omutimbasafi
JF-Expert Member
- Oct 17, 2017
- 609
- 771
Binafsi usingizi wa leo usiozidi masaa matatu yani nimeota ndoto mbili za kutisha. Moja imemhusu mfanyakazi mwenzangu ambaye nimeota amefiwa na Baba yake mzazi kwa ugonjwa wa korona. Ubaya wa ndoto hii ni kuwa namtambua huyu mfanyakazi mwenzangu kuwa Baba yake alishatangulia mbele ya haki miaka mingi sana huko nyuma.
Ndoto hii ya kwanza ilikuwa na mazingira magumu sana maana ilihusisha kuzikwa na serikali akiwepo mkuu wa mkoa na eti marehemu anakuja kuzikwa maeneo ya kazini kwetu, imenisononesha sana na kunichosha sana.
Ndoto ya pili nimeitwa na mkuu wa operation ya ulinzi na usalama tukiwa maeneo ya kazi akinambia askari anataka kujiua maeneo ya kazi hivyo tukasaidiane kumshika ili tumpige pingu tumnusuru asijiue. Kwenda kumshika jamaa ananiambia mimi nina familia hivyo siwezi kujiua, wenzangu tuliondoka kumshika naye wakasepa wakaniachia msala peke yangu, mara pa akanirushia shoka na kukimbia.
Wanasaikolojia wabobevu hapa nchini ni muda sasa wa kufanya kazi zenu kuokoa maelfu ya Watanzania ambao wanaweza kuathirika kisaikolojia katika wakati huu mgumu dunia inaoupitia. Watu watakufa wengi kwa hofu, na naunga mkono serikali mbalimbali duniani na wanaharakati tofauti wanaoshauri watu kupuuza baadhi ya taarifa zisizo za ukweli, zinatengeneza taharuki ambayo inaweza kuathiri jamii.