarifa nitakueleza
Yes FDA wamerudi mezani baada ya watu 15 kuonyesha serious side effects.
Kwa majuha hii ni mada na washamba waliitumia sana kudanganya watu .
Ni hivi vaccines zinatengeneza katika njia mbali mbali, lakini muhimu ni 'vehicle' ya vaccines.
Hizi ni protein ndogo sana lazima ziwe katika volume fulani kuweza kuwa injected na kuleta
Kila kampuni ina ingredients zake ndiyo maana kuna tofauti ya kuhifadhi. Hizo ingredients zinaweza kuwa na matatizo kwa baadhi ya watu.
Kumbuka, hakuna dawa ambayo ni 100% bila kuwa na makando kando.
Muhimu ni benefit risk ratio ndio utasikia watalaam pale Paris wakisema '' the benefit outweighs the risks'
Kwa nchi za wenzetu maisha ya mtu 1 yana thamani.
Hata kama watu milioni 300 wametumia vaccines ikitokea tatizo ambalo ni 0.0001% bado linafanyiwa kazi kwasababu kwa mtu aliyeathirika ni 100% na lengo ni kuponya
Hawa ni tofauti na washamba wanaosema 'hata wakifa hawatakufa wote'' wasiothamini maisha ya watu
Kwahiyo Johnson and Johnson au AstraZeneca kuwa na side effects ni jambo lililotarajiwa.
Watu wanadhurika na maji ya kawaida yenye PH 7 seuse dawa?
Muhimu hapa ni je, watu wangapi wametumia na nini chance ya watu kauthirika?
Leo kuna mahali wamesema the chances ni 1 in a milllion , kabla sijamaliza mawasilian '' Bundle' ikakata ! nchi masikini hizi
Kwako Mwalimu Kashasha
Nguruvi3 , tuelezee hii ikoje.
Yes utafanya 'sarcasm' etc, lakini maandishi yangu yana prove kuwa sahihi. Nilisema chanjo wapambe wakazogoa leo wamesimama katika viambaza, mbuzi kala mkeka watakalia nini?
Taifa letu limeumizwa sana kwa maamuzi yasiyozingatia sayansi. Leo wanasayansi wanaibuka kutoka katika madema ya kufikiza moshi na kusema eti kuna miongozo ya watu wa misitu, wasafiri wa anga na hata dischargeReal? kwamba haya ni makundi yenye risk? Real!!!
Kundi lisilojua hata priorities ndio kashasha. Ni aibu kubwa sana.
Ni kundi lile lile lililokubali mabanda ya kufukiza huku Maprofesa wakitukuza Togwa na mitindi bila ushahidi
Tunasema hivi, hatuhitaji kamati , tunahitaji Chanjo leo.
Kama unadhani ujanja ni ghali basi jaribu Ushamba!